Umeshawahi kukutana na watu (viumbe) wa aina hii?

Askarimtu

JF-Expert Member
Sep 7, 2019
277
185
Nina imani wote ni wazima wakuu!!!

Katika pilika pilika za kila siku za maisha hapa duniani, kuna aina fulani ya watu ambao kiasili sio watu wa kawaida (sio binadamu) na hao viumbe, huzunguka zunguka duniani kwa malengo yao binafsi; hasa kwa malengo ya kiroho zaidi. Sasa nitataja baadhi ya sifa (au matukio) hapa chini, halafu utuambie kama ulishawahi kukutana na visanga kama hivyo.....na pia unaweza ukatuongezea maujuzi...!!! Mara nyingi hupenda kuchukua maumbo ya kiume.

1/ Watu hao ni wazuri sana (handsome men) sana, sana na wana akili sana, lakini huwa hawajulikanagi vyanzo vyao; yaani wametokea wapi, wanaishi wapi, au hata familia yao ni ipi! Watu hao hawazeeki. Miaka itapita tu, akiamua kufa, basi anakufa...akiamua kupotea, basi hupotea tu.

2/ Watu hao ni jasiri sana na hujifanya kwamba kana kwamba hakuna Mungu. Hujifanya hawaamini chochote kuhusu kitu kinachoitwa roho. Hujifanya kuwa wanapenda mno pesa, starehe, na hakuna kitu kinachowasumbua duniani. Huvunja amri zote za Mungu waziwazi ili binadamu waone namna wanavyofanya kwa ujasiri, binadamu wengi hujua labda ndio MAISHA.
(Nimetumia neno '' kujifanya'' ili uwagundue, kwasababu inawezekana ilifika kipindi ukagundua kuwa wanachosema sio wanachomaanisha)

3/ Hujiingiza kwenye nyadhifa kubwa ...just from nowhere. Ikitokea siku akasema anahama au akaacha kazi, basi record zake za kazi hupotea vichwani mwa watu na hata kwenye makaratasi. Mtu wa Mungu tu ndiye atakayemkumbuka. (Nimerudia hii point ili kuonyesha msisitizo tu, inafanana na point namba 1). Mda mwingine hujichomeka au kuchomeka viongozi fulani ili watimize malengo yao.

4/ Hujawahi kukutana na mtu mzima anayependa mazingaombwee?? Au mtoto?? Au kijana?? Na hao watu hudai wamezaliwa na mazingaombwe hayo?? Lakini, hufanya mazingaombwee kwa kufurahisha watu tu na kuingiza watu kwenye ulozi (USHIRIKINA)!

Hujawahi kuona mtu fulani akifika nyumbani kwenu, kunakuwa na mikosi tu??? Akiondoka tu, baraka zinaanza...tena za kumiminika?? Lakini, ujue huyo kiumbe mpaka aondoke, basi ameondoka na kitu, sio burebure.

5/ Watu hao (viumbe hao) hata wanywe bia za kiwanda kizima , hawalewi hata chembe, bali hubakia na utulivu tu. Hupenda masihara hata ya kumtukana Mungu ili watu wacheke tu kwa kisingizio kuwa pombe imeanza kuingia kichwani (kumbe wanajifanyisha).

Hawapendi kabisa watu wenye upendo, watu watulivu, hawapendi watu kabisa watu wa ibada, hujitenga nao na huwasema vibaya sana (japo wao wenyewe hujifanya ni wema na watulivu). Hukuangalia machoni tu iwapo akitaka kuku-manipulate mawazo yako na kuingiza ya kwake, na baadae binadamu hujikuta akisema "Anhaaa...ni kweli, jambo lile ni hivi, nilikosea sanaa...."

6/Iwapo watu hao (hivo viumbe) wakiingia kwenye mwili wa mtu, basi watu hao huharibu watoto wa Mungu kwa kuwafanya wawe wakaidi sana, tasa na wagumba, hufanya watu waanze kupenda tattoos...au kuanza kujiita "bad girl" au "bad boy", na kweli huwa bad kwelikweli, badder hata baddest (worse, worst). Pia hutumia misemo hii mara kwa mara;
- Watu weusi ni wajinga
-Ungechelewa ningekuzaa (hasa kwa wazazi)
-Role model, role model, role model...wangu ni... (humpa credit mtu kwa mabaya..kuwa fulani ni shupavu)
-Ushoga ni haki. Kila kiumbe ana haki ya kuishi jinsi atakavyo...kwasababu kadha wakadha...
-Ishi duniani kabla hujafa, usije ukajuta kuwa hukuishi kwa raha, acha kujibanabana....
-Depopo...depopulation agenda is better ***...
-Mimi ni gemin, leo,aries ...(utabiri wa nyota)...



7/ Watu hao hupenda kulazimisha urafiki. Ukijisikia ndani ya moyo wako kuwa hutaki kuwa rafiki na mtu fulani (yaani roho haitaki katakata)...basi tubu kwanza. Halafu kimbia...kwasababu amekuja kuiba kipawa chako ili akampe fulani aliyeenda kuomba kipawa hicho kwa mganga. Ni mtaalamu wa kusababisha madhara ili atatue hayo madhara kwa hila...! Akiingia kanisani au nyumba yoyote ya ibada, hufanya ishara kubwa tena kinyume na sheria za Mungu, isipokuwa kufufua mtu tu ndio hawezi.

8/ Watu hawa hujua siri zako mpaka za ndani kabisa, na huweza kukuhadithia ukweli mtupu, japo wewe humjui kabisa mtu huyo na hujawahi kumuona. Iwapo atamtongoza mwanamke fulani...basi siku moja atakuja ndotoni mwa mwanamke na kumuahidi kuwa atafunga nae ndoa (na hapo mwanamke hulainika) na kisha kuteka uzao wake.

Iwapo akijibadilisha kuwa mwanamke, basi huteka wanaume tena hutoa huduma ya ngono buree (free of charge). Na ukiamka asubuhi, hutamkuta. Ndugu umetekwa wewe, na kizazi chako kinachofuata...(manii yako yamechukuliwa). Huingia kwenye mitandao ya kijamii na huweka picha za utupu...sometimes ukitoa jicho kidogo utaona kama picha imecheza (inadaiwa hivi), mda mwingine huweka picha zenye ishara za kutisha....

9/ Hupenda kusifiwa sana kuwa wana nguvu na hodari michezoni, kazini na kadhalika. Hupenda watoto wadogo wakorofi. Lengo lao ni kuhakikisha dunia inaenda kwa namna wanavotaka wao, maana hupingana na Muumba. Hujawahi kusisimka ukipita sehemu fulani au kukaa mahali fulani ?? Kusisimka yaani bila baridi wala homa, nywele kusimama kiaina na vipele kutoka kwenye ngozi. Unakumbuka ule msemo wa shetani kapita...iwapo kukatokea ukimya fulani??? Basi, inawezekana msemo haukuja kibahati mbaya, mda mwingine kuna ukweli ndani yake (japo ni kidokezo tu).

10/ Mara nyingi huwa wengi sana kwenye miji ambayo ina majina yao (mfano: LA), na miji hiyo huwa na aina fulani ya mfanano! Pia hupenda sehemu zenye mkusanyiko wa watu wengi sana...au sehemu za watu wakorofi ili wawatumie au sehemu za watu watulivu ili wawaharibu.​

HAWA NI...FALLEN ANGELS A.K.A Majini. Tahadhari!! Ukweli ni kwamba hakuna wazuri, wote ni wabaya...! Shauri yenu, mnaotakaga watoto wa dawa za kiganga...! Unadhani hili neno"kizazi cha nyoka" lilitokea wapi?? La! hasha...!! sio unavyofikiria!!! Jamani, masheikh...mbona hamtuambii ukweli?? Maana hii elimu mnaijua vizuri kuliko yeyote yule...!!! Watoto wa hawa viumbe huitwa MAPEPO! Sio kweli, suicide zote ni sababu ya kusalitiwa au maisha magumu...bali ni stress za hawa viumbe hasa ukikataa kazi zao wakati hata Mungu huna!!

-- AYUBU 1:7 BWANA akamuuliza Shetani, “Umetoka wapi wewe?” Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema“ Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.”

-- 1 PETRO 5:8 Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.

Tuambie ulishawahi kukutana nao wapi viumbe hawa?? Ukiacha Kariakoo...??? Ulipambana nao vipi?? Hii thread haina matusi, na yeyote atakayejibu kwa matusi basi ujue ndio yule (aidha ndio yeye au anaye ndani yake).

<<<<Sasa sio kila utakayemuona utasema nae ni hawa viumbe (inawezekana tu anawatumikia kwa kujua au kutokujua)...tumia akili, umepewa utashi...lengo usikae gizani, uwe makini, hasa huko unapopenda kwenda stareheni!! Utakutana nao pale udhaifu wako ulipo...>>>!
 
Back
Top Bottom