Umewahi kukutana ana kwa ana na mnyama gani mkali?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,579
44,825
Mimi kuna siku niko na Pikipiki nimetoka site huko Nyengedi napanda Milima ya Rondo mida ya saa 2 usiku aisee Mara simba huyu hapa nilianguka na Pikipiki nikainyanyua sikugeuka nyuma nilipofika kijijini palepale nilizimia.

Kuna siku tena natoka Makangaka naelekea Kiranjeranje kupanda basi saa 12 Asubuhi niko na miguu aisee ghafla naona simba dume na jike huwezi amini simba Walikuwa hawana njaa walinisindikiza ila Mimi begi nilitupa na Viatu nilikimbia baadae akaja jamaa wa baiskeli aliokota viatu na begi kauliza nani mwenye begi nikamtajia vitu vilivyopo ndani kitambulisho na nguo akanipa begi.

Kuna siku tena niko speed natoka kinyope nakuja Rutamba pale katikati chui huyu hapa kainua miguu aisee nilinyosha wanguwangu akaruka pembeni.

Siku nyingine tuko na gari Tukaona tembo wanne ruangwa wanapita.

Kiboko ashanikosa kwenye mtumbwi mto Ruvuma daraja la Mkenda hakuwa na mtoto alikuwa anaibuka nasikia akiwa na mtoto ndio anakuwa mkali.

Nyoka ndio sana barabarani nishakutana nao zaidi ya Mara tatu ila wadogo wadogo sijawahi kukutana na joka kubwa na kuna siku tumekaa kwenye mti ghafla nyoka kadondoka.

Aisee tunaoishi huku Lindi tumepakana karibu sana na pori kubwa la selous yaani tunapocheza Cheza huku njiani tunakutana na viumbe machachari hapa ninahamu tu kuja kukutana na mamba live ndio sijawahi kumuona.
 
Nilikoswa koswa na nyoka nimeenda Kwa jirani kama saa moja hiv wakat naingia nasikia kitu kinafoka sikuwa na toch na umeme ulikuwa hakuna nikasimama bahat nzuri walikuwa na tochi wakamulika aisee bonge la joka wakamuua hatujakaa vizuri mwingine anakuja wakamuua nae nafikir ni wale wanatembeaga wawili wawil
 
Nilikoswa koswa na nyoka nimeenda Kwa jirani kama saa moja hiv wakat naingia nasikia kitu kinafoka sikuwa na toch na umeme ulikuwa hakuna nikasimama bahat nzuri walikuwa na tochi wakamulika aisee bonge la joka wakamuua hatujakaa vizuri mwingine anakuja wakamuua nae nafikir ni wale wanatembeaga wawili wawil
Nasikia nyoka wanatembea Bibi na Bwana 'Koira'
 
Kuna jamaa wa humu Jf alikutana na mjusi huko daslam, njebma ili changanyikiwa...🤣🤣
Baada ya kufanikiwa kumuua kwa kutimia fimbo ya ufagio, basi akaja hapa chap kujimwambafai jinsi alivyo pambana na mnyama mkali ndani kwake....😂😂
Mbaya zaidi akatupia na picha ya huyo mnyama (mjusi) kwenye ule uzi...😜😜
 
nimetoka kuua hili dude masaa machache yaliyopita
IMG-20240130-WA0007.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom