Aisee, mimi naogopa nyoka. Nyoka nawaogopa kiasi kwamba nikimuona tu, naanza kuhisi kuishiwa nguvu kwenye joint zate za miguu. ophidiophobia yangu ni ya kiwango cha juu sana. Hataa huu uzi tuu kuusoma kunanamna umenichukua.
Juzi kati tuu hapa nimesoma habari mtandaoni huko kenye mtoto aling'atwa na kitu usiku wamelala, alivozidiwa wakampeleka hospitali akaenda kufa. Ila wakaambiwa ameng'atwa na nyoka. Walivorudi nyumbani wakamkuta cobra kajizungusha kwenye blanketi walilokuwa wamejifunika. Hiyo habari inanipa wakati mgumu usiku nikilala. Hadi leo.
1. Miaka ya nyuma, kulikuwa na kichaka cha wastani kwenye shamba letu la mihogo. Palikuwa na uvumi kwamba kile kichaka ni makazi ya chatu. Na kuna watu waliwahi kikiri kabisa kumwona chatu akiingia na kutoka kwenye kile kichaka sio mara moja.
Mzee wangu alitafuta watu wa kukifyeka kile kichaka lakini hakupata. Watu waliogopa kujigeuza kitoweo cha chatu kwaajili ya vijisenti.
Mimi wakati huo ndo nmemaliza form four nasubiri matokeo nipo tu home najishughulisha na kazi za shamba. Jioni moja mzee akanichukua tukakifyeke kile kichaka. Niseme tuu kwamba kazi tuliifanya hadi ikaisha na hatukukuta chatu wa dalili ya chatu ila hakuna wakati nmewahi kuuona mgumu maishani mwangu kama wakati tunafyeka kile kichaka.
2. Mwaka 2015 nilikuwa najitolea kufundisha shule moja ya kata. Nilikuwa hosted pale pale shuleni. Kwenye ile nyumba tulikuwa tunaishi watatu, kila mmoja chumba chake tunashea sebule.
Ile shule ilikuwa na hostel. Baadhi ya wanafunzi hasa wa mbali walikuwa wanakaa hostel. Kwahyo walikuwa wajisomea madarasani usiku (Prepo)
Siku hiyo nimeenda kuzurura jioni. Mida ya saa mbili usiku nikarudi. Nikamkuta ticha mwenzangu kakaa sabuleni. Ile nataka kwenda chumbani kwangu akaniambia 'kuna nyoka huko'. Nilikuwa kama nimepigwa shoti ya umeme. Yaani nyoka, chumbani kwangu?!!. Nikamuuliza nimkubwa, akasema ni wa wastani tuu. Yule jamaa ni wale watu wasioogopa nyoka. Lakini kwangu, nyoka ni nyoka.
Nikamuuliza ameingiaje humu. Akaanza kunisimulia. Kwamba alikuwa amekaa pale pale alipokuwa, akasikia kama kitu kinakwaruza kwenye floor. Kutupa jicho akamuona nyoka mweusi anamfukuzia chura. Wametokea nje, wamepita sebuleni wakaenda chumba cha ticha mmoja hakuwepo.
Yeye akaanza kuwafuata kwa nyuma. Baade yule nyoka akahisi anafuatwa, akakurupuka arudi atoke nje. Akakutana uso kwa uso na ticha. Nyoka akabadili uelekeo ndo akaingia chumbani kwangu. Muda huo nasikiliza hiyo story nahisi kuishiwa nguvu kabisa.
Nikamuuliza sasa mbona hujamuua. Akanambia ameita madogo (wanafunzi) waje wamuue. Tunazungumzia nyoka lakini jamaa amekaa kwa kurelax utafikiri tunazungumzia panzi.
Dakika sifuri nikaona vijana wamefika. Kamawatano hivi na silaha za jadi. Wakazama rum wakaanza kumtafuta nyoka. Mi ndo kwanza nikaondoka kabisa. Asije akakurupushwa huko anikimbilie mimi.
Baada ya kama nusu saa nikarudi. Bado wanamsaka. Ile nauliza tu 'hawajampata?' Nikasikia chumbani huyo huyo huyoo.... paa...paa...kii..kii... tayari.
Kwa mashambulizi yale ilikuwa ni mda mfupi tu nyoka akakata kauli. Wakamto sasa. Aisee. Cobra jeusi tii...lirefu unene wa kufikia tairi ya baiskeli. Nilitetemeka balaa. Wakaliweka hapo nje tukaanza kulipiga picha.
Niliingia chumbani kwa hofu kubwa. Chumba kimeparaganyika. Walipoliulia limeacha damu nyingi sana. Damu inatoa haru. Inanuka yani. Nikaifuta nikapanga panga kwa tahadhari kubwa. Siku hiyo nililala kwa shida sana. Usingizi wa mang'amung'amu.
Kama mimi ningekuwa jasiri wa nyoka, ningekuwa nawafuga. Sumu ya nyoka inalipa sana.