Umeshawahi kukutana na balaa la nyoka?

Umeshawahi kukutana na balaa la nyoka?

Kobra ana ng'ata na kudunga sumu. Silaha yake ya kutemea / kurushia mate ni anapokuwa kwa mbali anaanza nayo hiyo kisha akikufikia anakutandika meno na kukudunga sumu kwa njia hiyo na ni kwa Kasi ya ajabu.

Mate yake yakikupata sehemu tofauti na machoni yanasababisha muwasho mkali na kwa baadhi ya watu eneo hilo huvimba hata wakati mwingine hutoa vidonda vinavyosababishwa na kujikuna sana.
Asante sana mkuu kwa ufafanuzi. Nawaogopa sana hawa viumbe hapa nasoma tuu ila mwili unasisimuka hata nikijigusa nastuka
 
Ni nyoka wawili tofauti mkuu, cobra ni swila na koboko ni black mamba au green mamba, ijapokuwa jamaa kashangaza kudhani swila hawapo huku
Screenshot_20230519-160751_Chrome.jpg
 
Narudia tena mkuu...
Kama hujamkanyaga au hujamzuia kuingia shimoni kwake cobra kamwe hawezi kukufuata akudunge.
Nimeishi maeneo yenye cobra na nimewahi kuua cobra wakubwa tu nikiwa peke yangu.
Ukimpiga nshingo aliyoinyanyua na kuitanua huwa anajizinga kwenye fimbo na habari yake inaishia hapo
Ila kweli nyoka wengi huwa hawana habri na sisi binadamu labda mpaka akihisi kuwa yuko kwenye hatar au uki mchokoza.

Nimeishi sehemu zenye nyoka tena wakati wa baridi una wakuta ndani na wala hawalet madhara kwa watu
 
Ila kweli nyoka wengi huwa hawana habri na sisi binadamu labda mpaka akihisi kuwa yuko kwenye hatar au uki mchokoza.

Nimeishi sehemu zenye nyoka tena wakati wa baridi una wakuta ndani na wala hawalet madhara kwa watu
Hasa huyo cobra, huko vijijini usiku anapanda hadi vitandani utamkuta amechangia shuka na mwenye nyumba bila madhara.

Ukimgusa na akahisi hatari ndipo atakugonga, usipomgusa anakukimbia kujificha
 
Mapori yenye kware na kanga yanakuwa na nyoka wengi kwakuwa ndege hawa hutaga mayai chini, na nyoka, hasa cobra, wanapenda mayai sana.
Bana lile Gereza lilikuwa na uzio wa miti ya asili na ya kupandwa mingi sanaaa iliyozungushiwa seny'enge hakukuwa na ukuta na nyumba za askari baadhi zilikuwa na nyasi juu na kulikuwa hakuna umeme!

Kwa masika tatu nilizoishi pale hakuna nyoka sijawahi muona, huyu Swila na koboko ni popular sana lile eneo kuna magereza mawili moja ni kambi inaitwa Uganda mzee nashindwa hata kusimulia vizuri

Niliwahi kuamshwa ndani kumejaa siafu sasa katika purukushani nao kumbe kuna ndumila kuwili wawili kwenye madumu ya maji tukawabomoa kumbe mzee wa kazi koboko yuko around hehehehe
 
Chatu na dereva wa gari za Dangote.

Miaka kadhaa iliyopita Kuna Docta mmoja alikuwa anatoka Dar anaelekea Masasi mkoani Mtwara kwa mambo yake binafsi. Alipofika ndani ya viunga vya wilaya ya kilwa mkoani Lindi kwa mbali mbele yake akaoana na gari (roli) ya Dangote ambayo ilikuwa inaelekea Mtwara. Baada ya dakika chache jamaa wa Dangote akapunguza mwendo akapaki kando ya barabara Kisha akashuka akasogea kwa ndani kwenye majani. Ilikuwa mida ya jioni Kama saa kumi na moja. Doctor akalipta lile roli na kuendelea na safari yake.

Kesho yake Doctor alipomaliza mishe zake mjini Masasi akawasha gari na kurudi Dar. Cha ajabu alipofika eneo lile la Jana mahali gari la Dangote limepaki alilikuta lipo vile vile. Na gari halikuwekwa triange kuashiria kwamba limehaeibika. Ilikiwa Kama limepaki kwa muda Kisha safari itaendelea.

Jamaa akapunguza mwendo Kisha akawa anaendesha mdogo mdogo mpaka usawa wa lile roli. Akapaki pembeni Kisha akashuka na kuvuka barabara kwenda upande wa pili kuangalia pengine dereva ana shida au amepata ugonjwa wa ghafla alafu watu/madereva wapita njia wasijue maana gari halikuonekana Kama Lina ishara ya kuharibika na halikuwa na mzigo maana lilikuwa linarudi Mtwara.

Alipofika akapiga hodi kwa mlango wa dereva hakukuwa na response yoyote. Akajaribu kufungua mlango ukafunguka bila shida. Akaangalia ndani hakuona mtu. Wasiwasi ukamwingia akahisi Kuna uwezekano wa tatizo,ile haikuwa hali ya kawaida.

Akasogea barabarani kuangalia magari yanayokuja. Kwa bahati Kuna gari ndogo ikawa inapita akaipungia mkono ikasimama. Wakapita madereva Kama watatu nao wakasimama. Jamaa akawasimulia kilichotokea kuanzia jana. Wakaamua kuingia kwa ndani,ndani ya kamsitu kuangalia Kama wataona chochote.

Kilichotokea....

Kumbe yule dereva ile Jana aliposhuka kwenye gari alienda kujisaidia (tafsida). Huko porini ndiyo akakutana na balaa la chatu. Inavyoonyesha chatu aliweka mtego jamaa akauingia,na kwa kukosa msaada akazidiwa nguvu akauawa Kisha akamezwa.

Pale porini walimkuta chatu amelala hoi kwa kushiba na tumbo lake limejichora alama ya mtu akiwa amelala kwa kunyooka.

Taarifa ikawafikia wenye mamlaka,chatu akauawa na marehemu akatolewa nje ya mwili wa chatu. Picha za yule jamaa zilikuwa zinatisha sana maana alimezwa mzima mzima,yeye,viatu hadi nguo. Alikuwa Kama amemwagiwa mayai au mlenda.

Kama humu ndani Kuna madereva au wahusika wa Dangote wanaweza kukumbuka hiki kisa Cha dereva wao aliyemezwa na chatu Miaka kadhaa iliyopita.

Kuna kisa kingine Cha kishujaa Kati ya chatu na Mamba...

Narudi
Hii nami niliisikia
 
Yeah ni kisanga sana, mpaka nimecheka nikikumbuka mambo yake enzi hizo kwenye mashamba ya Gereza Ushora daaah!

Unawafahamu Kanga na kware?
Kanga nimewahi kuwafuga, enzi hizo unachukua mayai kanga unamuwekea kuku.
 
Hasa huyo cobra, huko vijijini usiku anapanda hadi vitandani utamkuta amechangia shuka na mwenye nyumba bila madhara.

Ukimgusa na akahisi hatari ndipo atakugonga, usipomgusa anakukimbia kujificha
NI JUZI TU ITV KWENYE TAARIFA YA HABARI NA HATA HUKU MITANDAONI WALITUONESHA HUKO ARUSHA DOGO MMOJA ALIFARIKI BAADA YA NYOKA AINA YA COBRA KUINGIA NDANI USIKU NA KUPANDA KITANDA WALICHOLALA WATOTO KISHA KUMNG,ATA MTOTO MMOJA. MTOTO ALISHTUKA NA KUANZA KUPIGA KELELE NA KUSEMA KUNA KITU KIMEMNG,ATA NDIO WAZAZI WAKAAMKA NA KUMPELEKA HOSPITAL ILA KILA WAKIONGEA NAE MTOTO ANAZIDI KULEGEA NA ULIMI UNAKUA MZITO.
KUFIKA HOSPITAL MTOTO AKAFARIKI NA MADOKTA WAKASEMA ALING,ATWA NA NYOKA, HIVYO WAZAZI WAKARUDI KUKAGUA WAJUE NI NYOKA YUPI. KATIKA KUFUNUA KITANDA NDIO WAKAKUTA NYOKA AINA YA COBRA AMEJIVIRINGISHA KWENYE BLANKET WAKAMUUA HAPO HAPO.
 
NI JUZI TU ITV KWENYE TAARIFA YA HABARI NA HATA HUKU MITANDAONI WALITUONESHA HUKO ARUSHA DOGO MMOJA ALIFARIKI BAADA YA NYOKA AINA YA COBRA KUINGIA NDANI USIKU NA KUPANDA KITANDA WALICHOLALA WATOTO KISHA KUMNG,ATA MTOTO MMOJA. MTOTO ALISHTUKA NA KUANZA KUPIGA KELELE NA KUSEMA KUNA KITU KIMEMNG,ATA NDIO WAZAZI WAKAAMKA NA KUMPELEKA HOSPITAL ILA KILA WAKIONGEA NAE MTOTO ANAZIDI KULEGEA NA ULIMI UNAKUA MZITO.
KUFIKA HOSPITAL MTOTO AKAFARIKI NA MADOKTA WAKASEMA ALING,ATWA NA NYOKA, HIVYO WAZAZI WAKARUDI KUKAGUA WAJUE NI NYOKA YUPI. KATIKA KUFUNUA KITANDA NDIO WAKAKUTA NYOKA AINA YA COBRA AMEJIVIRINGISHA KWENYE BLANKET WAKAMUUA HAPO HAPO.
Huenda alimlalia au kumgusa mkia.
Nyoka yuko sensitive sana mkiani ukimgusa kwisha habari yako.
Huyu inaonyesha alizongwa na blanketi akashindwa kuchomoka
 
Tanzania safari channel wana kipindi Chao walifanya mahojiano na wataalamu kutoka chuo cha wanyama pori cha mweka, wakaelezea mambo mengi tu kuhusu nyoka. mojawapo walisema 85% ya nyoka duniani hawana sumu, ila tunawaua tu kwa hofu na kutokujua kutofautisha wenye sumu wana mwonekano gani na wasio na sumu wako vipi.
 
Back
Top Bottom