Umeme wakatisha maisha ya vichanga Hospitalini Muhimbili


Hii Hospital si iko chini ya yule waziri anayeunda tume kuchunguza tume ? na hata matokeo ya tume ya kuchunga tume huwa hayatoi hadharani? sintoshangaa mh huyu akiunda tume kuchunguza tume na tume ambayo itakuwa inachunguza tume zilizopita..kazi kweli kweli, pole wa wafiwa wa watoto wao jamani....inauma lakini ni Tanzania yetu
 



Una hakika gani kuwa jenereta iliyokuwepo ni automatic? Kwa kuongezea, mashine sensitive za karne hii, jenereta haitoshi. Kutosikia taarifa kama hizi si ushahidi kuwa havitokei. Watanzania hawana kawaida ya kulalamika. Ndiyo tulivyo. Ukisoma majibu ya madaktari ni ya kujihami. Sitoshangaa kesho kusikia kuwa halikuwa tatizo la kukatika umeme.

Nakubaliana nawe kuwa kuna dalili za uzembe katika suala zima. Kwa kawaida mashine zakisasa zinahitaji UPS ambayo inahakikisha kuwa hakuna downtime hata ya sekunde moja. Na hizi si vile vinavyowekwa chini ya meza kwenye maofisi yetu. Lakini pengine hizo mashine za kupumilia hazihitaji hizo UPS. Hilo nakiri sijui.

Kinachonisikitisha zaidi ni kuwa haya yanatokea Muhimbili. Je huko ambako waandishi wa habari hawafiki? Wangapi wanapoteza maisha kutokana na uzembe?

Mimi matatizo yangu ni hao madaktari na wataalamu wengine. Sijawahi kuwasikia wakifanya mgomo kulalamikia mazingira ya kufanyia kazi.Mazingira haya yanajumuisha pia vitendea kazi vya kuaminika. Wao ni mishahara tu. Ninavyoona mimi, mazingira ni muhimu zaidi. Sidhani kama nimemtaja JK kwenye hili!
 
"Tuunde tume, kuna tume imeundwa, tusubiri matokeo ya tume, tume yatembelea vijjij kukusanya maoni, tume yafanya majadiliano, tume tume tume'!

Tume ya Muhimbili kuchunguza upasuaji, tume ya Raisi ya Madini, tume ya uchunguzi BOT, tume ya Dawasco, tume uratibu wa tume!

This is what our government has become. everything has a tume that is given a time frame that allows last minute uhujumu!

Okay, kwanza ni pole kwa wafiwa.

Pili je ni nini kilichotokea?

  • Je ni kwa nini umeme wa Tanesco ulikatika? ni sababu za kiufundi, kiutendaji, uzembe, ajali au...?
  • Je kwa nini ilichukua dakika 10 kwa Muhimbili kuanza kutumia umeme wa jenereta? je fundi alikuwa amelala, walikuwa hawana mawe kwenye kurunzi kuona swichi ilipo? je mafuta yalikuwa yamepungua kina cha kuwasha jenereta? je walisubiri mhandisi mkuu aongee na mkurugenzi mkuu wapate kibali cha kuwasha jenereta na kutumia mafuta ya dharura?
  • Yameshatokea, je ni mipango gani itfanyika kuhakikisha kuwa patakapotokea tatizo kama hili wakati mwingine, ile mitambo ya kisasa inayojiwasha katika sekunde moja itakuwa ipo na inafanya kazi?
  • Je hospitali na sehemu nyingine nyeti zina mipango gani madhubuti ya kuwa na mitambo ya kisasa kuhakikisha kuwa panapotokea matatizo kama haya, basi kuna back na recovery inafanyika katika sekunde na si dakika?
  • Je Tanesco hawana powersource maalumu ambazo zitalisha sehemu nyeti daima kwa kualternate hata kama powersource moja imepata shida?
Tunadai uwajibikaji, je ni nani awajibike? Mhandisi mkuu, fundi wa zamu, mganga mkuu, wakurugenzi wakuu Muhimbili na Tanesco?, Waziri wa Afya, waziri wa Nishati, waziri mkuu, Raisi?

Kwa kuwa awamu ya nne imejijengea sifa ya kufanya mambo at ease, na kujivuta, sishangai ghadhabu za wana JF kudai ni uzembe wa Serikali hata kudai Rais awajibike. Iwapo Raisi angekuwa anafanya maamuzi mengine swiftly bila kuonekana na kigugumizi au kutafuta "win-win situation" inayoishia kumuonyesha kuwa hana uwezo wa kufanya maamuzi ya kuwajibisha watu, tusingekuwa na malezi komau ya watu na watendaji wasiojituma na kuwajibika bila kusukumwa!
 

Fundi,

Watalalamikije kuhusu mazingira na vitendea kazi wakati kuna uwezekano wanavihujumu? Alipokuwepo Daudi Trigonometry, walilalamika sana kuwa jamaa ni mkoloni, mkali ananyanyasa.

Lakini Daudi alikuwa akifanya kazi kuhakikisha kuwa hospitali ina zana za kutosha na nidhamu ya kazi inarudi. Walichokimbilia kulalamika si kuhusu utendaji wa Daudi bali ni marupurupu anayolipwa.

Tumemfukuza Trigonometry, tumewaleta "wenzetu". Tumeanza majungu tena, ooh sijui ni Mchaga, hana Digrii za kutosha za upasuaji, kila mtu kafungulia bomba la kula na kubangaiza maana mkoloni kaondoka na malalamishi mengi.

Sijui tena ni ni nini ambacho tunahitaji kama Taifa tunawajibika kukifanya kuhakikisha kuwa tunaachana na uzubafu ambao unatuondolea ufanisi na upevu wa kufanya mambo kwa kujituma na kuwajibika!

Tutadai mishahara zaidi kama wenzetu wa Botswana, huku kusoma chati kuuliza jina la mgonjwa vinatushinda!
 
......hayo ndio matatizo ya serikali kuuuuuuuuuubwa kama dunia!!
Hizo ndio zinaitwa bureaucratic nightmare, hii siyo issue ya JK ila hapo muhimbili inabidi mtu awajibike. hii kitu imekaa kama mchezo wa kuigiza.
 
Apa kwanza waziri wa afya awajibike pamoja na na uyo aliyepewa rungu la kusimamia iyo hospitali.

Hospitali kubwa kama muhimbili mnakosa standby Generator wakati nowdays ni kitu cha kawaida.

Utasikia soon tume itaundwa kuchunguza ilo na uku generator likiwa bado ni tatizo.

Kwa mtu makini TANESCO sio wa kuwategemea kabisa mimi mwenyewe kwangu tuu siwategemei sembuse hosp kubwa kama muhimbili.

Mbona kila kona kona watz tunaonekana hatuko seriuous wapi sasa tutakuwa serious jamani?

Someone has to pay the cost of of our beloved children who have passed away.

My their souls rest in peace.Amen
 
Kamwambie aliyekutuma, wanaJF wanauliza hivi huko jikoni ni wapi ili tuje tumsaidie kutafuta dawa?


Hivi miaka yote JK aliyo kaa serikalini hakuwahi kujua nini hasa matatizo ya Tanzania ? Uliutaka wa kazi gani kama hakujua lolote la Nchi ? Hebu acha kutuptezea muda kusema JK kaurithi wakati JK ni mmoja wa hawa walio lete matatizo haya .
 
dar Es salaam hapa vipi hujasema jk asifiwe ? Mbona unaacha hoja na kumshambulia jamaa ? Nilitegemea utaendeleza kumwaga sifa kwa jamaa kwamba anachapa kazi .

kasome thread kuanzia mwanzo ujue nimesema nini, usikurupuke.
 



Kwa hili Mkuu Rufiji nakuunga mkono mia kwa mia.


Ingekuwa ni hivyo usemavyo wewe basi kila siku tungesikia tatizo hilo.


Ungekuwa unaweza ungewahi wewe jikoni.

dar Es salaam hapa vipi hujasema jk asifiwe ? Mbona unaacha hoja na kumshambulia jamaa ? Nilitegemea utaendeleza kumwaga sifa kwa jamaa kwamba anachapa kazi .

Kwa kukurahisishia nimekuwekea posts zangu zote kuhusu thread hii hapa ili usisumbuke kuzitafuta. Halafu sasa tuanze na maswali yako, kama hayana majibu kwenye hizo post.
 

Labda lilichelewa kuwaka kwa sababu lilikuwa linasubiri kuundiwa Kamati Teule!
 
kwi kwi kwi kwi kwi...

kamati teule na baada ya hapo iundwe tume ya kuchunguza kamati teule!

kama ile kamati teule tuliyoiunda kutaka kamati ya ushindi KiTETO ichunguzwe ilishindwaje? au sio? Ha ha ha ha haaaaaaaaaaa ha!
 
kama ile kamati teule tuliyoiunda kutaka kamati ya ushindi KiTETO ichunguzwe ilishindwaje? au sio? Ha ha ha ha haaaaaaaaaaa ha!

Cha kuchekesha hapa ni kipi sasa! Watu walisha-move on kutoka Kiteto na sasa kuna miziki mipya inawekwa hapa JF na wewe unaleta kifafa hapa!

tik tak tik tak!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…