Umeme wakatisha maisha ya vichanga Hospitalini Muhimbili

Mwanamalundi

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2007
Messages
3,130
Points
1,500

Mwanamalundi

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2007
3,130 1,500
Shhhhh usiongee kwa sauti kabla Kitila Mkumbo hakusikia na akazuia pepa yangu ya disertation....lol.

Ndugu yangu, katika hili mimi niko radhi kuzuiwa pepa yangu kuliko watu kutumia mabilioni kulipa makampuni ya umeme yasiyo na huduma za hakika na katika hili JK na serikali yake wako full responsible.
Mwafrika wewe endelea kunivunja mbavu tu hapa. Lakini tusipokuwa makini tunapoelekea ni kubaya zaidi. Maana hata wahasibu katika wizara ya afya sasa hivi wanapindisha mahesabu yao usiku kucha ili kesho na kesho kutwa wambebeshe lawama zote kikwete. Na wana haki ya kufanya hivyo. Lakini wahasibu hao hao wanaendelea kuporomosha magorofa msasani penisula. Kesho, umeme ukikatika muhimbili, jibu rahisi na la haraka watakalokupa ni RICHMOND.
 
BabaH

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2008
Messages
704
Points
195

BabaH

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2008
704 195

Hapo ndo ninapokwambia kuwa kuna tatizo serikalini ndugu yangu
iweje wahasibu wanapindisha mahesabu, kwani hayo mahesabu hayakaguliwi mpaka ngazi za juu, tatizo lipo kwa sababu wanajua wanalindana kaka.
Kikwete ana watu wake anaowalinda na hao wanaolindwa wana wanowalinda pia, kwahiyo hiyo cheni imeanzia juu
Kama kungekuwa hakuna kuonea haya, wasingekuwa na uwezo wa kupindisha mambo kiorela kaka, kwani wanajua watawajibishwa.
Lakini kwa serikali hii viongozi wengi wako corrupted kaka, ndo maana mambo yanakuwa hovyo
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2007
Messages
5,194
Points
0

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2007
5,194 0
Mwafrika wewe endelea kunivunja mbavu tu hapa. Lakini tusipokuwa makini tunapoelekea ni kubaya zaidi. Maana hata wahasibu katika wizara ya afya sasa hivi wanapindisha mahesabu yao usiku kucha ili kesho na kesho kutwa wambebeshe lawama zote kikwete. Na wana haki ya kufanya hivyo. Lakini wahasibu hao hao wanaendelea kuporomosha magorofa msasani penisula. Kesho, umeme ukikatika muhimbili, jibu rahisi na la haraka watakalokupa ni RICHMOND.
Nakuhakikishia kuwa kama hao wahasibu unaosema wangeona Kikwete akiwachukulia hatua mafisadi katika serikali basi wangejua kuwa hakuna mchezo.

Kama Kikwete mwenyewe anaacha mapapa wa wizi wakipeta kwa wizi katika serikali (anza na Chenge) unategemea nani atakuwa serious katika chochote.

Nasisitiza kuwa kama Kikwete haguswi na watoto wachanga wanaokufa hostpitali kwa kutegemea kuwa kuna watendaji huko basi this is beyond hali ya kawaida ya ubinadamu.

Katika hili I hold Kikwete na serikali yake ya ccm responsible kwanza kabla ya kutafuta mchawi au wale wanaoshikilia pepa za wanafunzi kule mlimani.
 
zomba

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2007
Messages
17,071
Points
0

zomba

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2007
17,071 0
Hongera sana ndugu JK . Nategemea ndugu Dar Es Salaam utafika hapa kumpa Hongera ndugu Rais kwa mambo yake makubwa haya .Mungu awarehemu hawa watoto .
Ahsante kwa kuniikumbuka, nimefika.

Jee, kama genereta lipo tatizo ni JK? ingekuwa genereta hakuna hapo ndio tungemshutumu Mkuu.

Haya ni makosa ya watendaji na inabidi hatuwa za haraka zifanyike na wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu kwa makusudi kabisa.

Uozo wa utendaji Muhimbili unaonyesha kukomaa, (nikikumbuka na kisa cha kizembe kabisa cha kuchanganya wagonjwa).
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2007
Messages
5,194
Points
0

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2007
5,194 0
Ahsante kwa kuniikumbuka, nimefika.

Jee, kama genereta lipo tatizo ni JK? ingekuwa genereta hakuna hapo ndio tungemshutumu Mkuu.

Haya ni makosa ya watendaji na inabidi hatuwa za haraka zifanyike na wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu kwa makusudi kabisa.

Uozo wa utendaji Muhimbili unaonyesha kukomaa, (nikikumbuka na kisa cha kizembe kabisa cha kuchanganya wagonjwa).
Maisha ya watanzania yanapokuwa hatarini na kupotea kama hili la muhimbili basi raisi wa nchi anakuwa responsible. yaani bucks zote zinaishia kwake!
 
MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2007
Messages
3,922
Points
1,250

MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Joined Jun 24, 2007
3,922 1,250
Kwani wafanyakazi wa serikali mnajua mishahara yao? Ni laki 3, 4 au 5!

Angalia majumba walioporomosha ya 100m Kimara, Mbezi, Segerea n.k je hizi pesa wanapata wapi???

Kuna wizi na uporaji mkubwa wa pesa za serikali throgh bogus seminars za Morogoro, supersion za kiajabu ajabu mikoani na hii ndi mwanya ya pessa ya serikali kuliwa na kujenga hizo nyumba!

Wizara ya Afya alikuja tu KM mama Gonjwe akaziba hii kula kwa mda mfupi angalia walimpiga jungu kwa JK ili amwondoe na akaondolewa sasa RAS Kilimanjaro!

Kwa kifupi wafanyakazi ktk Wizara Tz hawaishi kwa mishahara.. ila hizi allowance na wizi wa mchana.. yet if you evaluate perfomance kila Wizara in say 5 years yuo find so little echievemets Mikoani! Zaidi tu outcome ni mijumba ya mamilioni ya pesa zilizoibiwa ndo utaziona!

Hii hali ni sawa ktk Tawala za Mikoa na Halimashauri za Wilaya!

Wizi na uporaji wa pesa za kodi ndo kinachoonekana zaidi sikalini!

JK analijua hili na hii ndi imekuwa ni utamaduni wa kulindana, Mawazarani, Sekratariate za Mikoa na Halmashauri za Wilaya!

JF Mnasemaje?
 
Augustoons

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2007
Messages
411
Points
195

Augustoons

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2007
411 195
Ahsante kwa kuniikumbuka, nimefika.

Jee, kama genereta lipo tatizo ni JK? ingekuwa genereta hakuna hapo ndio tungemshutumu Mkuu.

Haya ni makosa ya watendaji na inabidi hatuwa za haraka zifanyike na wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu kwa makusudi kabisa.

Uozo wa utendaji Muhimbili unaonyesha kukomaa, (nikikumbuka na kisa cha kizembe kabisa cha kuchanganya wagonjwa).
Dar-es-salaam,
Kwa mara ya kwanza umeongea pointi,nadhani sasa umeanza kuelewa mfumo wa utawala ukoje toka juu hadi chini.Na kwa hilo tuko pamoja.Manaake wale wakurugenzi wa muhimbili,some ni presidential appointees,akiwamo waziri husika,hivyo kama waziri akishindwa kusimamia watumishi wa wizara au mtumishi wa wizara akifanya blanda ndio maana mtu wa kwanza kulaumiwa ni waziri hata kama hakuwepo wakati blanda inatokea,na wa pili ni Rais kama atashindwa kumwajibisha waziri wake.Vivyo hivyo katibu mkuu ndiye mkuu wa utumishi wa wizara,hao wakurugenzi,wahasibu n.k.wapo chini yake,na yeye yupo chini ya waziri na waziri yupo chini ya Rais, kwa hiyo chain of command ndio maana anayeonekana juu kabisa ya pyramid ndio tunaanza naye.wengine wanafuata baadaye.
Wenzetu kwenye sheria za makampuni wanaita doctrine of corporate veil. Kwamba kampuni ni lile shela,chochote kitakachofanyika tunaliangalia kwanza shela kama shela(yaani mkurugenzi mkuu na bodi) halafu baadaye ndio tunaenda kwenye kulifunua shela(lifting corporate veil) ambapo tunachambua sasa samaki yupi kaoza yupi bado mzima,kwa mantiki hiyo nani hasa anahusika.

Inapotokea hali kama hiyo usalama wa waziri ni kumuwajibisha katibu mkuu ili naye awawajibishe waliochini yake hadi tunamfikia mtu wa mwisho mhusika mkuu akishindwa kufanya hivyo na kusababisha bunge kuingilia kati au wananchi,sisi hatuwajui hao wafanyakazi yeye ndio anawajua vizuri,sisi na wabunge tunaanza na yeye waziri kwanza,akileta nyodo tunapanda kwa Rais.Na huu hasa ndio msingi wa kusema serikali haijafanya hiki au kile.Na tunaposema serikali kwa ufupi ni baraza la mawaziri.
Japo kinadhari na kisiasa watu watakuambia serikali ni mimi na wewe.Ndio maana wananchi wakiandamana magazeti hayaripoti kwamba serikali ya tanzania imeandamana,kama kweli wewe na mimi ndio serikali,ila waziri akisema jambo ama rais utasikia serikali imesema.Hivyo Dar-es-salaam kuanza na Rais ni sawa kabisa
 
Rufiji

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2006
Messages
1,786
Points
1,500

Rufiji

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2006
1,786 1,500
Wanabodi ,

Ni jambo la kusikitisha kuona watoto wadogo wakipoteza maisha kutokana na uzembe wa watu wachache ! Ni lazima wawajibishwe wale wote waliohusika na kitendo hiki cha kizandiki. Pili napendekeza serikali isitishe mara moja mchezo wa kutibu viongozi nje badala yake watibiwe hapo nyumbani ili Hospitali hiyo ya Muhimbili iweze kuboreshwa.
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
Wakuu hiii ni JF, hatuandikii mate na wino upo wanaohusika watajwe hapa kuanzia wa chini mpaka wa juu, tutawasukumia kuanzia wabunge mpaka mwene kaya, waamue kusuka au kunyoa,

hao wazembe huko Muhimbili wanaohusika na hivi vifo vya watoto watajwe hapa, tukate mzizi wa fitina! Until then ninampa muungwana the benefit of the doubt kwenye hili!
 
green29

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2007
Messages
312
Points
225

green29

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2007
312 225
Muhimbili kulikuwa na automatic standby generator labda kama wameiua.
Hivi Mkurugenzi mkuu wa hospitali ya Muhimbili ni nani sasa hivi...bado ni prof. Lema au!? Kuna yule jamaa Tregonin ni mbabe mmoja alikuwa raia wa Ireland alikuwa mkurugenzi pale sijui alienda wapi. Yule jamaa ni mzungu lakini inasemekana alikuwa anawapandishia huko wizarani wakichelewesha vitu vinavyohatarisha maisha ya watanzania pale hospitali. Nilipataga tetesi wakurugenzi waliokuwa chini yake walikuwa wanamchukia pale hospitali sababu ya kuwabania mafisadi wasile pesa za wagonjwa. Sina hakika kama aliondoka kwa heri.
 
zomba

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2007
Messages
17,071
Points
0

zomba

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2007
17,071 0
Dar-es-salaam,
Kwa mara ya kwanza umeongea pointi,nadhani sasa umeanza kuelewa mfumo wa utawala ukoje toka juu hadi chini.Na kwa hilo tuko pamoja.Manaake wale wakurugenzi wa muhimbili,some ni presidential appointees,akiwamo waziri husika,hivyo kama waziri akishindwa kusimamia watumishi wa wizara au mtumishi wa wizara akifanya blanda ndio maana mtu wa kwanza kulaumiwa ni waziri hata kama hakuwepo wakati blanda inatokea,na wa pili ni Rais kama atashindwa kumwajibisha waziri wake.Vivyo hivyo katibu mkuu ndiye mkuu wa utumishi wa wizara,hao wakurugenzi,wahasibu n.k.wapo chini yake,na yeye yupo chini ya waziri na waziri yupo chini ya Rais, kwa hiyo chain of command ndio maana anayeonekana juu kabisa ya pyramid ndio tunaanza naye.wengine wanafuata baadaye.
Wenzetu kwenye sheria za makampuni wanaita doctrine of corporate veil. Kwamba kampuni ni lile shela,chochote kitakachofanyika tunaliangalia kwanza shela kama shela(yaani mkurugenzi mkuu na bodi) halafu baadaye ndio tunaenda kwenye kulifunua shela(lifting corporate veil) ambapo tunachambua sasa samaki yupi kaoza yupi bado mzima,kwa mantiki hiyo nani hasa anahusika.

Inapotokea hali kama hiyo usalama wa waziri ni kumuwajibisha katibu mkuu ili naye awawajibishe waliochini yake hadi tunamfikia mtu wa mwisho mhusika mkuu akishindwa kufanya hivyo na kusababisha bunge kuingilia kati au wananchi,sisi hatuwajui hao wafanyakazi yeye ndio anawajua vizuri,sisi na wabunge tunaanza na yeye waziri kwanza,akileta nyodo tunapanda kwa Rais.Na huu hasa ndio msingi wa kusema serikali haijafanya hiki au kile.Na tunaposema serikali kwa ufupi ni baraza la mawaziri.
Japo kinadhari na kisiasa watu watakuambia serikali ni mimi na wewe.Ndio maana wananchi wakiandamana magazeti hayaripoti kwamba serikali ya tanzania imeandamana,kama kweli wewe na mimi ndio serikali,ila waziri akisema jambo ama rais utasikia serikali imesema.Hivyo Dar-es-salaam kuanza na Rais ni sawa kabisa
Laiti ungekuwa unazitazama vizuri posts zangu kwa muono mpana ungenielewa vizuri kabisa.

Kumbuka uozo wa hii nchi kaurithi JK, na hivi sasa yupo jikoni kuutafutia dawa. Kwanza tumeona ameanza na rushwa, ubadhirifu na ufisadi na hivyo ndio vyanzo vya matatizo yote haya. Halafu yanafatia haya ya uzembe, kumbuka aliwekwa Muingereza pale Muhimbili kuiendesha, akapikiwa majungu mpaka akatimka, kwa nini? kwa kuwa alikuwa anawajibika ipasavyo na kuna wengi pale wakaona wanazibiwa njia zao za ubadhirifu na ufisadi na matokeo ndio hayo.

Uzembe huu (wa Muhimbili in particular) ni confined within Muhimbili na haujaanza leo na inabidi ushughulikiwe kikamilifu.

Hau-expect kuwa Rais wa nchi akumbushe mpaka mafuta ya genereta!

Hii itakuwa si kumtendea Rais haki, kabisa.
 
BabaH

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2008
Messages
704
Points
195

BabaH

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2008
704 195
Wanabodi ,

Ni jambo la kusikitisha kuona watoto wadogo wakipoteza maisha kutokana na uzembe wa watu wachache ! Ni lazima wawajibishwe wale wote waliohusika na kitendo hiki cha kizandiki. Pili napendekeza serikali isitishe mara moja mchezo wa kutibu viongozi nje badala yake watibiwe hapo nyumbani ili Hospitali hiyo ya Muhimbili iweze kuboreshwa.

Kaka ninakubliana na wewe kwenye hili kabisa
Kitendo cha viongozi wa nchi kwenda kutibiwa nchi za nje ndo chanzo kabisa cha kushindwa kuboresha Hospitali zetu, kwa sababu wao wanajijua wakipata matatizo wanapelekwa nchi za nje, na cha ajabu wakija huku nje wanajionea mahospitali yalivyo jamani. sasa inakuwaje National Hospital kama muhimbili inakosa vifaa vya muhimu
Mwalimu alianzisha Hospitali ya Lugalo kwa ajili haswa ya kutibu viongozi wa serikali, alikuwa na nia nzuri sana, lakini angalia sasa hivi watu wameiharibu, hakuna madawa sio standard, na wao wanaenda kutibiwa nchi za nje.
Kibaya zaidi ndugu wapendwa ni kwamba, hao viongozi wanapokwenda nje kutibiwa,
  1. wanatibiwa na pesa za walipa kodi amabao wao waliolipa hizo kodi wanakufa hapo muhimbili na hospitali zingine.
  2. wanazidisha matumizi maradufu ya zile gharama zilizotumika huko kwenye hospitali, na hivyo kiongozi kuumwa na kupoelekwa njee siku hizi ni dili

Ebu tuelezane hapa, je kikwete hapa na napo hausiki direct jamani, kwani si anaona kila siku haya mambo na yeye ndo mkuu wa kaya? Nisaidie hapa.
 
BabaH

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2008
Messages
704
Points
195

BabaH

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2008
704 195
Laiti ungekuwa unazitazama vizuri posts zangu kwa muono mpana ungenielewa vizuri kabisa.

Kumbuka uozo wa hii nchi kaurithi JK na hivi sasa yupo jikoni kuutafutia dawa. Kwanza tumeona ameanza na rushwa, ubadhirifu na ufisadi na hivyo ndio vyanzo vya matatizo yoye haya. halafu yanafatia haya ya uzembe, kumbuka aliwekwa Muingereza pale Muhimbili kuiendesha, akapikiwa majungu mpaka akatimka, kwa nini? kwa kuwa alikuwa anawajibika ipasavyo na kuna wengi pale wakaona wanazibiwa njia zao za ubadhirifu na ufisadi na matokeo ndio hayo.

Uzembe huu (wa Muhimbili in particular) ni confined within Muhimbili na hayajaanza leo na inabidi yashughulikiwe kikamilifu.

Hau-expect kuwa Rais wa nchi akumbushe mpaka mafuta ya genereta!

Hii itakuwa si kumtendea Rais haki, kabisa.

Naona ndugu hapo hujaelewa kinachozungumziwa kabisa
Kwanza nikueleze, kikwete hajaonyesha dalili zozote za kiukweli zaidi ya unafiki mtupu katika kulitafutia swala la rushwa suluhu, kwa sababu nyingi tu, unakumbuka watu walipowataja mafisadi wakuu alitoa kauli gani ya kuwajibu wapinzani? lakini umeyaona yaliyoibuliwa na Slaah sasa,
Unakumbuka wakati anaongea na wazee wa mkoo wa Dar alieleza nini kuhusu EL na baadae alieleza kitu gani kuhusu Kamati teule ya BUNGE, kama unayo majibu hapo utakubaliana nami kuwa JK anatupuliza uku akitungata.
Na kinachozungumziwa hapa, sio kuwa JK anatakiwa kukumbusha mppaka mafuta ya Generate, swana ni kwamba kutokana na kasumba mbovu ya kuindesha serikali, ambapo anashindwa kuwawajibisha mawaziri wake, haya ndo yanatokea, na ndo maana watu wanamuona JK kama responsible person, kwa sababu hafanyti kazi zake huko juu, kama juu hawawajibiki inategemea nini huku chini kaka??
Tafakari haya mambo kaka
 
Ogah

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
6,233
Points
1,225

Ogah

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2006
6,233 1,225
..............Jee, kama genereta lipo tatizo ni JK? ingekuwa genereta hakuna hapo ndio tungemshutumu Mkuu. ..............
.....Ndugu Dar Es Salaam...kwa hili nakuunga mkono na kw ahiyo swali la msingi la kujiuliza ni

1. Standby Generator Ipo au haipo?
2. Kama ipo nani yuko resonsible nayo? (nafikiri hapa ni uongozi mzima)
3. Kama haipo WHY?.....je ni suala la bajeti? je ilikuwa knocked out kwenye bajeti? (again hapa ni uongozi mzima unawajibika)

.........kuna vitu vingine ni very basic katika institution nyeti kama hii ambayo huwezi kukwepa kwa kusingizia bajeti au sababu yeyote ile......ni lazima kuwepo na Standby Generator tena iwe ina-chekiwa na kupashwa moto mara kwa mara

Kwanini JK analaumiwa........
mikataba mibovu na kushindwa kwake kuwashughulikia viongozi wabovu ndio unasababisha uzembe kama huu uliotokea Muhimbili.........this may not be seen by many of us.....lakini ndio ukweli wenyewe.....................kila mtu serikalini ameuchapa usingizi mnono.........mikataba mibovu hawaioni na hata wakiona hawasomi na hata wakisoma hawaelewi na hata wakielewa.............kwa sababu ya interest ambazo hazijulikani.............WANASAINI!!!............shame on them!!!..................all these blunders have a knock on effect ktk idara nyingine za serikali kiuchumi na ndio sababu mambo kama yaliyotokea Muhimbili yanakuwepo
 
zomba

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2007
Messages
17,071
Points
0

zomba

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2007
17,071 0
Naona ndugu hapo hujaelewa kinachozungumziwa kabisa
Kwanza nikueleze, kikwete hajaonyesha dalili zozote za kiukweli zaidi ya unafiki mtupu katika kulitafutia swala la rushwa suluhu, kwa sababu nyingi tu, unakumbuka watu walipowataja mafisadi wakuu alitoa kauli gani ya kuwajibu wapinzani? lakini umeyaona yaliyoibuliwa na Slaah sasa,
Unakumbuka wakati anaongea na wazee wa mkoo wa Dar alieleza nini kuhusu EL na baadae alieleza kitu gani kuhusu Kamati teule ya BUNGE, kama unayo majibu hapo utakubaliana nami kuwa JK anatupuliza uku akitungata.
Na kinachozungumziwa hapa, sio kuwa JK anatakiwa kukumbusha mppaka mafuta ya Generate, swana ni kwamba kutokana na kasumba mbovu ya kuindesha serikali, ambapo anashindwa kuwawajibisha mawaziri wake, haya ndo yanatokea, na ndo maana watu wanamuona JK kama responsible person, kwa sababu hafanyti kazi zake huko juu, kama juu hawawajibiki inategemea nini huku chini kaka??
Tafakari haya mambo kaka
Kama mimi sijaelewa kinachozungumzwa nadhani na wewe hujaelewa kabisa nnchozungumza mimi, simply, Jee, unataka kumlaumu JK kwa kucheleweshwa kuwashwa genereta muhimbili? Ukisha jibu hilo itakuwa umeelewa nichozungumza.

Kuhusu maswala ya ufisadi na rushwa nadhani unajuwa ni nini JK anachokifanya kwa uozo alioukuta. Sina haja yakurudia rudia, tume zipo na kazi zinazofanyika zinajulikana kwa wanaotaka kuona.

Kuhusu kuwajibisha mawaziri wake, duhhh, unanishangaza, yaani hata mwezi haujapita, haujayaona ya kina Lowassa, karamagi na msabaha. Wacha kuwajibisha mawaziri. JK kaweka history ya kumuwajibisha waziri mkuu.

Kuhusu kuto-kufanya kazi zake, na hili pia unanishangaza sana tena sana, wewe unaujuwa uozo aliouruthi JK? au huujuwi? kama unaujuwa sina haja ya kuanza kukutajia mmoja mmoja, kama huujuwi niambie nikutajie na nikujulishe anaushghulikia vipi kama hujui.
 
zomba

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2007
Messages
17,071
Points
0

zomba

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2007
17,071 0
Wanabodi ,

Ni jambo la kusikitisha kuona watoto wadogo wakipoteza maisha kutokana na uzembe wa watu wachache ! Ni lazima wawajibishwe wale wote waliohusika na kitendo hiki cha kizandiki. Pili napendekeza serikali isitishe mara moja mchezo wa kutibu viongozi nje badala yake watibiwe hapo nyumbani ili Hospitali hiyo ya Muhimbili iweze kuboreshwa.
Kwa hili Mkuu Rufiji nakuunga mkono mia kwa mia.
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,878
Points
2,000

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,878 2,000
Jamani Jenereta ya kukaa standby kama pale Muhimbili inagharimu karibu dola laki moja hivi na kidogo. Kimsingi mnachosema ni kuwa katika Wizara yetu ya Afya hakukuwa na mtu yeyote ambaye angeweza kuchukua dakika chake kuangalia mtandao na kugundua kuwa zipo "Standby Generators" ambazo tunaweza kuzimuda na tunaaweza kununua moja kwa moja toka kwa watengenezaji.

kwa vile mimi ni mzalendo nimewapa website ya kampuni ambayo ni "maslahi" kidogo. Nawashauri wawasiliane nao na wakiulizwa nani amewarefer waandike, http://www.klhnews.com ili na miye nipate katenda kidogo.

http://www.generac.com/Default.aspx
 
zomba

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2007
Messages
17,071
Points
0

zomba

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2007
17,071 0
.....Ndugu Dar Es Salaam...kwa hili nakuunga mkono na kw ahiyo swali la msingi la kujiuliza ni

1. Standby Generator Ipo au haipo?
2. Kama ipo nani yuko resonsible nayo? (nafikiri hapa ni uongozi mzima)
3. Kama haipo WHY?.....je ni suala la bajeti? je ilikuwa knocked out kwenye bajeti? (again hapa ni uongozi mzima unawajibika)

.........kuna vitu vingine ni very basic katika institution nyeti kama hii ambayo huwezi kukwepa kwa kusingizia bajeti au sababu yeyote ile......ni lazima kuwepo na Standby Generator tena iwe ina-chekiwa na kupashwa moto mara kwa mara

Kwanini JK analaumiwa........
mikataba mibovu na kushindwa kwake kuwashughulikia viongozi wabovu ndio unasababisha uzembe kama huu uliotokea Muhimbili.........this may not be seen by many of us.....lakini ndio ukweli wenyewe.....................kila mtu serikalini ameuchapa usingizi mnono.........mikataba mibovu hawaioni na hata wakiona hawasomi na hata wakisoma hawaelewi na hata wakielewa.............kwa sababu ya interest ambazo hazijulikani.............WANASAINI!!!............shame on them!!!..................all these blunders have a knock on effect ktk idara nyingine za serikali kiuchumi na ndio sababu mambo kama yaliyotokea Muhimbili yanakuwepo
Mkuu, 1, 2, 3, hapo juu ni kweli kabisa na naunga mkono.

Ukishuka chini kuhusu mikataba mibovu, nadhani JK kisha weka tume huru ya kuichunguza yote hii. Ulitaka afanye nini zaidi ya hilo. Mikataba mingi sana kairithi na akienda nayo kwa pupa itamtokea puani, nadhani action yake kuunda tume ni muruwa na sahihi kabisa, tungoje Mheshimiwa Zitto kabwe na wenzake watatushauri nini baada ya kuipitia. Au unasemaje?

Yes, waliosaini mikataba mibovu wakakaaa kimya wakijuwa ndio imeshatoka hiyo, JK ndie atawaumbua hao, na kwa mara ya kwanza tunaona hata bunge limekubali kuweka library ya mikataba, kwa juhudi za nani? nani kiongozi wa nchi hii? utajaza mwenyewe hapo.

Hayo ma blunders unayoyasema nakubaliana na wewe mia kwa mia na hayo ndio urithi wa JK kwa aliomtangulia na JK ndio anajitahidi kurekebisha mambo na juhudi zake tunaziona. kafikia mpaka kumuaibisha sitta kwa kumteua Mheshimiwa Zitto kwenye kamati. Nadhani na hili pia unalijuwa. Kwa hiyo Tungoje tume zitasemaje.
 
BabaH

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2008
Messages
704
Points
195

BabaH

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2008
704 195
Jamani Jenereta ya kukaa standby kama pale Muhimbili inagharimu karibu dola laki moja hivi na kidogo. Kimsingi mnachosema ni kuwa katika Wizara yetu ya Afya hakukuwa na mtu yeyote ambaye angeweza kuchukua dakika chake kuangalia mtandao na kugundua kuwa zipo "Standby Generators" ambazo tunaweza kuzimuda na tunaaweza kununua moja kwa moja toka kwa watengenezaji.

kwa vile mimi ni mzalendo nimewapa website ya kampuni ambayo ni "maslahi" kidogo. Nawashauri wawasiliane nao na wakiulizwa nani amewarefer waandike, http://www.klhnews.com ili na miye nipate katenda kidogo.

http://www.generac.com/Default.aspx
Asante sana mwanakijiji kwa kuangaika na kutuletea mahala tunapoweza kupata Gerereta,
tatizo ni kwamba kwa bei hiyo ya Generate watu wanaona hawawezi kuweka dili zao humo ndani ili wajenge migorofa, kwa sababu hizo hawaoni umuhimu wake, Mimi bado nasema serikali ya kikwete ndi mbovu sana,
watu wanaajiliwa na kulipwa laki tatu mpaka tazo, ila utakuta ana minyumba ya ajabu, ukimuuliza vipi bwana, anakwambia nafanya kazi serikalini, manake ni kwamba kuna matumizi mabaya sana ya fedha za walipa kodi uko hospitalini
 
zomba

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2007
Messages
17,071
Points
0

zomba

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2007
17,071 0
Kuna watu wantaka kupotosha kuwa genereta ilikuwa hakuna, nawashangaa sana, yaani hamkuisoma ile post ya mwanzo? inasema hivi:

" ...Walieleza kwamba baada ya kukaa gizani kwa muda wa dakika 10, umeme wa jenereta uliwaka ambapo waliruhusiwa kwenda kuwanyonyesha watoto wao...

Jenereta lipo, tatizo ni kwa nini liwake dakika 10 baadae?

Forum statistics

Threads 1,391,507
Members 528,420
Posts 34,083,107
Top