BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,845
Na hii ndio hospitali yetu ya rufaa! Nilidhani sehemu nyeti kama hiyo umeme ukizimika tu basi majenereta yanaanza kazi mara moja, kumbe sivyo! Wafungue kesi dhidi ya Muhimbili
Posted Date::2/28/2008
Umeme wakatisha maisha ya vichanga Hospitalini Muhimbili
*Ni baada ya kukatatika usiku wa manane
*Watano wadaiwa kufariki kwa kukosa hewa
Na Jackson Odoyo
WATOTO watano waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam, wanahofiwa kufariki dunia baada ya kukosa hewa kutokana na kukatika kwa umeme hospitalini hapo.
Habari kutoka hospitalini zinaeleza kuwa kabla ya tukio hilo, watoto hao walikuwa wakipumua kwa kutumia mashine kutokana na matatizo mbalimbali ya kiafya, ikiwamo wawili waliozaliwa wakiwa njiti.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hii hospitalini hapo jana, baadhi ya akina mama wanaouguza watoto wao (majina yanahifadhiwa) walisema kwamba, umeme ulikatika majira ya saa 9 usiku wa kuamkia jana.
Akina mama hao walisema, baada ya umeme kukatika, walizuiwa kwenda kuwanyonyesha watoto wao kutokana na giza nene kutanda katika maeneo mbalimbali, ikiwamo chumba walichokuwa wamelazwa watoto hao hospitalini hapo.
Walieleza kwamba baada ya kukaa gizani kwa muda wa dakika 10, umeme wa jenereta uliwaka ambapo waliruhusiwa kwenda kuwanyonyesha watoto wao.
Hata hivyo, walisema baada ya kufika, walikuta baadhi ya vitanda walikolazwa watoto vimezungushiwa mapazia ya kijani.
Umeme ulikatika majira ya saa tisa. Tukakaa gizani kwa muda wa dakika 10. Ndipo umeme wa jenereta ukawashwa. Tulipokwenda kuwanyonyesha watoto wetu, tukakuta vyumba vitano vimezungushiwa mapazia ya kijani huku wenzetu wakilia kwa uchungu wa kupoteza watoto wao, alisema mmoja wa akina mama hao.
Baadhi ya madaktari wa watoto hospitalini hapo, walikiri kwamba, kitendo cha umeme kukatika ndani ya dakika 10, ni hatari kwa afya ya mgonjwa yeyote anayepumua kwa kutumia mashine na kwamba, kwa watoto wachanga ni hatari zaidi japo hawajafahamu kama kweli vifo vyao vimetokana na kukatika kwa umeme.
Madaktari hao pia walikiri kwamba watoto hao walikuwa wachanga na wengine walizaliwa wakiwa njiti na kusisitiza kuwa kinachosababisha waweze kuishi ni mashine.
Kutokana na hali hiyo, walisema hawawezi kupinga wala kukubali kufariki kwa watoto hao kwani hawakuwa zamu ya usiku siku hiyo na kukiri kwamba umeme ulikatika.
Hebu fikiria. Ukiwa ndani ya lifti, halafu umeme ukatike ndani ya dakika 10 au zaidi utakuwa kwenye hali gani? Sasa, kumbuka kwamba wale ni watoto na ni wagonjwa. Wataweza kuishi? Kama kweli walikufa kwa kukosa hewa, inabidi tumshukuru Mungu kwa kuwanusuru wagonjwa wengine waliokuwa katika hatari hiyo,? alisema daktari mmoja kati yao.
Naye Afisa Uhusiano wa MNH, Aminieli Aligahesha akizungumza na mwandishi wa habari hii ofisini kwake, alikiri kukatika kwa umeme hospitalini hapo na kukiri kwamba kuna baadhi ya maeneo yaliyoathirika kazi hazifanyiki, lakini sehemu muhimu wanatumia umeme wa jenereta.
Alisema baada ya umeme kukatika, mafundi wao walitumia dakika 10 kuunganisha umeme katika maeneo yote ya muhimu, ikiwemo wodi ya watoto na kwamba walipowasiliana na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) waliambiwa kuwa kuna kifaa cha kusambazia umeme kina tatizo na umeme huo umekatika sehemu nyingi za Jiji na si Muhimbili peke yake.
Aligahesha alisema baadhi ya maeneo yaliyoathirika baada ya umeme kukatika hospitali hapo, ni jengo jipya la watoto (OPD), maabara maalum ya watoto, vyumba vya upasuaji, wodi namba 36 inayotumika kuhifadhi watoto waliozaliwa njiti ni wadi 'A' na 'B', vyumba vya wagonjwa mahututi (ICU) na vyumba vya kuhifadhia maiti (mochwari) na kwamba kwa sasa wanatumia umeme wa jenereta.
Mbali na maeneo hayo yaliyoathirika na tukalazimika kutumia umeme wa jenereta, maeneo mengine yaliyoathirika na tukalazimika pia kubadilisha mfumo wa huduma kama vile sehemu za usajili wa wagonjwa ambapo awali tulikuwa tunatumia kompyuta ila kwa sasa tunatumia usajili wa kawaida, alisema Aligahesha.
Hata hivyo, Afisa Uhusiano huyo hakukiri wala kukanusha kufariki kwa watoto hao, badala yake alimtaka mwandishi wa habari hii kuwasiliana naye baadaye baada ya kuwasiliana na wahusika wa wodi hizo.
Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hii umebaini kuwa maeneo mengine yaliyoathiriwa na tatizo hilo, ni Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) ambako wamelazimika kutumia umeme wa jenereta.
Afisa Uhusiano wa MOI, Almas Jumaa alikiri na kusema japo umeme ulikatika, lakini maeneo ya muhimu yote hayakuathirika kwa sababu jenereta yao ni kubwa na imeunganishwa moja kwa moja kiasi kwamba umeme ukikatika ndani ya sekunde mbili unawaka tena.
Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili, Profesa Leonard Lema jana jioni alikataa kuzungumzia suala hilo kwenye simu na kusema kwamba kama gazeti linahitaji taarifa mwandishi amfuate ofisini.