Umeme huoo umepaa kwa 40%

Mwandishi: mheshimiwa waziri ngeleja huoni kuwa bei ya umeme iko juu sana kiasi kwamba wanachi wa vijijini na wafanyakazi wa kawaida hawataweza kumudu gharama hizo na bidhaa nyingi zinazozalishwa viwandani vitapanda bei.

Waziri: Hilo limezingatiwa lakini gharama lazima zipande kwani gharama za uzalishaji ziko juu sana na Kama mnavyovua tanesco wana mzigo mkubwa sana wa Deni la Dowans. Wananchi ambao wataona kuwa gharama hizo ziko juu na hawawezi kuzimudu basi warudi vijijini au watumie vibatari.

Ingekuwa wizara ya bwana Dr. John Pombe Magufuli tusingelala hapa JF!!!!!!!. :shock:
Bwana mdogo Ngeleja anachapa usingizi tu, shamba la bibi kuna shida gani?
Kwani malipo ya Dowans lazima yawekwe wazi kwamba sasa wanalipwa?
Si mliataka kutumia NGUVU YA UMA kuyapinga? sasa tunalipa kimya kimya:A S embarassed:
 
kuanzia unit 0 hadi 50,ongezeko hili haliwagusi,ila ukinunua unit zaidi ya 50,basi ongezeko limekugusa

Mkuu nisaidie. Kwa hiyo, kama natumia units 90 kwa mwezi, ninachoweza kufanya ni kununua mara mbili. 45 units and then 45 units!
hapo imekaaje?
 
Na baada ya miezi sita utapanda tena (japo wamsema watathmini ipande au ishuke ) lakini THUBHUTU......ishuke?? yaani hiyo 150% iliyoombwa lazima ifike kiana, utasikia misamiati ile ya ya KUKOKOTOA, MCHAKATO, KUOANDA GHARAMA ZA UENDESHAJI nk
 
AFU MAJAMAA WAPUMBAVU KWELI HEBU ANGALIA HIZI STATEMENTS
Masebu alisema ongezeko hilo ambalo ni la dharura, litadumu kwa muda wa miezi sita
ANGALIA TENA HUYO HUYO MASEBU SIJUI

"Tumezingatia weledi wa hali ya juu, tumeona wanastahili japokuwa mambo mengine walisema ni dharura lakini baada ya kupitia, tumeona si dharura,"alifafanua Masebu.

TUMEISHAPIGWA KITU NGOJA TUENDELEE KUUGULIA
 
Nimekuwa nikijiuliza hivi hii serikali ya ccm huwa inakusanya vipi takwimu zake maana ukisikia zingine utashangaa kama kweli zimekusanywa kitaalamu au ni usanii mtupu.

Nimeshawishika kuamini kuwa hakuna tafiti ila usanii kwa vile linapokuja swala la umaskini utasikia watanzania wengi ni maskini wanatumia chini ya $1 kwa siku lakini linapokuja swala la umeme utasikia mlalahoi ni yule anayetumia chini ya unit 50 kwa mwezi jambo ambalo sio kweli! Ninaamini kama utafiti ukifanyika maskini wengi wenye umeme majumbani wanatumia zaidi ya huo na pia tanesco wamekuwa waongo maana kila mwenye mita ya luku sio mlalahoi kwani hazina hiyo tariff ya maskini bali watumiaji wa kati.
Fredmlay nakuapia kwa jina la Mungu hai aliye juu, mimi nyumbani kwangu natumia units chini ya 50 kwa mwezi!. Nyumba yenyewe ina taa moja tuu ya energy server na ina socket moja ambayo situmii kitu chochote kwa socket hiyo zaidi ya kuchajia simu!. Angalau sisi walala hoi this time Tanesco wametukumbuka!.

Kuna wakati ilitokea shughuli tukanunua umeme zaidi ya zile unit 50!. Amini usiamini!,,bei ya kila unit ni mara 3 ya bei ya zile unit 50 za mwanzo!. Yaani ukizidisha hizo unit 50, unaadhibiwa!.
 
Utter useless and brainless government. Watu wametoka kwenye msiba (mgao) hapo hapo ndio unawaumiza na 'bei mpya"?
 
baada ya kupandisha bei ya mafuta ya taa, wamefanikiwa kuwachakaza watu kule vijijni sasa wameamua kumalizia mjini kwa kupandisha bei ya umeme. MUngu anawaonesha watanzania jinsi ccm inavyowakandamiza ila hawasikii. then eti wanasema mabadiliko hayatawahusu watumiaji chini ya unit 50 nani kawadanganya? hivi huyo mwenye kiwanda ukimpandishia gharama za uzalishaji nani atakayezilipa kama siyo mtumiaji? hakuna namna ya kukwepa hili? Umeme wenyewe upo?
 
Fredmlay nakuapia kwa jina la Mungu hai aliye juu, mimi nyumbani kwangu natumia units chini ya 50 kwa mwezi!. Nyumba yenyewe ina taa moja tuu ya energy server na ina socket moja ambayo situmii kitu chochote kwa socket hiyo zaidi ya kuchajia simu!. Angalau sisi walala hoi this time Tanesco wametukumbuka!.

Kuna wakati ilitokea shughuli tukanunua umeme zaidi ya zile unit 50!. Amini usiamini!,,bei ya kila unit ni mara 3 ya bei ya zile unit 50 za mwanzo!. Yaani ukizidisha hizo unit 50, unaadhibiwa!.

Duh. Poa tu .Lakini mko wangapi?
 
NI bora tuwe na umeme wa uhakika hata kama wa bei juu,kuliko kuukosa kabisa,si lazima tulalamike kwa kila kitu tu,kama vipi tumieni njia mbadala solar,jenereta nk mkishindwa VIBATARI VIPO

umefikiria bei za bidhaa zitakavyopanda au unafikiria umeme kama mwanga wa taa na kuangalia tv tu. Hili ni balaa jingine hata kwa mwanchi aliyeko kijijini kule kisokolokumwino. Think big mkuu not like the above.
 
Na baada ya miezi sita utapanda tena (japo wamsema watathmini ipande au ishuke ) lakini THUBHUTU......ishuke?? yaani hiyo 150% iliyoombwa lazima ifike kiana, utasikia misamiati ile ya ya KUKOKOTOA, MCHAKATO, KUOANDA GHARAMA ZA UENDESHAJI nk

The way the cookie crumbles.......
 
Fredmlay nakuapia kwa jina la Mungu hai aliye juu, mimi nyumbani kwangu natumia units chini ya 50 kwa mwezi!. Nyumba yenyewe ina taa moja tuu ya energy server na ina socket moja ambayo situmii kitu chochote kwa socket hiyo zaidi ya kuchajia simu!. Angalau sisi walala hoi this time Tanesco wametukumbuka!.

Kuna wakati ilitokea shughuli tukanunua umeme zaidi ya zile unit 50!. Amini usiamini!,,bei ya kila unit ni mara 3 ya bei ya zile unit 50 za mwanzo!. Yaani ukizidisha hizo unit 50, unaadhibiwa!.

Bado hujakumbukwa kwa lolote. Ngoja uone bei ya vitu itakavyopanda, kuanzia ndoo ya maji kwenye lile bomba la jirani mnaloenda chota maji. Kwa taarifa yako bei itamwathiri hata mtu asiyetumia umeme ambaye yuko kule kijiji ambako hawajawahi kuona hata nguzo ya umeme. Shtuka..........!!!!!! Umeme ni zaidi ya mwanga, kuangalia TV na kusikiliza radio.
 
Halafu umepanda wakat ambao atleast unapatikana,wale wanaotumia unit 0-50,hauwagusi,wanaopinga wakate rufaa kwenye tume ya ushindani ya biashara

Asavali. Lkn wale unaowagusa ndio wanakoboa sembe tunayokula, je na wao wakipandisha bei ya sembe, si yale yale ya nauli za kivuko na guta?!
 
Tanesco kweli hawaeleweki, mita za luku baadala ya kuonyesha units za umeme zina display tsh. Kwa mtumiaji umeme relevant information ni units za umeme zilosalia siyo balance ya pesa! Mfano gauge ya petoli inaonyesha ujazo wa mafuta yaliyosalia kwenye tank in litres, siyo balance ya petroli in tsh equivalent which in itself is a pretty useless piece of information.
 
Fredmlay nakuapia kwa jina la Mungu hai aliye juu, mimi nyumbani kwangu natumia units chini ya 50 kwa mwezi!. Nyumba yenyewe ina taa moja tuu ya energy server na ina socket moja ambayo situmii kitu chochote kwa socket hiyo zaidi ya kuchajia simu!. Angalau sisi walala hoi this time Tanesco wametukumbuka!.

Kuna wakati ilitokea shughuli tukanunua umeme zaidi ya zile unit 50!. Amini usiamini!,,bei ya kila unit ni mara 3 ya bei ya zile unit 50 za mwanzo!. Yaani ukizidisha hizo unit 50, unaadhibiwa!.
Nyumba yangu yote bwana Pasco nimefunga energy server lakini matumizi ni unit 8 kwa siku, kikubwa kwenye uhitaji wa nishati hii ni matumizi ya pasi na kuchemsha maji ya kuogea ili kuokoa mazingira vinginevyo huduma hizo itabidi kutumia mkaa ambao ni uharibifu wa mazingira
 
TANESCO-Tanzania No electricity Supply Company,

Nasikitika na hulka za watanzania kuwa wapole na wajinga namna hii,Nigeria serikali ilipotoa ruzuku kwenye mafuta ya petroli na kusababisha bei kupaa,wanachi chini ya vyama vya wafanyakazi walisimama kidete kuonyesha kutokubaliana na hali hii...Matatizo ya Nigeria ni madogo unapofananisha na Tanzania.Huku kila kitu ni gharama na watanzania tumeridhika tunamchekea yule jamaa pale magogoni...

Nani wa kuyasemea haya?
Kwa hakika nimekuja kugundua kuwa mtu wa kuyasemea haya ni zaidi ya CDM na vyama vingine vya upinzani vya kweli,ukiangalia nchi zote ambazo wananchi wake wako makini na utendaji wa serikali zao vyama vya wafanyakazi,wanaharakati na taasisi nyingine za zisizo za kiserikali ndio walichukua hatu kujitoa muhanga kwa ajili ya wananchi...nauliza hapa Tanzania wapi JUKWAA LA KATIBA,WAPI KITUO CHA HAKI ZA BINADAMU,WAPI TUCTA,WAPI WAPI CWT,WAPI TUGHE,WAPI RAAWU,WAPI THTU,WAPI FIBUKA nk...hawa ndio wanaweza kuchukua hatua za kweli kupambana na uharamia huu wa serikali ya CCM na si vinginevyo....

Nawasilisha!!
 
Nyumba yangu yote bwana Pasco nimefunga energy server lakini matumizi ni unit 8 kwa siku, kikubwa kwenye uhitaji wa nishati hii ni matumizi ya pasi na kuchemsha maji ya kuogea ili kuokoa mazingira vinginevyo huduma hizo itabidi kutumia mkaa ambao ni uharibifu wa mazingira

ili kutovuka 50 units tanesco threshold inabidi kuinstall solar/wind power units kugenerate ziada ya units unazotumia kwa mwezi ie 240 minus 50.
 
Watanzia tuna mbinu mbali mbali za kupambana na matatizo yetu.
kwenye hili, wafanyakazi wa TANESCO watanufaika kwa vishoka.
wananchi ndio watazidi kuiba umeme.
At the end of the day: TANESCO 0, wananchi 0
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom