Umeme huoo umepaa kwa 40%

Umeme huoo umepaa kwa 40%

Mkuu nisaidie. Kwa hiyo, kama natumia units 90 kwa mwezi, ninachoweza kufanya ni kununua mara mbili. 45 units and then 45 units!
hapo imekaaje?

hahahahah,u mean 45 pa month?nadhan ukinunua 2 tymz within a m0nth watakulapua coz ur beyond 50 units,
 
AFU MAJAMAA WAPUMBAVU KWELI HEBU ANGALIA HIZI STATEMENTS
Masebu alisema ongezeko hilo ambalo ni la dharura, litadumu kwa muda wa miezi sita
ANGALIA TENA HUYO HUYO MASEBU SIJUI


“Tumezingatia weledi wa hali ya juu, tumeona wanastahili japokuwa mambo mengine walisema ni dharura lakini baada ya kupitia, tumeona si dharura,”alifafanua Masebu.

TUMEISHAPIGWA KITU NGOJA TUENDELEE KUUGULIA

wameupandisha umeme wakat murua kweli,hakuna kikao cha bunge,kuna adha ya mcwepande,na umeme unapatikana kiaina,
 
Fredmlay nakuapia kwa jina la Mungu hai aliye juu, mimi nyumbani kwangu natumia units chini ya 50 kwa mwezi!. Nyumba yenyewe ina taa moja tuu ya energy server na ina socket moja ambayo situmii kitu chochote kwa socket hiyo zaidi ya kuchajia simu!. Angalau sisi walala hoi this time Tanesco wametukumbuka!.

Kuna wakati ilitokea shughuli tukanunua umeme zaidi ya zile unit 50!. Amini usiamini!,,bei ya kila unit ni mara 3 ya bei ya zile unit 50 za mwanzo!. Yaani ukizidisha hizo unit 50, unaadhibiwa!.

unadhan umeokoka na hlo rungu la ewura?pole mzee,hivi unadhan wahind hawataongeza bei ya bidhaa zao?mlaji nani?
 
Thursday, 12 January 2012 18:28
0diggsdigg
YAPANDA KWA ASILIMIA 40.29, ONGEZEKO HALIWAHUSU WALALAHOI
Waandishi wetu
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imeidhinisha kupanda kwa bei ya umeme kwa asilimia 40.29 kuanzia kesho kutwa Januari 15 mwaka huu.Ongezeko hilo halitawahusu wateja wa hali ya chini, wanaotumia chini ya uniti 50 kwa mwezi pamoja na Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco), huku wafanyakazi wa shirika hilo wakitakiwa kulipa gharama za umeme kama watumiaji wengine.

Katika bei hizo, wateja wa hali ya chini wanaotumia chini ya uniti 50 kwa mwezi, bei itabaki kuwa Sh 60 kwa uniti wakati watumiaji wa majumbani wanaotumia zaidi ya uniti 50, bei hiyo itapanda kutoka Sh 195 hadi kufikia Sh 273 kwa uniti.

Watumiaji wa kawaida wakiwemo wenye biashara ndogondogo, bei imepanda kutoka Sh 157 hadi Sh 221 kwa uniti wakati watumiaji umeme mkubwa wa kati, bei imepanda kutoka Sh 94 hadi Sh 132 kwa uniti, wakati watumiaji umeme mkubwa hasa wenye viwanda na migodi, bei imepanda kutoka Sh 84 hadi Sh 118 kwa uniti na kwamba Zeco wamepandishiwa kwa asilimia 28.21 kutoka awali ambako, walikuwa wakilipa Sh 83 na sasa watalipa Sh 106 kwa uniti.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu, alisema bei hizo hazihusishi kodi na kwamba Tanesco walitaka umeme upande kwa asilimia 155 lakini, baada ya mamlaka hiyo kuchambua maoni ya wadau, iliamua upande kwa asilimia 40.29 ili maisha yasizidi kuwa magumu.

Masebu alisema ongezeko hilo ambalo ni la dharura, litadumu kwa muda wa miezi sita na kwamba baada ya hapo, Ewura itafanya tathmini nyingine ya kujiridhisha juu ya huduma zinazotolewa na Tanesco na matokeo yake yanaweza kupandisha au kushusha gharama ya umeme.

Alifafanua kwamba kwa sasa kuna mtaalamu anayeangalia gharama halisi ya umeme kama ni halali ama la, ili kulinganisha na sababu za kupandisha gharama zilizotolewa na shirika hilo.

“Tumezingatia weledi wa hali ya juu, tumeona wanastahili japokuwa mambo mengine walisema ni dharura lakini baada ya kupitia, tumeona si dharura,”alifafanua Masebu.

Aliongeza, “Tumewapa uwezo Tanesco wazalishe umeme bila kuwa na mgawo na ikibidi, wakope ili waweze kuwa na mtaji mkubwa zaidi.”

Masharti
Alisema moja ya masharti waliyowapa Tanesco, ni pamoja na kuwataka kuanza kusambaza umeme unaozalishwa katika vyanzo rahisi kama maji na kwamba umeme huo ukipungua, ndipo waanze kutumia ule unaozalishwa kwa gesi, mafuta mepesi na mazito.

“Umeme unaozalishwa katika vyanzo vya maji una unafuu na tumewaeleza kwamba umeme huo ndio wanatakiwa kuanza kuutumia ila ukipungua ndio waanze kutumia unaozalishwa kwa gesi na mafuta,” alisema Masebu.

Akizungumzia upatikanaji wa vyanzo vingine vya umeme, alisema unatakiwa ufanyike kwa kutangaza zabuni ili wawekezaji waweze kupatikana kwa urahisi huku Ewura nao wakihusishwa katika uingiaji wa mikataba mbalimbali.

Naye Mkurugenzi wa Umeme katika mamlaka hiyo, Anastas Mbawala, alisema shirika hilo limetakiwa kutekeleza mambo mbalimbali ambayo yataboresha ufanisi ili wateja wapate huduma nzuri.

Kwa mujibu wa Mbawala, mambo hayo ni kuunganisha wateja wapya zaidi ya 100,000 kila mwaka, kuboresha mifumo ya usambazaji umeme ili kuondoa hali ya kukatikakatika mara kwa mara.

Alitaja mambo mengine kwamba ni kuhakikisha umeme unaopatikana usiwe hafifu, makusanyo yasipungue asilimia 96 kwa mwezi na mfanyakazi mmoja kuhudumia wastani wa wateja 172.

Alisema Tanesco pia wametakiwa kutoa ripoti kila mwezi na kwamba kutakuwa na mfumo wa elektroniki wa upashanaji habari ili kusiwe na matatizo ya kutofautiana kwa ripoti zitakazokuwa zinatolewa.

Mchango wa Serikali
Awali, Masebu alisema kutokana na Tanesco kutaka gharama hizo kupanda kwa kiwango cha asilimia 155, Serikali iliamua kuingilia kati suala hilo ikiwa ni pamoja na kutotoza kodi katika mafuta yanayotumika katika mitambo ya kuzalishia umeme.

“Serikali imefuta kodi ya mafuta kwenye mitambo ya IPTL sasa Serikali itakuwa inalipa Sh 18 bilioni na kusamehe deni la Sh 136 bilioni kwa Tanesco,”alisema.

Sababu za Tanesco
Masebu alisema sababu walizotoa Tanesco za kupandisha bei ya umeme ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mvua kunakosababisha upungufu mkubwa wa umeme na kuathiri hali ya kifedha ya shirika hilo na uchumi kwa ujumla, Ewura waliikataa.

Alisema hoja hiyo waliitupilia mbali, baada ya kuwasiliana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ambayo iliwahakikishia kuwa hali ya mvua kwasasa ni nzuri.

Masebu alisema kutokana na uhaba wa mvua, Tanesco iliingia mkataba na kampuni ya IPTL kuzalisha megawati 100 kwa kutumia mafuta mazito, Symbion LLC kuzalisha megawati 112 kutumia gesi asilia na mafuta, pia ilisaini mkataba wa kuuziana umeme (PPA) na Aggreko kuzalisha megawati 100 kutumia mafuta ya dizeli.

Alisema shirika hilo pia lilifafanua miradi yake ambayo itakamilika mwaka huu ambayo ni megawati 220 ambayo itatumia mafuta mazito (HFO) na gesi.

Alisema licha ya Tanesco kueleza kwamba mikataba hiyo imesaidia kupunguza mgawo wa umeme, pia ilieleza kuwa imeongeza kwa kiasi kikubwa gharama za uendeshaji wa Tanesco.

“Kutokana na hali hiyo, Tanesco iliwasilisha maombi ya dharura Ewura, ikiomba kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 155, ombi ambalo lilikubaliwa na Waziri mwenye dhamana ya umeme,”alisema.

Mkurugenzi huyo, alisema shirika hilo pia lilitaka madeni yake yaingizwe kwenye bei mpya ya umeme lakini Ewura ilikataa hoja hiyo.

Maoni ya Dk Slaa
Wakati Ewura ikibariki ongezeko hilo la bei ya umeme , Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa, amesema urasimu wa Serikali kutoruhusu watu na kampuni binafsi kuzalisha umeme, ndicho chanzo cha kuwepo bei kubwa za nishati hiyo nchini.

Dk Slaa aliyasema hayo juzi wakati akihutubia wananchi wa Jiji la Mbeya, katika Viwanja vya Shule ya Msingi Nzovwe, ambako alisema tayari Bunge limeshapitisha sheria kuruhusu watu binafsi kuzalisha umeme lakini Serikali ndiyo haijaruhusu kutokana na urasimu wake.

Alisema hivi sasa Tanesco linafanya linavyotaka kwa kuwapandishia wananchi bei za umeme bila sababu za msingi kutokana na kukosa mpinzani katika biashara hiyo.

Dk Slaa alisema Serikali inatakiwa kuruhusu watu na kampuni binafsi kuzalisha nishati ya umeme, kama ilivyoruhusu kwa sekta zingine kumilikiwa na watu binafsi ili kuweza kuendelea kuzalisha umeme huo na kuchangia maendeleo mbalimbali ya kiuchumi nchini.

Alisema kwa kipindi kirefu, Tanesco inazalisha nishati hiyo lakini imekuwa ikifanya mambo inavyotaka bila kuangalia mustakabali wa watumiaji kwa kujipandishia bei za umeme itakavyo.

“Serikali inatakiwa kuondokana na ukiritimba huo na kutoa fursa kwa watu na kampuni binafsi kuzalisha nishati ya umeme kama inavyofanya kwa sekta zingine na sio kuendelea kuiangalia Tanesco pekee, kwa kuiachia kuzalisha umeme hali inayosabaisha utendaji mbovu katika sekta hiyo,” alisema Dk Slaa.

Alisema viongozi wa Serikali wanashidwa kubuni mbinu zitakazo wawezesha wananchi kuondokana na umasikini katika maisha yao, badala yake wanajali maslahi yao.

“Tatizo kubwa linaloisumbua Serikali yetu ni kwamba viongozi wanashindwa kuwa wabunifu wa kubuni na kubaini matatizo yanayowakabili wananchi wao, ndio maana miradi mbalimbali ya nchi imekufa wakati viongozi wapo, na hii ni sababu mojawapo inayosababisha kuwepo urasimu wa kutotoa fursa hiyo kwa watu na kampuni binafsi kuzalisha umeme,”alisema Katibu huyo wa Chadema.

Alisema wananchi wanaendelea kukubwa na adha kubwa ya kupandishiwa bei za umeme pasipo sababu za msingi, huku wengine wakiendelea kulala gizani kila mara kutokana na Serikali kushindwa kutoa uamuzi mgumu dhidi ya Tanesco na kushindwa kuruhusu watu binafsi kuzalisha umeme.

Habari hii imeandaliwa na Fidelis Butahe na Nora Damian, Dar, Godfrey Kahango,Mbeya,

My Comments

Mimi ninataka kufahamu hivi ni watanganyika wangapi wanaofahamu kwamba wanalipia gharama kubwa ya umeme ili kuwabeba Wazanzibari?!. Ama kweli Wazanzibari wako sahihi wanaoposema mzigo mzito mpe mnyamwezi (read Mtanganyika).

Wakati watumiaji wa kawaida wa Tanganyika wamepandishiwa bei ya umeme kutoka Tsh 195 hadi 273 kwa unit ambayo ni 40.29%, Wazanzibari waliokuwa wanalipia bei kidogo tangu awali, wamepadishiwa kwa 28.1% kutoka Tsh 83 hadi 106 kwa unit.

Je haya ndiyo makubaliano ya Muungano kutumiza watangayika at the expenses of Zanzibaris? Umeme tuzalishe sisi (Tangayika), halafu tuiuzie nchi nyingine (Zanzibar) kwa bei nafuu, hivi huu ni uchumi wa wapi?, hivi hii serikali ya CCM ina akili kweli? Ndiyo maana mara nyingine mimi nampenda Mch. Mtikila. Kwa ujinga huu wa CCM bora hata huo muungano uvunjike. Huu
uhusiano wa Chcko Chetu, Changu Changu bora ufe. I'm very dissapointed.

Hebu tujiulizi hivi leo mafuta yachimbwe huko Zanzibar, halafu yauzwe bei rahisi Tangayika eg US $ 106 kwa ltr, halafu Zanzibar yauzwe mathalani US $ 273 kwa ltr. Hivi kweli wazanzibari wanaweza kukubali huu upuuzi?

Pamoja na ZECO kubebwa na Watanganyika bado yeye ndiye
mdaiwa sugu wa TANESCO, FYI ZECO inadaiwa na TANESCO Tsh 5 billion, halafu tukisema haya leo tunaonekana eti tunahatarisha Munngano?

Kama EWURA wameweza kuwafutia msamaha watumishi wa TANESCO na kuwataka walipe kama watumiaji wengine EWURA wameshindwaje kuwaambia watumiaji wa ZECO walipe kama watumiaji wegine wa Tanganyika? Kama serikali ya SMZ inawapenda wananchi wake kuliko seriklai ya Muugnao basi SMZ ndiyo inatakiwa i-subsidized hilo pengo lakini TANESCO ipate malipo yake kama ilivyo kwa watumiaji wa Tanganyika. Mchumi yeyote na sio mchumia tumbo kama EWURA watakueleza hivyo.

Kwa ushuzi huu wa CCM, siasa kutumikia uchumi badala uchumi kutumikia siasa, ndiyo maana Tanzania ni nambari tatu ombaomba duniani. Ninajuta kuzaliwa Mtanganyika!
 
Bobuk swala la Zanzibar linakera hasa, na inaonekana kama vile tumepigwa zengwe maana wali tayari kulizungumzia kimamlaka hakuna kila mmoja anakwepa utafikiri ni bomu litakalo lipuka wakati wowote, mimi nafikiri wakati umefika watanganyika tupinge hili kwa nguvu zetu zote kama kuna haja ya wao kupata hiyo subsidy basi itokane na serikali yao (SMZ)
 
Kweli CCM wamefikia mwisho wa kufikiri na kutawala.
 
Waache watukamue mpaka tubaki mifupa mitupu si tuliwachagua wenyewe!
 
Thursday, 12 January 2012 18:28
0diggsdigg


My Comments

Mimi ninataka kufahamu hivi ni watanganyika wangapi wanaofahamu kwamba wanalipia gharama kubwa ya umeme ili kuwabeba Wazanzibari?!. Ama kweli Wazanzibari wako sahihi wanaoposema mzigo mzito mpe mnyamwezi (read Mtanganyika).

Wakati watumiaji wa kawaida wa Tanganyika wamepandishiwa bei ya umeme kutoka Tsh 195 hadi 273 kwa unit ambayo ni 40.29%, Wazanzibari waliokuwa wanalipia bei kidogo tangu awali, wamepadishiwa kwa 28.1% kutoka Tsh 83 hadi 106 kwa unit.

Je haya ndiyo makubaliano ya Muungano kutumiza watangayika at the expenses of Zanzibaris? Umeme tuzalishe sisi (Tangayika), halafu tuiuzie nchi nyingine (Zanzibar) kwa bei nafuu, hivi huu ni uchumi wa wapi?, hivi hii serikali ya CCM ina akili kweli? Ndiyo maana mara nyingine mimi nampenda Mch. Mtikila. Kwa ujinga huu wa CCM bora hata huo muungano uvunjike. Huu
uhusiano wa Chcko Chetu, Changu Changu bora ufe. I'm very dissapointed.

Hebu tujiulizi hivi leo mafuta yachimbwe huko Zanzibar, halafu yauzwe bei rahisi Tangayika eg US $ 106 kwa ltr, halafu Zanzibar yauzwe mathalani US $ 273 kwa ltr. Hivi kweli wazanzibari wanaweza kukubali huu upuuzi?

Pamoja na ZECO kubebwa na Watanganyika bado yeye ndiye
mdaiwa sugu wa TANESCO, FYI ZECO inadaiwa na TANESCO Tsh 5 billion, halafu tukisema haya leo tunaonekana eti tunahatarisha Munngano?

Kama EWURA wameweza kuwafutia msamaha watumishi wa TANESCO na kuwataka walipe kama watumiaji wengine EWURA wameshindwaje kuwaambia watumiaji wa ZECO walipe kama watumiaji wegine wa Tanganyika? Kama serikali ya SMZ inawapenda wananchi wake kuliko seriklai ya Muugnao basi SMZ ndiyo inatakiwa i-subsidized hilo pengo lakini TANESCO ipate malipo yake kama ilivyo kwa watumiaji wa Tanganyika. Mchumi yeyote na sio mchumia tumbo kama EWURA watakueleza hivyo.

Kwa ushuzi huu wa CCM, siasa kutumikia uchumi badala uchumi kutumikia siasa, ndiyo maana Tanzania ni nambari tatu ombaomba duniani.
Ninajuta kuzaliwa Mtanganyika!



This is very serious! please usifikie huko!
Hii ndio gharama ya kuendelea na muungano, ambao ni wa gharama kubwa sana kwa watu wa Bara. Wanasiasa Mamluki kama Jussa, hawalioni hilo na mizigo tunayolipishwa, wanatutukana kila siku, wanadharau hata wazee wetu, na wataendelea kufanya hivyo, kwa jeuri tunayowapa wenyewe. Wao wanapata kwa bei rahisi, sisi tunawabeba.
 
Hata siku moja EWURA hawawezi kuacha kupandisha bei ya bidhaa wanazosimamia. Katika bill ya umeme kila ukinunua utakuta imeongezewa 1% EWURA,3% REA na 18% VAT Kama tanesco wanauza umeme wa 40Billion ina maana EWURA hujipatia million 400 na REA hulipwa million 1200 kwa hiyo kila bei ikipanda na wao hupata ulaji hivyo hivyo kwenye mafuta. Haw a jamaa mishahara Yao minono ndio maana wana kiburi. Zanzibar waligoma kulipa bill mpya tangu mwaka jana 2011 January ilipopandishwa na bado wanalipa bei ya Tshs. 50 per Kwh. Siko bongo watu wa Unguja wakanushe. Ukiona taasisi inapanga bei kwa ubaguzi ujue imefikia ukomo wa kufikiria.Tariff ya zamani ilipangwa kiubaguzi kutokuzingatia gharama halisi matokeo yake ni haya. Siwatetei Tanesco ila gharama zao za kuendesha ni za kifisadi kwamba hata hawajui gharama halisi na kwa kuwa Serikali inaweka Board mbovu kama hiyo mpya naskia inaongozwa na a very corrupt retired General Mboma and failures like Luhanga and Masanja
What do you expect. Tanesco yenyewe wanapeana vyeo kindugu bila kuzingatia weledi na competence hapo hakuna kitu. Dawa tujaribu kuwaiga wanaigeria na mgomo kufuatia kuondolewa kwa ruzuku kwenye mafuta. Vinginevyo bunge la CCM liko mfukoni mwa wenye mitambo ya Symbion na Aggreko mbona EWURA hawataki kuzungumzia hiyo mikataba mibovu? Mwamba ngozi huvutia kwake!:A S 465:
 
NI bora tuwe na umeme wa uhakika hata kama wa bei juu,kuliko kuukosa kabisa,si lazima tulalamike kwa kila kitu tu,kama vipi tumieni njia mbadala solar,jenereta nk mkishindwa VIBATARI VIPO

una pesa ya kerosene
 
Hata siku moja EWURA hawawezi kuacha kupandisha bei ya bidhaa wanazosimamia. Katika bill ya umeme kila ukinunua utakuta imeongezewa 1% EWURA,3% REA na 18% VAT Kama tanesco wanauza umeme wa 40Billion ina maana EWURA hujipatia million 400 na REA hulipwa million 1200 kwa hiyo kila bei ikipanda na wao hupata ulaji hivyo hivyo kwenye mafuta. Haw a jamaa mishahara Yao minono ndio maana wana kiburi. Zanzibar waligoma kulipa bill mpya tangu mwaka jana 2011 January ilipopandishwa na bado wanalipa bei ya Tshs. 50 per Kwh. Siko bongo watu wa Unguja wakanushe. Ukiona taasisi inapanga bei kwa ubaguzi ujue imefikia ukomo wa kufikiria.Tariff ya zamani ilipangwa kiubaguzi kutokuzingatia gharama halisi matokeo yake ni haya. Siwatetei Tanesco ila gharama zao za kuendesha ni za kifisadi kwamba hata hawajui gharama halisi na kwa kuwa Serikali inaweka Board mbovu kama hiyo mpya naskia inaongozwa na a very corrupt retired General Mboma and failures like Luhanga and Masanja
What do you expect. Tanesco yenyewe wanapeana vyeo kindugu bila kuzingatia weledi na competence hapo hakuna kitu. Dawa tujaribu kuwaiga wanaigeria na mgomo kufuatia kuondolewa kwa ruzuku kwenye mafuta. Vinginevyo bunge la CCM liko mfukoni mwa wenye mitambo ya Symbion na Aggreko mbona EWURA hawataki kuzungumzia hiyo mikataba mibovu? Mwamba ngozi huvutia kwake!:A S 465:

ukiona hvo ujue hyo mikataba haikuhusu 1 kwa 1
 
Wajameni!! MBONA JK ALILISEMA KWENYE HOTUBA YAKE YA MAJUZI?
Alisema "hayo magharama ya uzalishaji na uendeshaji" kuwa yameongezeka na hakusema "ushauri wake, ushauri wa wataalamu wake wala ufuatiliaji wake kuhusu "hayo magharama kupunguzwa ama kuachwa kama zamani" so ILE NDIO ILIKUWA HODI YA KUPANDA KWA BEI.

Kama presidaa hana vikao na washauri pengine na anakuja "kulitaja tatizo" kwa wananchi wake "kama taarifa" bila suluhisho au walau mawazo yake, tungetarajia nini kifuate????
 
Bei impenda kwa miezi 6 tu, tunatafuta fedha ya kuwalipa Dowans then tukishamaliza kuwalipa tutawashushia tena bei.Watz tuna-deserve this sababu hatutaki mabadiliko kila siku ccm ccm.
 
ewura wana 1% katika gharama za umeme unazopigwa,kadri gharama inavyoongezeka wao wanafaidi,..conflict of interest ambayo hawataki kuisema.
 
Hii nchi inaendeshwa kiwendawazimu sana, kwani ukiacha matumizi ya watu wa kawaida wanaotumia umeme; kunaviwanda vingi vinavyotumia umeme kuzalisha bidhaa mbalimbali, Hivyo tutegemee ongezeko kubwa kwenye bidhaa mbalimbali zinazotoka viwandani, kwahiyo ongezeko hili linawahusu wa Tanzania wote pasipo kujarisha unatumia umeme au hutumii ila kuna kundi lita double hizo gharama hasa watakao zidi unit 50. Kazi tunayo sana. MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.?
 
Yah! hiyo ni short term solution ila ukiisha utanunua kwa bei mpya! Kuna haja ya kutafuta long term solution ya hili tatizo baada ya kuhoji na kujua sababu zilizopelekea kupanda kwa gharama hizo mana isije ikawa wananchi wanaingizwa kwenye gharama ili kuneemesha mafisadi.

Hilo ni suala la kawaida ktk taifa letu hili!
 
Nasubiri miujiza mingine ya wabongo lol....
Sitaizungumzia Zambia na sokomoko lake na kupanda kwa bei ya mkate kipindi kile....
Uganda na "walk to work"......
Congo na valangati la maandamano na mishumaa ya usiku...
Hapa kwetu kilitokea nini siku zile za giza uh? Bei za majenereta ya kichina zilipanda kweli sababu demand ilikuwa juu....
Nadhani kwa bei hizi tutarajie bei za solar na nishati mmbadala kama mkaa na kuni kupanda zaidi.....
Hili ni taifa la kipuuzi na raia wapuuzi sijawahi ona Makondoo kama ya tz!

Nakuunga mkono na miguu yote kwani hata kama kuna uvumilivu una mwisho
 
Back
Top Bottom