Umeme huoo umepaa kwa 40%

Umeme huoo umepaa kwa 40%

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imeidhinisha kupanda kwa bei ya umeme kwa asilimia 40.29 kuanzia kesho kutwa Januari 15 mwaka huu.Ongezeko hilo halitawahusu wateja wa hali ya chini, wanaotumia chini ya uniti 50 kwa mwezi pamoja na Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco), huku wafanyakazi wa shirika hilo wakitakiwa kulipa gharama za umeme kama watumiaji wengine.

Katika bei hizo, wateja wa hali ya chini wanaotumia chini ya uniti 50 kwa mwezi, bei itabaki kuwa Sh 60 kwa uniti wakati watumiaji wa majumbani wanaotumia zaidi ya uniti 50, bei hiyo itapanda kutoka Sh 195 hadi kufikia Sh 273 kwa uniti. Watumiaji wa kawaida wakiwemo wenye biashara ndogondogo, bei imepanda kutoka Sh 157 hadi Sh 221 kwa uniti wakati watumiaji umeme mkubwa wa kati, bei imepanda kutoka Sh 94 hadi Sh 132 kwa uniti, wakati watumiaji umeme mkubwa hasa wenye viwanda na migodi, bei imepanda kutoka Sh 84 hadi Sh 118 kwa uniti na kwamba Zeco wamepandishiwa kwa asilimia 28.21 kutoka awali ambako, walikuwa wakilipa Sh 83 na sasa watalipa Sh 106 kwa uniti.

Maoni yangu kuhusu bei hizi

Mwananchi wa kawaida kabla ya umeme kupanda ilikuwa Tsh 195 baada ya kupanda kwa 40.29% bei imekuwa Tsh 273 kwa unit. Wenye migodi ambao ni watumiaji wakubwa sana wa umeme nchini walikuwa wanalipa Tsh 84 baada ya ongezeko hili sasa watalipa Tsh 118 kwa unit. Hii maana yake mtumiaji wa kawaida analipa kwa zaid ya 130% ukilinganisha na bei ya wale wa migodini.

Ikumbukwe kuwa DHAHABU inayochimbwa kwenye migodi haiuzwi nchini, yaani inasafirishwa nje ya nchi, wenye migodi wana tax holiday, wenye migodi wanalipa less than 5% tu ya mapato yao kwa serikali ambayo kimsingi hatuna namna ya uhakika ya kuyapima. Hao hao wamesamehewa kodi ya mafuta ya kuendeshea mitambo yao. Jamani hata umeme nao walipe NUSU BEI???nini sasa tunachopata kama hata gharama za umeme kwao tumepunguza wakati wanatengeneza pesa nying na ndio watumiaji wa zaidi ya 50% ya umeme wa taifa hili???Hivi mapunguzo yote haya yanalenga kumnufaisha nani???Kwanini serikali imeamua kumuumiza mwananchi kwa maslahi ya wenye migodi????Hivi hata kwa nchi za wenzetu ukarimu huu upo kweli??Nini asili ya ucheshi huu uliopitiliza?Naimani kuwa haya yote hayafanyiki kwa bahati mbaya. Nini kifanyike??Wabunge haya mnayaona???

Aidha, Ewura inasema upandaji huu wa umeme hauta muathiri mwananchi wa kipato cha chini. Hii kauli inaqualify kuitwa ni ya kipuuzi na ya kipumbavu.Ikumbukwe kuwa walalahoi wengi wamepanga chumba kimoja kimoja, wakishakuwa zaidi ya walalahoi 6 kwenye hiyo nyumba ya kupanga hapo matumizi ya umeme ni zaidi ya hizo 50 units, hivyo ongezeko litawaguza.

Pia ikumbukwe pia kuwa walalahoi hawaidhi kwenye kisiwa chao wenyewe, hivyo kwa Serikali kupandisha bei ya umeme kwa wenye biashara ndogo ndogo kama vinyozi, wenye biashara za kati kama wenye mashine za kusaga nafaka na kubwa itapelekea wenye biashara hizo kupandisha bei za bidhaa zao ili kumudu gharama za uzalishaji. Hapa pia mlalahoi atakumbana na athari la ongezeko la bei za umeme iliyopelekea kupanda kwa bei ya bidhaa uso kwa uso. J​e Serikali (EWURA) inamaanisha nini hasa inaposema ongezeko la bei za umeme halita mgusa mlalahoi???Ningewaelewa kama wangesema ongezeko la umeme litawagusa wenye MIGODI tu kwani hawa DHAHABU wanaiuza nje ya nchi na mlalahoi haguswi na ununuzi wa Dhahabu, vinginevyo ni siasa tu.


Mwisho, Ewura itupe sababu za msingi za kupandisha umeme maana sababu zilizotolewa na Ewura na pamoja na Tanesco bado hazitoshi kupandisha gharama za umeme. Naimani wakati wanatoa sababu walizozitoa ukiwaangalia usoni wataona aibu au watavunga kwa kushika pua au kukohoa maana zimekaa kibabaishaji sana.


 
Fredmlay nakuapia kwa jina la Mungu hai aliye juu, mimi nyumbani kwangu natumia units chini ya 50 kwa mwezi!. Nyumba yenyewe ina taa moja tuu ya energy server na ina socket moja ambayo situmii kitu chochote kwa socket hiyo zaidi ya kuchajia simu!. Angalau sisi walala hoi this time Tanesco wametukumbuka!.

Kuna wakati ilitokea shughuli tukanunua umeme zaidi ya zile unit 50!. Amini usiamini!,,bei ya kila unit ni mara 3 ya bei ya zile unit 50 za mwanzo!. Yaani ukizidisha hizo unit 50, unaadhibiwa!.
duh...hivi mkuu kati ya wewe, mbowe na dr kimei nani ana taa nyingi? yaani watu
mkiwasha taa zenu mitaa yote inang'aa kama mchana halafu tunadanganyana humu?
 
What a country! Where the leaders just mind their own business only, hata tuki complain hivi kwa nini huwa hawatusikii?
 
Its not too late kaka let's us wake up and fight for our right, kweli sasa tunaelekea kwenye vitu ambavyo sina uhakika kama tutaabakia taifa llenye amani ya kuzuga hata kile kidogo ambacho tunacho wananyang'anya!!!
 
Yah kwa kweli naona sasa Serikali imeamua kututovuga au kututumbukiza kidole jichoni kabsaaaa. Nadhani kuna kitu inahitaji kutoka kwa wananchi ni sisi tu wananchi tunajifanya hatuelewi Serikali yetu inatutaka nini.
 
What a country! Where the leaders just mind their own business only, hata tuki complain hivi kwa nini huwa hawatusikii?

The country where its leaders do not understand why Tanzania is a poor despite presence of ample natural resources.
 
Wananchi hata mkicomplain no action will be tacken na mtapewa maelezo matamu mpaka mupoe. When are you going to tack actions. Bila ya action this will go on and on and on..........Kama wewe ulio mjini unafahamu na ana achia kama ilivyo je wengi walio vijijini na ndiyo wanaoathirika zaidi wafanye nini. Jaribu kuonea huruma wasio fahamu labda itakupa motisha ya kuchukuwa actions.
The most important human endeavor is the striving for morality in our actions. Our inner balance and even our very existence depend on it. Only morality in our actions can give beauty and dignity to life. ​
 
Kweli sikio la kufa halisikii dawa Tanesco pamoja na ewura si zipo chini ya hii serikali ya ccm? Kwanini wanapandisha bei ya umeme wakati bajeti ya mwaka huu ilishapita na mishahara hawajaongeza hili ongezeko la umeme sisi wafanyakazi tuliopanga tutafidia vipi hili ongezeko kwasasa naona vituo vya tution vitaongezeka na rushwa ndogo ndogo barabarani na hosipitali za serikali zitaongezeka.
 
Back
Top Bottom