Umeme huoo umepaa kwa 40%

Tafadhali nisaidie katika hili ni kwa jinsi gani inakula kwako nataka ami ni nunue unit nyingi kesho.

kwa mujibu wa Ewura,ukinunua kesho n b4 jan 15 haina tatizo,ila afta 14 jan ukinunua beyond 50units unaichangia Dowans
 
Mwandishi: mheshimiwa waziri ngeleja huoni kuwa bei ya umeme iko juu sana kiasi kwamba wanachi wa vijijini na wafanyakazi wa kawaida hawataweza kumudu gharama hizo na bidhaa nyingi zinazozalishwa viwandani vitapanda bei.

Waziri: Hilo limezingatiwa lakini gharama lazima zipande kwani gharama za uzalishaji ziko juu sana na Kama mnavyovua tanesco wana mzigo mkubwa sana wa Deni la Dowans. Wananchi ambao wataona kuwa gharama hizo ziko juu na hawawezi kuzimudu basi warudi vijijini au watumie vibatari.

hahahahahah,mafuta ya taa ameshusha BEI?
 
Ukitumia chini ya 50 ina maana ongezeko hulifikii au inakuwaje?tuelewesheni basi

kuanzia unit 0 hadi 50,ongezeko hili haliwagusi,ila ukinunua unit zaidi ya 50,basi ongezeko limekugusa
 
Halafu umepanda wakat ambao atleast unapatikana,wale wanaotumia unit 0-50,hauwagusi,wanaopinga wakate rufaa kwenye tume ya ushindani ya biashara
Hivi ni kweli chini ya unit 50 hawaguswi mbona nimesikia wakisema chini ya hapo utalipia sh 194 kwa unit
 
Watanzania wanahitaji msaada,
kama umeme unapanda bei, na huku mafuta yapo bei juu, sidhani kama ile kaulimbiu ya TUNZA MAZINGIRA YAKUTUNZE itakuwa na uhai tena.

Serikali ikubali kwamba imefilisika kwenye upande wa ubunifu na iwe sikivu kwa faida ya Watanzania, iepuke washauri elekezi kutoka nje maana hawaji kwa maslahi ya nchi....
 
Yaani hadi Serikali ya JK imalize muda wake 2015, umeme utakuwa umepandishwa bei mara 5 ktk miaka hiyo, tutabaki hoi.
 
Tamko lao hili hapa...hebu oneni sababu walizotoa kuhalalisha ugumu wa maisha kwa watz....naomba kuwasilisha......


SIXTH FLOOR, HARBOURVIEW TOWERS, SAMORA AVENUE, P O BOX 72175 DAR ES SALAAM, TANZANIA

TEL: (+255-22) 2123850; 2123853; 2123854; 2123856; FAX: (+255-22) 2123180

E-mail: info@ewura.go.tz Website: http.//www.ewura.go.tz

clip_image004.gif



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUHUSU UAMUZI WA BODI YA EWURA JUU YA MAOMBI YA DHARURA YA TANESCO YA KUPANDISHA BEI YA HUDUMA YA UMEME




Tarehe 9 Novemba 2011, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilipokea maombi la dharura kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la kuidhinishiwa ongezeko la bei za huduma ya umeme kwa wastani wa asilimia 155 ya bei ya sasa. Maombi haya yalisajiliwa Namba TR-E-11*-012.

Kulingana na maombi yaliyowasilishwa, katika mwaka 2010 na 2011 Tanzania ilikuwa na hali mbaya ya mvua katika maeneo ya mabwawa na hivyo iliathiri uzalishaji wa umeme. Hii ilisababisha nchi kuwa na upungufu mkubwa wa umeme na kuathiri sio tu hali ya kifedha ya TANESCO, bali pia na uchumi kwa ujumla wake.

Ili kumaliza tatizo hilo, TANESCO ilisaini mkataba na IPTL kuzalisha Megawati 100 kwa kutumia mafuta mazito (HFO); ilisaini mkataba wa kuuziana umeme (PPA) na Symbion LLC kuzalisha Megawati 112 kutumia gesi asilia na mafuta; na ilisaini mkataba wa kuuziana umeme (PPA) na Aggreko kuzalisha Megawati 100 kutumia mafuta ya dizeli.

Vilevile, TANESCO inatekeleza mradi wake wa Megawati 150 ambao utatumia gesi asilia pamoja na mafuta (dual fuel plant) na mradi mwingine wa Megawati 70 ambao utatumia mafuta mazito (HFO). Ukiacha miradi ya TANESCO ambayo itakamilika mwaka 2012, umeme unaozalishwa kupitia mikataba tajwa umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la mgao wa umeme hapa nchini. Hata hivyo, juhudi za kumaliza mgao wa umeme zimeongeza kwa kiasi kikubwa gharama za uendeshaji za TANESCO.

Katika kukabiliana na hali hiyo, TANESCO iliwasilisha maombi ya dharura EWURA ikiomba kuongeza bei za huduma zake kwa 155.

Kulingana na kifungu Na. 15(1)(3) cha Mwongozo wa Uwasilishaji Maombi ya Bei wa mwaka 2009 (Tariff Application Guidelines of 2009), Waziri mwenye dhamana (kwa hali hii) wa Nishati na Madini, aliwasilisha Hati ya Dharura (Certificate of Urgency) EWURA ili maombi husika yaidhinishwe haraka na sio kwa utaratibu wa kawaida.

Tarehe 11 Novemba EWURA ilipokea Hati ya Dharura kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini na hivyo kuanza mchakato wa kupitia maombi ya TANESCO baada ya kupata maoni ya wadau.

Kulingana na Kifungu Na.19(2)(b) cha Sheria ya EWURA (Sura 414 ya Sheria za Tanzania), tarehe 2 Desemba 2011, EWURA ilifanya mkutano jijini Dar es Salaam wa kukusanya maoni ya wadau, kuweka maombi husika katika tovuti ya EWURA, pamoja na kuwaandikia wadau wachache ili waweze kutoa maoni yao kuhusu uhalali wa maombi yaliyowasilishwa na TANESCO. Pia maombi tajwa yalitangazwa katika vyombo vya habari mbalimbali.

Baada ya kufanya uchambuzi wa maombi yaliyowasilishwa pamoja na kupata maoni kutoka kwa wadau mbalimbali, Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA ilikutana tarehe 12 Januari 2012 na kufanya uamuzi, pamoja na mambo mengine:

(a) Serikali imechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha kupunguza makali ya maisha kwa wa Tanzania kwa mosi; kufuta kodi ya mafuta kwenye mitambo, itakuwa inalipia Sh. bilioni 18 gharama za mitambo IPTL (Capacity Charges) na kusamehe deni la Sh. bilioni 136 kwa TANESCO.

(b) Kutokana na ukokotoaji uliofanywa na EWURA, kwa kuzingatia mzigo ambao Serikali imeubeba na pia kwa kuzingatia hali ya hewa ambayo inaweza kufanikisha upatikanaji wa mvua kwa wingi na hivyo kujaza kwenye mabwawa, bei ya umeme itaongezeka kwa wastani wa asilimia 40.29 kwa wateja wote isipokuwa wateja wanaotumia uniti 0 – 50 (0 – 50 kWh) kwa mwezi na ZECO, bei imepunguzwa kwa kwa asilimia 10. Na wafanyakazi wa TANESCO watalipa kama wateja wengine. Bei hizo zitaongezeka kama inavyoonekana katika Jedwali hapa chini.




(c) Bei zilizoidhinishwa zitaanza kutumika tarehe 15 January 2012 mpaka hapo uchambuzi wa kina utakapokamilika na hivyo kutolewa kwa Order nyingine.


Mkurugenzi Mkuu,


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji
 
Maisha bora kwa kila mtanzania.Tunatimiza ahadi.Asanteni sana kwa kura zenu
 
kwa nini hawajafanya unit moja sh 500? Hiyo mia 275 ni kidogo sana.
 
Vilevile, TANESCO inatekeleza mradi wake wa Megawati 150 ambao utatumia gesi asilia pamoja na mafuta (dual fuel plant) na mradi mwingine wa Megawati 70 ambao utatumia mafuta mazito (HFO). Ukiacha miradi ya TANESCO ambayo itakamilika mwaka 2012, umeme unaozalishwa kupitia mikataba tajwa umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la mgao wa umeme hapa nchini. Hata hivyo, juhudi za kumaliza mgao wa umeme zimeongeza kwa kiasi kikubwa gharama za uendeshaji za TANESCO.


Sasa hapo hiyo miradi ikikamilika(ahadi hewa?) ndo watashusha bei ya umeme au?
 
Hivi kumbe mpaka leo bado kuna watu mnasumbuka na umeme wa taifa la haula! Kanunueni solar panels, mtakua watumwa ktk serikali za kifisadi mpaka lini!?? wakey wakey!!
 
saa izi ni kufikiria kutumia unit zisizozidi 50! cko tayari kumlipia kikwete,lowasa na rostamu kwenye ile tuzo yao ya dowans. KIKWETE "SIWAJUI DOWANS"

Utayalipa tuu haya Mafisadi mkuu how? bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kupitia umeme tegemea zitapanda maradufu kwa mantiki si utakua umewalipa mkuu? Swala hapa kama una mudu nunua Solar Power
 
Yote Tisa Tanesco wameingia mikataba ya kuzalisha umeme wa dharura na Makampuni ya Rostam : Symbion na Aggreko kwa bei ya wastani wa senti za kimarekani arobaini USD 0.40 kwa exchange rate ya Tshs. 1700 kwa dola moja ni sawa na Tshs. 680 hapo hujazingatia upotevu alioongelea Eng. Mbawala. Tunataka majibu yafuatayo hivi EWURA wana akili timamu? Tanesco wananunua Umeme kwa Dola za Kimarekani lakini wao wanapanga bei ya Umeme kwa shilingi je hawa Tanesco inakula kwao kwani hawana kinga ya kuserereka kwa shilingi ! Je kuna uwezekano wa huyo fisadi kurekebisha bei yake kwa kuzingatia iliyopitishwa hilo pengo la tofauti ya bei serikali ya CCM inayowakilishwa na Ngeleja watatoa wapi hizo pesa. Tatu
 
hIVI UKINUNUA unit nyingi kabla ya hiyo tarehe si itasaidia, japo kwa miezi 4 mbele!

Itasadia japo si saana. Mie mwenyewe nimenunua kama unit mianane hivi, zitavuta kama miezi mitatu hivi

unafanyia tanesko?
Next tym ukinunua jitaid uwe na unit 50 ,beyond that itakula kwako

Tafadhali nisaidie katika hili ni kwa jinsi gani inakula kwako nataka ami ni nunue unit nyingi kesho.

Service CHARGE ZOTE ZA KILA MWEZI watakuja kukata baadae ukija kununua tena, ila itakuokoa kwenye bei ya umeme na sio service charge ambayo ni constant kila mwezi.
 
Yote Tisa Tanesco wameingia mikataba ya kuzalisha umeme wa dharura na Makampuni ya Rostam : Symbion na Aggreko kwa bei ya wastani wa senti za kimarekani arobaini USD 0.40 kwa exchange rate ya Tshs. 1700 kwa dola moja ni sawa na Tshs. 680 hapo hujazingatia upotevu alioongelea Eng. Mbawala. Tunataka majibu yafuatayo hivi EWURA wana akili timamu? Tanesco wananunua Umeme kwa Dola za Kimarekani lakini wao wanapanga bei ya Umeme kwa shilingi je hawa Tanesco inakula kwao kwani hawana kinga ya kuserereka kwa shilingi ! Je kuna uwezekano wa huyo fisadi kurekebisha bei yake kwa kuzingatia iliyopitishwa hilo pengo la tofauti ya bei serikali ya CCM inayowakilishwa na Ngeleja watatoa wapi hizo pesa. Tatu ongezeko la bei ya bidhaa huwa kwa kuanzia wateja huwa wanatafuta njia mbadala kwa Umeme watu wataacha kununua na vishoka wataongezeka ina maana Tanesco wataongeza wakaguzi kupambana na wizi nadhani happ EWURA na serikali wameingia kushoto huwezi ukaongeza bei na kutatajia kuongeza wateja labda hao wa 50Kw ambao ni vijijini nako Umeme hakuna this is crazy kazi kwa Rostam na akina Williams .Wabunge
mlidanganya tusubiri happ . Mnyika pamabana sasa ongezeko la nauli ya Kigamboni mi cha mtoto!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom