Umekumbwa na nini ex -wangu

Umekumbwa na nini ex -wangu

Hiv kwanini wote maex wenu wamechakaa hakuna mwenye Nuru. Mi wangu sasa hiv ni muke ya boss moja. sema amekuwa ni mshikaji tunapiga story tu tukikumbukana. Tunaishi maeneo tofauti.
ww bado unapiga show, be careful
 
Kama sina mtoto na wewe basi hakuna ushahidi kama wewe ni Ex wangu. Na kama tuna mtoto tumeachana basi umevuka kiwango cha Ex wewe ni mzazi mwenza. Kwahiyo mkuu sina Ex kabisa
 
Wiki hii nilipata safari ya kikazi mkoani kwetu Iringa -mafinga.
Baada ya kuisha kwa ukaguzi na kuandikia ripoti ya kazi zangu nikaamua kujisogeza nyumbani
sababu sijaenda kuwasalimu miaka kadhaa sasa tangu nipate ajira.

basi ndugu zangu nilifurahi sana kufika home, nikasalimu wazazi ndugu, jamaa na marafiki. ilipofika mida ya mchana nikawa nimetoka kwenda uwanjani kutafuta network(mtandao).

Kila napopiga hatua kuelekea mbele nikawa namuona mdada ambaye sura yake sio ngeni machoni pangu anaendesha baiskeli akiwa kambeba mama mtu mzima ambaye anakuja usawa wangu .

doh! vile amekaribia kumbe ni ex wangu ,yule aliye utesa moyo wangu . aliye nisulubu nikaona dunia chungu mpaka nikashindwa kufanya mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka huo.

Nikaita jina lake mara mbili akasimama, nikamsalimu uhali gani ? ulikumbwa na nini? ajabu sana ex wangu katika maongezi ya dakika tano bado alishindwa kunifahamu mi ninani? mpaka pale nilipo mwambia mimi ni fulani umenisahau.!!

Ex wangu alishindwa kujizuia akaanza kulia. Hali iliyo nifanya namimi nianze kujikaza kiume kutoa chozi sababu ex wangu kapoteza nuru ,tabasamu na muonekano, jamani Huyu mwanamke nilimpenda sana.

Nilipo muuliza ulikua wapi kipindi chote , katikati ya mapenzi yetu uliondoka bila hata kuniaga nilikukosea nini Akaniambia Mama alimpeleka Dar kwa wajomba zake kusoma!!

ebu funguka hapa chini ex wako yuko wapi, umewahi tenga muda kujua anajihusisha na nini kwasasa?
Mbona hujamalizia stori sasa?
....

Kitu kikishakuwa out of time
Uhangaike tena kujua kimeenda wapi?

Tutaonana Mbinguni.
 
Sio kila x lazima achakae muulizeni steve Nyerere na Welu alipomuacha akajua atafubaa mtoto akazidi kung'ara kuona vile steve acha roho imuume ikafikia hatua akijua unataka umpe dili Welu anakuja hata na magoti usiku wa manane na majungu kibaoo eti usimpe kazi yule atakuharibia blah blah blahh[emoji23][emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Usiombe ukutane na ex wa kike alie chakaa...Mademu wanatia huruma kama mbwa koko yaaani ni huwa wanachakaa haswa kama ulimpenda ukweli unaweza lia aisee kuna watu wanajua kuwachakaza wanawake aisee sio poa
 
Back
Top Bottom