Umekumbwa na nini ex -wangu

Objective football

JF-Expert Member
Oct 21, 2023
1,196
2,758
Wiki hii nilipata safari ya kikazi mkoani kwetu Iringa -mafinga.
Baada ya kuisha kwa ukaguzi na kuandikia ripoti ya kazi zangu nikaamua kujisogeza nyumbani
sababu sijaenda kuwasalimu miaka kadhaa sasa tangu nipate ajira.

basi ndugu zangu nilifurahi sana kufika home, nikasalimu wazazi ndugu, jamaa na marafiki. ilipofika mida ya mchana nikawa nimetoka kwenda uwanjani kutafuta network(mtandao).

Kila napopiga hatua kuelekea mbele nikawa namuona mdada ambaye sura yake sio ngeni machoni pangu anaendesha baiskeli akiwa kambeba mama mtu mzima ambaye anakuja usawa wangu .

doh! vile amekaribia kumbe ni ex wangu ,yule aliye utesa moyo wangu . aliye nisulubu nikaona dunia chungu mpaka nikashindwa kufanya mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka huo.

Nikaita jina lake mara mbili akasimama, nikamsalimu uhali gani ? ulikumbwa na nini? ajabu sana ex wangu katika maongezi ya dakika tano bado alishindwa kunifahamu mi ninani? mpaka pale nilipo mwambia mimi ni fulani umenisahau.!!

Ex wangu alishindwa kujizuia akaanza kulia. Hali iliyo nifanya namimi nianze kujikaza kiume kutoa chozi sababu ex wangu kapoteza nuru ,tabasamu na muonekano, jamani Huyu mwanamke nilimpenda sana.

Nilipo muuliza ulikua wapi kipindi chote , katikati ya mapenzi yetu uliondoka bila hata kuniaga nilikukosea nini Akaniambia Mama alimpeleka Dar kwa wajomba zake kusoma!!

ebu funguka hapa chini ex wako yuko wapi, umewahi tenga muda kujua anajihusisha na nini kwasasa?
 
Ni vizuri Kama kijana ukajitenga na ngono au Uzinzi maana hakuna faida utakayopata ukiachana na kutengeneza idadi kubwa ya singo Mama na kuua uchumi wako plus maradhi ya ngono

Kuhusu x wako ni kukosa kuiwekeza Akili yako katika Mambo muhimu.
sahihi chief,japo hali niliyo mkuta kwa kweli ili upasua moyo wang
 
Back
Top Bottom