Kilichomwondolea sifa ya kuwa mbuge ni kutojaza hizo fomu au kutojulikana alipo kama spika alivyo dai.
Mimi kwa mawazo yangu, naona ni mambo yaliyokuwa yamepangwa yafanyike.Kusema kwa spika hajui Lisu aliko halina mashiko, kwani asilimia kubwa ya watu, Tanzania akiwepo Ndugai na hata nje ya Tanzania wanajua Lisu yuko kwenye matibabu. Walikuwa wanamlipa mshahara na posho kwa kipindi chote. Viongozi mbalimbali wa serikali walishaenda kumwona na kumpa pole.
Kusema Ofisi ya spika haina taharifa za kimaandishi, haina maana kuwa hajui ila anatumia hicho kigezo kukwapua ubbunge wa Lisu.
Kwangu mimi uhai wa lisu ni muhimu kuliko ubunge, hapo wamempiga chura teke ili kumwongezea mwendo.
Ndugai, kabla ya kukalia hicho kiti, kulikuwepo wengine waliokikalia na sasa hawapo tena kwenye kiti hicho.
Hiyo ni daladala, ukifika kituoni utashuka tu.