Ndugu zangu,
Sheria ya viongozi wa umma inatamka wazi kuwa kila kiongozi wa umma kama ilivyoinishwa katika sheria anapaswa kutoa tamko la mali ndani ya siku 30 baada ya kutumikia nafasi ya uongozi husika na kila mwisho wa mwaka.
Fomu za kujaza tamko la mali na madeni zinapatikana katika tovuti ya Tume ya maadili ya viongozi wa umma.Hivyo basi Tundu hana sababu ya kutojaza fomu hiyo kwani anatakiwa kuingia katika tovuti ya Tume kudownload fomu hivyo na kuijaza na kuituma kwa DHL kwenye ofisi ya Tume ya maadili kwani katika kipindi chote hicho amekuwa akipata mshahara na marupurupu ya ubunge.
Kutokana na ushahidi kuwa Tundu amekuwa akizurura nchi mbalimbali hana sababu ya msingi kushindwa kuijaza fomu hiyo na kuiwasilisha Tume kwa njia yoyote ikiwamo kumtuma mwanasheria wake au nduguye.
Ni mjadala usiohitaji mihemko bali utulivu wa akili.
Nawasilisha