Umbumbumbu wa Sheria umemponza Lissu

Umbumbumbu wa Sheria umemponza Lissu

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,505
Reaction score
16,006
Ndugu zangu,

Sheria ya viongozi wa umma inatamka wazi kuwa kila kiongozi wa umma kama ilivyoinishwa katika sheria anapaswa kutoa tamko la mali ndani ya siku 30 baada ya kutumikia nafasi ya uongozi husika na kila mwisho wa mwaka.

Fomu za kujaza tamko la mali na madeni zinapatikana katika tovuti ya Tume ya maadili ya viongozi wa umma.Hivyo basi Tundu hana sababu ya kutojaza fomu hiyo kwani anatakiwa kuingia katika tovuti ya Tume kudownload fomu hivyo na kuijaza na kuituma kwa DHL kwenye ofisi ya Tume ya maadili kwani katika kipindi chote hicho amekuwa akipata mshahara na marupurupu ya ubunge.

Kutokana na ushahidi kuwa Tundu amekuwa akizurura nchi mbalimbali hana sababu ya msingi kushindwa kuijaza fomu hiyo na kuiwasilisha Tume kwa njia yoyote ikiwamo kumtuma mwanasheria wake au nduguye.

Ni mjadala usiohitaji mihemko bali utulivu wa akili.

Nawasilisha
 
Madam minister..
Japo nakuunga mkono kwenye chama na serkalii..hili la mh lissu sioni mantiki kwa mawazo yangu..

Ubunge uliobakia ni mwaka 1 tuu tungelipotezea tuu..haya ya sheria ya viongozi na maadili ni move/sababu za kishamba.
 
Kamanda dada sheria haina muda mdogo wala mkubwa
 
Vigezo na mashart kuzngatiwa kama hizo fomu zinzpatikana online alishindwaje kujaza sasa,mbona kwenda safari za mbali anaweza kwenda
kama mnaona anaonewa basi haina haja ya kuwa na sheria,kwani zinawekwa ili nani afuate?
 
Tatizo lake Tundu ni kusoma baadhi ya mistari ya sheria abayoipenda na kuipuuza inayombana
 
Madam minister..
Japo nakuunga mkono kwenye chama na serkalii..hili la mh lissu sioni mantiki kwa mawazo yangu..

Ubunge uliobakia ni mwaka 1 tuu tungelipotezea tuu..haya ya sheria ya viongozi na maadili ni move/sababu za kishamba.
Mkipotezea mtakuwa hamumtendei haki Tundu Lissu na siku moja yeye ataliibua hili na kusema bunge halifuati sheria - na atatolea mfano wake mwenyewe. "Atasema ushahidi ni mimi! Sikuwasilisha ripoti ya mali zangu lakini bunge la Ndungai halikuchukua hatua (in Lissu's voice)". Don't play with him, his not trusted.
 
Tatizo lake Tundu ni kusoma baadhi ya mistari ya sheria abayoipenda na kuipuuza inayombana
Unajua wewe ni mbulula kabisa. Mgonjwa mtumishi kitu gani kinafanya asiende kazini na mwajiri atambue kuwa ni mgonjwa?
Daktari anatoa kitu kina itwa ED.
ED ni nini? ED ni Exempt from Duty, ndiyo aliyopewa na madaktari ambayo Bunge linaitambua na ndio maana liliendelea kumlipa mishahara na stahiki nyingine kama mbunge.
Kwa nini hakujaza hizo form? Hakujaza document hiyo kwa vile ni tamko la kisheria na sehemu ya kazi na ugonjwa wake waweza kuifanya doc hiyo kukosa sifa kwani yuko kwenye ED.
 
Kamanda ukiugua miezi sita mfululizo kisheria unaachishwa kazi kwa sababu za ugonjwa.Usiwe mbumbumbu wa sheria.Kipindi cha majadiliano ya katiba mpya Tundu alikuwa anaponda sana wabunge wagonjwa hadi JK akamshangaa.Japo sheria hii haipo kwa wabunge.

Pili,mbona unakwepa swala la fomu ya tamko la mali?nini kimemzuia kujaza kwa mujibu wa sheria wakati mabalozi wanajaza?
 
Kilichomwondolea sifa ya kuwa mbuge ni kutojaza hizo fomu au kutojulikana alipo kama spika alivyo dai.

Mimi kwa mawazo yangu, naona ni mambo yaliyokuwa yamepangwa yafanyike.

Kusema kwa spika hajui Lisu aliko halina mashiko, kwani asilimia kubwa ya watu, Tanzania akiwepo Ndugai na hata nje ya Tanzania wanajua Lisu yuko kwenye matibabu.

Walikuwa wanamlipa mshahara na posho kwa kipindi chote. Viongozi mbalimbali wa serikali walishaenda kumwona na kumpa pole.

Kusema Ofisi ya spika haina taharifa za kimaandishi, haina maana kuwa hajui ila anatumia hicho kigezo kukwapua ubbunge wa Lissu.

Kwangu mimi uhai wa lisu ni muhimu kuliko ubunge, hapo wamempiga chura teke ili kumwongezea mwendo.

Ndugai, kabla ya kukalia hicho kiti, kulikuwepo wengine waliokikalia na sasa hawapo tena kwenye kiti hicho.

Hiyo ni daladala, ukifika kituoni utashuka tu.
 
Back
Top Bottom