Umasikini na aibu

Umasikini na aibu

Pole sana, ila nyakati ngumu hazidumu.

Ni wewe sasa kuvumilia kipindi hicho cha mpito
Kaka hali ilinipiga nikaona, isiwe KESI nilime mchicha, pale ULIPO mji wa serikali imejengwa makao makuu ya mahakama pale ka sikosei Hilo eneo nimepiga jembe hapo kulima mchicha enzi hizo hapajajengwa, weeee jembe unapiga linadunda njaaa Kali Hadi nataka kuanguka dahhh, alafu nimetoka kusimamishwa chuo maumivu yake moyoni daaaah
 
Siku utakayo wasamehe hao watu na kuachilia mambo yapite ndio siku Mungu atakayo fungua milango ya baraka kwako

Kila changamoto zina mwanzo na mwisho hakuna marefu yasio na ncha,

Kikubwa samehe
Oga
Vaa
Pendeza

Kingine, mwanaume anaekupenda kweli hawezi kukuomba nyuma yaani hawezi
 
Mi sioni kama kuna uhafueni kwakweli….tatz la akili ni kubwa sana…unakua una function ila linakuangamiza kama ukimwi au zaidi ukimwi..huwz kunielewa kwa sababu hujawai kupata iyo severe depression ni deadly sana… na kpnd icho ndo moyo wangu umeanza kuuma nilkue nimepata chance za kazi, ajira portal nilkua nimeitwa interview lkn mwili wangu ulkua huwz kunyanyuka…miguu nikama inakua kama imeshikwa ganzi unaitest kujua kama inawza kufnya kazi….unazimia,nguvu zinakuishia unaona ukae kwaza sehemu, upo kwny umati unaona kwanza utfte sehemu ulie,uwoga unaonkn kwnye sura yako,yaani huzuni wa kweli kweli, mikono inatetemeka ukjrbu ti kushika simu kujarbu kumpgia inatetemeka ki namna sijawai ona….. unakua mtu ambae sie acha kabsa inauwa…kpk miezi kama mi3 ipite ivi ndo kdg mwili wako untegneneza kinga…
Kwa mm naona bora nipate ttzo lolote ila sio severe depression.. mwili wako unagombana na akili yako na moyo wako vyote kuna vita kubwa ndani yako… unalia kwa sauti kama mjina moyo unashindwa ku istaimili…acha kbsa…. Akili ikitkswa kdg binadamu anaisha…….
Bahati nzuri hajaambukizwa ukimwi tena hao wa migodini geita wameua sana dada zetu wengi, naongea kama mwana geita napajua vizuri
kama
 
Kazi nimefanya zakujitolea na zakuwa busy sana…..ata mda wakupumzka nakosa…ila ata ndani siku nimebadlka nimekua kama zezeta imeniathiri mpk ki saikologia.. kuna kpnd nilkua naaibu ya kuangalia watu usoni..ni kitu tuu kinanitokea automatically najhs kama mtu hafai kuniangalia……na nikienda kulala navifikilia, mda wote mpk napitiwa na usingz ata kuota sazngn namuota kwnye mazingira kama nina gombana na uyo mbwana…au nipo kwnye mazingira mngn tofuati sizkmbk ndoto ila kuna namna kama uwa nipo kwnye mazingira yakupishana nae kwnye ndoto..yaan ni kama nina ile sonona yankweli kweli (severe depression) hainitoki ata nikiwa busy..….akili yangu ikiwa imesahau mwili wangu hausahau na watu wakiwa karbu ndo inajiactivate kabsa…..
Pole.
Utaysahau.
Fanata Kila unaloweza kusahau
Ndio liwe lengo lako
 
Pole sana, wewe ni mdada wa pili sasa kusema kuwa ulifanya kinyume na maumbile kisa kumridhisha, mwingine rafiki yangu aliniambia alifanya kinyume na maumbile na mchumba wake kutoka Uspania kisa kumridhisha....sijui inakuaje unamridhisha mtu kwa kumfanyia kitu cha namna hiyo.

Ushauri wangu: Rudisha akili yako nyuma kabla ya kukutana na huyo jamaa aliyekuumiza then anzia hapo kwenda mbele.
Asirudi nyuma mkuu nakataa, hapo alipo abadili plan. 30 miaka sio mingi kwa mwanaume ila mwanamke mingi sana.

Swali: sasa hiv ana uwezo wa kufanya nn kiuchumi? Aseme hapa kama kuna watu kiko ndan ya uwezo wao humhumu
 
Mi sioni kama kuna uhafueni kwakweli….tatz la akili ni kubwa sana…unakua una function ila linakuangamiza kama ukimwi au zaidi ukimwi..huwz kunielewa kwa sababu hujawai kupata iyo severe depression ni deadly sana… na kpnd icho ndo moyo wangu umeanza kuuma nilkue nimepata chance za kazi, ajira portal nilkua nimeitwa interview lkn mwili wangu ulkua huwz kunyanyuka…miguu nikama inakua kama imeshikwa ganzi unaitest kujua kama inawza kufnya kazi….unazimia,nguvu zinakuishia unaona ukae kwaza sehemu, upo kwny umati unaona kwanza utfte sehemu ulie,uwoga unaonkn kwnye sura yako,yaani huzuni wa kweli kweli, mikono inatetemeka ukjrbu ti kushika simu kujarbu kumpgia inatetemeka ki namna sijawai ona….. unakua mtu ambae sie acha kabsa inauwa…kpk miezi kama mi3 ipite ivi ndo kdg mwili wako untegneneza kinga…
Kwa mm naona bora nipate ttzo lolote ila sio severe depression.. mwili wako unagombana na akili yako na moyo wako vyote kuna vita kubwa ndani yako… unalia kwa sauti kama mjina moyo unashindwa ku istaimili…acha kbsa…. Akili ikitkswa kdg binadamu anaisha…….

kama
Kwa siku unalala masaaa mangapi? Unatkiwa unywe Azuma na amitriptiline angalau mwezi mmoja. Upate muda wa kulala mzuri baada ya kula vizuri!

Sasa unajishughulisha na nn
 
Pole sana kwa masaibu yako,hata hivyo sio mwisho wa dunia,kama binadamu tuna mapito yetu,ofcoz kuna muda ni ngumu kukubaliana na ukweli wa mambo lakini huwezi amini huwa yanapita,cha msingi hapa usikate tamaa,lakini acha kujifungia ndani,ondoa aibu ma toka ukutane na watu,maisha yana suprise nyingi na hutufundisha kwa njia ngumu..kila kioa hubadilika ndani ya sekunde,trust the process kila kitu kitakua sawa.
Gods plan is always better.
 
Kwakuwa umehisi una tatizo la akili ukweli ni kwamba huna tatizo la akili, wenye matatizo ya akili huwa hawajui kama wana tatizo la akili.

1. Usikate tamaa.
2. Usikate tamaa.
3. Usikate tamaa.
Asante nipo napambana
Asirudi nyuma mkuu nakataa, hapo alipo abadili plan. 30 miaka sio mingi kwa mwanaume ila mwanamke mingi sana.

Swali: sasa hiv ana uwezo wa kufanya nn kiuchumi? Aseme hapa kama kuna watu kiko ndan ya uwezo wao humhumu
hhmmmm!!
 
Pole sana kwa masaibu yako,hata hivyo sio mwisho wa dunia,kama binadamu tuna mapito yetu,ofcoz kuna muda ni ngumu kukubaliana na ukweli wa mambo lakini huwezi amini huwa yanapita,cha msingi hapa usikate tamaa,lakini acha kujifungia ndani,ondoa aibu ma toka ukutane na watu,maisha yana suprise nyingi na hutufundisha kwa njia ngumu..kila kioa hubadilika ndani ya sekunde,trust the process kila kitu kitakua sawa.
Gods plan is always better.
Asante dear
 
Ndugu zangu, mimi nakabiliana na changamoto kubwa ya maisha yangu, ambayo sijawahi kuhisi kama ipo siku itanifikia. Ni kama nimechanganyikiwa, na ukweli nimechanganyikiwa. Najiona kabisa akili yangu haina uwezo wa kufikiri.

Tatizo langu la kwanza ni umaskini. Sidhani kama nishawahi kuishi katika hali ya kiumaskini. Nilikuwa na maisha yaliyokuwa yanaendelea kawaida, lakini sasa ndiyo nagundua kuwa mimi ni maskini na sina cha kujisaidia kabisa zaidi ya matumaini. Hata jana na mwaka jana nilijikuta nimemtukana Mungu na nimejikatia tamaa, nikitamani anipe adhabu yangu ya dhambi ambayo ni kifo. Namjaribu ili tu afanikishe suala lake.

Mimi ni mwanamke mwenye miaka 30. Hapo awali, nilivyomaliza chuo nilipata kazi na nilikuwa napata kama laki moja kwa mwezi. Trainings ndogo zikitokea tulikuwa tunalipwa, hivyo pesa zilikuwa zinaongezeka ila mpaka trainings zitokee.

Baadaye nikaja kupata kijikazi fulani nikawa nalipwa laki tano kwa mwezi, hapo nikiwa na miaka kama 25 hivi. Ila siyo laki tano tu, kuna programs ambazo zikitokea take home inakuwa laki tano, lakini muda mwingine account inaweza kusoma zaidi ya milioni mbili.

Kwa kweli nilikuwa natumia tu pesa zangu na kusomesha watoto wa dada yangu. Nina dada yangu ambaye alipata changamoto za maisha zilizompelekea mpaka kujiua.

Kwa hiyo nilikuwa natumia pesa zangu tu. Nilikuwa najiona bado mdogo na kwamba lazima ntaolewa na tutafanya vitu pamoja.

Basi nikaja kupata mwanaume wa Australia anayefanya kazi Geita kwenye migodi. Huyo mwanaume alikuwa mkubwa kidogo kwangu, zaidi ya miaka 20.

Nilivutiwa naye, lakini mara ya kwanza sikuona kama huyu mtu nitafika naye popote. Sikuwahi kumuomba chochote, lakini alidanganya kwamba familia yake ilifariki kwenye ajali. Basi nikawa interested na nikaanza kumzingatia zaidi kuliko zamani.

Akanambia ananipenda, hapo nikiwa na miaka 26, na mimi nikaona nimepata mwanaume, nikatulia naye kabisa.

Sikuwahi kwenda Australia. Tulikuwa tunakutana tu akipata muda hapa Tanzania, halafu yeye anarudi Australia.

Sikuwahi kumuuliza chochote. Nilijua kama mtu ananipenda, yeye ndiye atasema kitu.

Basi ilibidi nianze kwenda kwenye camp anakofanyia kazi. Ujinga uliniingia niachane na kazi, maana promises alizonipa ni kwamba tutaenda wote Australia akihamishwa kikazi.

Pia alikuwa ananihudumia zaidi ya pesa niliyokuwa naingiza kwa mwezi. Kingine, nilikuwa nadanganya sana kazini kwa sababu ya kwenda kuonana naye. Kila akiwa Tanzania tulikuwa tunaonana kama mara mbili kwa mwezi, hotelini na camp kwake.

Niliacha kazi, akaanza kuniudumia zaidi, kisha nikaenda Dar kwa sababu sote tulikuwa tunapenda kukutana Dar.

Basi ndugu zangu, siku zilivyozidi kwenda, mwanaume hafikirii kuja nyumbani kujitambulisha. Hatufanyi plans zozote za maisha. Nikimwambia ninunue kiwanja, anasema hawezi kununua huku.

Ila pesa ya kodi na matumizi alikuwa ananipa. Tatizo ni kwamba akili yangu ilikuwa imefungwa. Nilijua siku moja tutaenda Australia au nchi nyingine, hivyo nilikuwa naogopa kuanzisha kitu nitakachokuja kuuza baadaye.

Kwa hiyo nilikuwa nafikiria kazi ambayo nitatoa huduma tu, siyo kuuza vitu.

Kadri siku zilivyozidi kwenda, niligundua kwamba familia yake ipo hai. Akanambia ana watoto wawili wa kike na mama yao wametengana (separated). Pia anasema ana cancer na anasubiri apone ndipo waachane kabisa, halafu sisi tuje kuoana.

Akanipa pete ya promise ring, tukaendelea na mapenzi yetu.

Siku zilivyozidi kwenda, nikagundua kwamba anapendana na mwanaume mwenzake. Ila nilikaa kimya kwa sababu tayari tulikuwa kwenye mahusiano zaidi ya mwaka mmoja, nilishampenda na sikuwa na kazi, hivyo nilimtegemea.

Akaanza kutaka tufanye mapenzi kinyume na maumbile. Nilikuwa nakataa, lakini baadaye nikamwambia tukishazaa ndipo tutaanza kufanya hivyo, maana nilikuwa naogopa aibu nikiwa labour kwa sababu nilikuwa nimesikia story nyingi.

Basi akaendelea kunikumbusha sana. Nikaona nimridhishe mpenzi wangu kwa sababu niliamini tunapendana na sitakuwa na mwanaume mwingine zaidi yake. Hata kama alikuwa na shida zake, nilijua ananipenda. Nilijichanganya sana.

Mwaka 2024 ulikuwa mgumu sana kwangu. Dada yangu alifariki, mama yangu akafariki, na bibi yangu naye akafuata. Nafikiri mama yangu alipata mshtuko baada ya dada yangu kufariki, akaja kufariki miezi kama minne baadaye.

Nilikuwa na mawazo sana. Nilinenepa sana na nikaanza kunyonyoka sana nywele mpaka nikapata kipara karibu kichwa kizima. Nilinyoa kumuenzi mama yangu, na uzuri wangu nikahisi umepotea kabisa.

Pia nilikuwa najihisi mpweke zaidi kwa sababu mtu wangu akiwa Australia alikuwa ananiambia tu “good morning” na “usiku mwema”. Hakuwa anachati ndani ya siku kwa sababu anakuwa busy sana.

Nikajikuta nachat na baadhi ya wakaka ili tu niwe occupied. Siku moja alikuja, nikasahau kufuta message kwa sababu sikuwa naona kama ni jambo kubwa.

Kama kawaida yake, huwa anaangalia simu yangu. Huwa naiacha kwa sababu sina kitu cha ajabu. Lakini baada ya kuona zile message akaanza kubadilika, ingawa bado alikuwa ananiambia ananipenda.

Siku moja muda wake wa kuondoka Australia ulipokaribia, akanambia kwamba ataenda nyumbani moja kwa moja kwa sababu kuna msiba wa rafiki yake. Ila maelezo yake hayakuwa yanaeleweka na nilijua ananidanganya.

Baadaye akaniambia yupo anapanda ndege kuondoka, lakini alijichanganya na akanitumia picha ambazo aliwahi kunitumia zamani. Nikajua ananidanganya.

Nikampigia simu, akaniblock. Hakuni-unblock mpaka alipofika Australia.

Baadaye nikamuona amejicommentisha kwenye picha za msichana mwingine kwa comments za lover vibes. Wamefollowiana, nikamuuliza kama huyo ndiye demu wake. Akaniblock, na huyo msichana naye akaniblock papo hapo.

Basi nikakaa nikasubiri siku atakaporudi.

Madereva waliokuwa wanatujua waliinishangaa kwa sababu sikuwa naye tena. Mmoja akanipigia simu, nikajua tu yupo naye.

Basi huyo bwana akampa huyo mwanamke namba yangu anipigie. Akanipigia, baadaye akaniblock. Nilipompigia hakupokea, ila yule mwanaume akapokea.

Wakiwa pamoja, walikuwa wanacheka na kusema, “Huyu ni mbibi amechakaa. Huyo bwana haendani naye kabisa. Kachakaa, ni mrembo wa zamani. Sasa ni muda wetu sisi watoto wa 2000. Bwana tunae na tunatamba naye.”

Nikajiuliza walinitafuta kwa sababu gani, wakati sikuwa hata na muda wa kuwatafuta.

Basi huyo bwana naye akaniblock kabisa.

Nikapauka sana. Sina mtu wa kumkimbilia. Mama yangu keshadondoka kaburini. Nilijihisi nimechanganyikiwa na nikawaza mambo mengi. Niliumia sana kwa sababu ya aibu na kwa sababu ya watoto, hasa mmoja ambaye yupo English medium school.

Nikaona niyaachie yote kwa Mungu, lakini hasira zilinijaa.

Nilipomtafuta, akanambia kwamba aliniona nachat na wanaume na kwamba hanipendi. Hilo limenijaza hasira mpaka leo.

Naona kabisa anamfanyia huyo mwanamke vitu ambavyo hakuwahi kunifanyia mimi. Ni TikToker, wanakutana airport, wanapost picha, na sasa amembebesha mimba. Wanaendelea kucommentiana na wakati mwingine nashikwa na kichaa mpaka natamani kuwavurugia.

Sasa hivi naishi maisha ya umaskini na sina pa kukimbilia. Kama walivyosema, mimi sasa ni mbibi. Sijui nifanye nini na nianzie wapi.

Sikuwahi kutegemea maisha yangu yatakuwa hivi. Vitu nilivyokuwa naogopa zaidi maishani mwangu vimenitokea.

Ila namshukuru Mungu kwa sababu ndugu zangu wengine wamechukulia kwa uzito suala la kuwasomesha watoto.

Lakini sasa hivi nimekuwa mtu mwenye hasira sana. Najihisi nina roho mbaya na chuki kubwa.

Nilirudi kuishi kwenye nyumba ya mama yangu pamoja na watoto. Ninaishi na dada yangu mkubwa ambaye anaangalia nyumba. Hana kipato chochote, ila Mungu anasaidia tunaishi.

Kama kweli Mungu yupo, ndugu zangu, mniombee kwa sababu naona maisha yangu yanaporomoka na nahisi nitaendelea kuishi maisha ya umaskini.

Marafiki zangu wote siwasiliani nao kwa sababu ninaona aibu. Zamani tulikuwa wote tunapambana, lakini sasa mimi ni maskini asiye na mbele wala nyuma.

Ila bado nina hasira na hao watu. Sijui naachaje kuwachukia. Sitaki kuendelea kuhisi hivi, lakini nahisi haya maumivu yataendelea kuwa nami maisha yangu yote.

❤️
Amka uvae vizuri nenda katafute KAZI. Uwe busy sana utasahau. Usiogope kuanzia hata kwa mama ntilie ama saloon hizi za kiume.Njia ya Kazi nzuri itafunguka tu. Pia utapata mwanaume mwingine mzuri tu.
 
Kwa siku unalala masaaa mangapi? Unatkiwa unywe Azuma na amitriptiline angalau mwezi mmoja. Upate muda wa kulala mzuri baada ya kula vizuri!

Sasa unajishughulisha na nn
Asante sana kwa kunisaidia ukweli uwa silalai sana…. Zazngn nakesha usiku mzima.. nawaza tuu nakuja kupata ka uchingz kadogo mnoo saa11 umo na ynyw sio kwamba nimelala yenyw….nikama nimejipumzsha tuu ila nakua sijalala….sio tu kulala ata kula kwangu ni kama najilzmsha nawza kuvuka ata siku 3 sijala na nsisikie njaa…mwili huoni kama unanjaa kabsa ni kama pia ata mungu ananilazmsha kufunga bila kujua hehehe… yaan kula kwangu ni
Kwamba najilazmsha… ata nikila ata chips yai ynyw ninayonipenda sana inakua haina ladha mdomoni..na siumwi chochot zaidi ya moyo wangu….
Kwakweli kwa sasa nimerudi kwetu… sina kazi kwa sasa..nipo nymbn ila ndo natafta kazi saiv ndo swala nalo shugulikia saiv.
 
Utakaa sawa inshallah ila ulale sana, nenda hospitali mwmabie dokta akupe dozi ya amitriptiline na azuma unahitaj relaxation urudi kwenye state ya mwili wa kawaida. I hope itakusaidia kwa kiwango kikubwa san hiyo. Magum dunian hayaishi! Mm nilikumbana na ngum sana miaka tofaut tofauti.

Kubwa hasa mpasuko ndani ya familia ambao mpaka kesho bado upo na hauna majibu. Weka Cv yako hapa bila mawasiliano yako mtu akiwa na nafas akucheki. Mana jf watu wema wapo na mbuzimbuzi- Kima wapo kibao tu. Dipshits!
 
Sikudanganyi ndugu yangu..mm sjioni kabsa nikiwa mama ntilie na iyo kazi siiwezi heheh au saloon..usidhani si tambui ilo natambua ibd ata niende nifagie bara bara nipate miambili…naitaji kujianda kiakili sasa kua saivi naweza kuanza life ambalo nilikua silifikilii kabsa…kwanza kitendo cha mm kutokua na wazazi kumenkmbsha kua inabd nianze kua mgumu nifanye chochote maana ndo kuna tupesa kdg…ila sasa uthubutu ndo sina yaan kuna mda natenganga mda nasema sasa leo tenga masaa mawili yakuaa kuset akili kwamba ntaenda niuze viazi sehemu,nikae kama wamama niamke asbui mapema nikachukue viazi ntapata izo laki 1 na kitu kwa mwezi…..nijiandae kiakili kwamba rfk zangu na ndugu zangu wataniona nitengeneza njia za kukubaliana na iyo aibu aisee
Amka uvae vizuri nenda katafute KAZI. Uwe busy sana utasahau. Usiogope kuanzia hata kwa mama ntilie ama saloon hizi za kiume.Njia ya Kazi nzuri itafunguka tu. Pia utapata mwanaume mwingine mzuri tu.
fan
Utakaa sawa inshallah ila ulale sana, nenda hospitali mwmabie dokta akupe dozi ya amitriptiline na azuma unahitaj relaxation urudi kwenye state ya mwili wa kawaida. I hope itakusaidia kwa kiwango kikubwa san hiyo. Magum dunian hayaishi! Mm nilikumbana na ngum sana miaka tofaut tofauti.

Kubwa hasa mpasuko ndani ya familia ambao mpaka kesho bado upo na hauna majibu. Weka Cv yako hapa bila mawasiliano yako mtu akiwa na nafas akucheki. Mana jf watu wema wapo na mbuzimbuzi- Kima wapo kibao tu. Dipshits
Asante sana mkuu…poleni na matatzo kifamilia…tftn mtu awasuluishe matatzo yenu
 
Sikudanganyi ndugu yangu..mm sjioni kabsa nikiwa mama ntilie na iyo kazi siiwezi heheh au saloon..usidhani si tambui ilo natambua ibd ata niende nifagie bara bara nipate miambili…naitaji kujianda kiakili sasa kua saivi naweza kuanza life ambalo nilikua silifikilii kabsa…kwanza kitendo cha mm kutokua na wazazi kumenkmbsha kua inabd nianze kua mgumu nifanye chochote maana ndo kuna tupesa kdg…ila sasa uthubutu ndo sina yaan kuna mda natenganga mda nasema sasa leo tenga masaa mawili yakuaa kuset akili kwamba ntaenda niuze viazi sehemu,nikae kama wamama niamke asbui mapema nikachukue viazi ntapata izo laki 1 na kitu kwa mwezi…..nijiandae kiakili kwamba rfk zangu na ndugu zangu wataniona nitengeneza njia za kukubaliana na iyo aibu aisee

fan

Asante sana mkuu…poleni na matatzo kifamilia…tftn mtu awasuluishe matatzo yenu
We did it! No hard feeling at all. Kila mtu maisha yake yanaenda bila mwingine. So let keep rise and shine
 
Back
Top Bottom