Top Gun
JF-Expert Member
- Dec 11, 2024
- 240
- 785
Kama mtu anaweza kupata nafasi hadimu ya kutoa maoni ila jambo analo sema ni hilo, na yuko serious kabisa.
===
Kero ya ghorofa la jirani imeibua mjadala na vicheko katika mkutano wa hadhara wilayani Monduli, baada ya mwananchi mmoja kudai ujenzi huo unavuruga faragha ya familia yake.
Mwananchi huyo wa Kijiji cha Losirwa, Kata ya Esilalei, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, aliyefahamika kwa jina la Laizer, aliwasilisha malalamiko yake mbele ya Mbunge wa Jimbo la Monduli, Isack Joseph, akieleza kuwa jirani yake alianza kujenga nyumba ya kawaida lakini baadaye akaendelea kuongeza ujenzi hadi kuwa ghorofa.