Umasikini Mbaya, Unaogopesha, Unatisha

Umasikini Mbaya, Unaogopesha, Unatisha

Umasikini ni Mkubwa KWA sababu mifumo yetu haisapoti watu kujikwamua tofauti na mifumo ya ulaya kule umasikini unataka mwenyewe.
Unafanywa muwe wengi masikini Ili iwe rahisi kuwatawala
 
Umenikumbusha title ya kitabu nnachokipenda sana Cha Zig Ziglar ( See you at the top)

Biashara zimeanza kukaa sawa mkuu? Naamini nikipindi Cha mpindo na ni darasa unapitia lakini mambo yataimarika tena
Amen.
Nilichojifunza mambo hupanda na kushuka.
Leo nauza sanaa, kesho nauza wastani na kesho kutwa nauzi kidogo sanaaa.

Ila NEVER GIVE UP.

#YNWW
 
Kama upo kwenye nafasi ya kumvuta Mtanzania mmoja au zaidi, awe ndugu, jamaa, rafiki au mtu baki kumtoa kwenye umaskini, pease do it, huo ndio mchango wako wa Taifa lako.

Umaskini mbaya, unaogopesha, unatisha.

Njia nzuri zaidi ya kukuhakikishia mafanikio, ni kwa kufanya kwa kadri ya uwezo wako kuwanyanyua wanaokuzunguka!
Inabidi utengenezewe sanamu lako pale mwenge
 
Kuna mstaafu kasomesha wanae kwa uchungu sanaa wote wanne wa lipata degree tofauti tofauti vyuo vikuu. Ila chakushangaza wote wameokoka wanashuda kanisani kunene neno la mungu mchana na usiku hawataki kutafuta ajira, tena sio kwamba ni viongozi wa kanisa ni wa fuasi wa kawaida wanao toa Sadaqa.....hiyo ni laana.
Duniani tunapita wao wamewekeza kwenye maisha yajayo.
Ndio maisha waliyochagua je wanakusumbua kwa chochote iwe chakula au mavazi nk?
 
Umasikini ni Mkubwa KWA sababu mifumo yetu haisapoti watu kujikwamua tofauti na mifumo ya ulaya kule umasikini unataka mwenyewe.
Unafanywa muwe wengi masikini Ili iwe rahisi kuwatawala
Tutasingizia mifumo ila hapana mfano

Elimu kwa sasa ni bure ila mzazi hajishughulishi kabisa kufuatilia maendeleo ya mtoto, hanunui vitabu wala madaftari.
Mtoto anafika la 7 hajui kusoma wala kuandika, hapo ulitaka mfumo gani?

Mzazi anaamua kuzaa zaa hovyo bila mpangilio hapo wategemea nini kama sio kuendeleza umasikini?
 
Nani kakwambia kufanikiwa kimaisha kunategemea mfumo wa elimu.
Hio elimu bure ni kisiasa tu na sio hali halisi, Hakuna elimu bure.
Mifumo inapokuwa imewekwa yenyewe ndio ukuongoza kutimiza ndoto zako.
Mfano unalima Kazi ya serikali ni kununua mkulima hatakiwi kutafuta soko sio Kazi yake yeye ni kulima tu, serikali inanunua inaweka gharani wanunuzi wananunua wanamuuzia tena mkulima wakati wa njaa.
 
Siku mkiacha wizi na ushirikina mkaamini kuwa unaweza kupata bila kuiba wala kupitia njia ya kuroga basi utafanikiwa

Ukiifanya hela rafiki yako pia utatoka
Jifunze kuweka akiba sana na uwe na malengo, kama ni mfanyakazi weka malengo ya miaka 10 tu kazini ukiwa na hela zako ulizokuwa unazithamini na kuzipenda utatoboa

Ila kama wewe una uadui na hela yaani ukipokea tu hutaki kuziona basi utakufa masikini na hela zitakulaani

Nimejifunza haya kutoka kwa wazazi na leo namshukuru Mungu niko na ukaribu sana na kitu kinaitwa hela na ndio rafiki yangu mkubwa

Vijana hatukuja kufanya Anasa duniani

Wengine wanakataa ndoa kisa wanaogopa kulea watoto na mama yao huo ni uzembe wa kutokujituma
 
Kuna jama alitafuta kazi kwa siku nyingi ni kamfanyia mpango akapata kibarua cha ulinzi shule ya wasichana mshahara wake ukawa 350k kwa mwezi, akapiga kazi kwa wiki tatu, wiki ya nne mkurugezi akamuagiza aende akanunue kopo la ragi moja kupaka getini akampa 28,000. Jama akakimbia mazima na pesa sh 28000, wakati mshahara wake ulikua umebakiza siku saba tu alipwe, kama sio laana ni nini hiyo?
Ukweli upo wa hiyo story
 
Mtu hupata laana baada ya kuzaliwa wengine wamebeba laana za ukoo wao, kwahiyo uwe mwangalifu na watu huwezi kupambana na mtu mwenye laana.
Hakuna mambo ya kurithishana au kubeba vitu vinavyoitwa laana sijui za mababu ukoo nk.

Ni kila mtu anawajibika na atawajibika kwa matendo yake yeye mwenyewe
 
Kuna jama alitafuta kazi kwa siku nyingi ni kamfanyia mpango akapata kibarua cha ulinzi shule ya wasichana mshahara wake ukawa 350k kwa mwezi, akapiga kazi kwa wiki tatu, wiki ya nne mkurugezi akamuagiza aende akanunue kopo la ragi moja kupaka getini akampa 28,000. Jama akakimbia mazima na pesa sh 28000, wakati mshahara wake ulikua umebakiza siku saba tu alipwe, kama sio laana ni nini hiyo?
Hiyo sio laana ni UJINGA na TAMAA za huyo muhusika
 
Ni mbaya zaidi ya ubaya wenyewe!....naomba wanajamvi mnitoe kwenye mkwamo huu wa umasikini,tafadhali sana
 
umeongea jamaa la maana sana ndg yangu.
nakumbuka siku za nyuma kuna mtawala mmoja aliwahi kuwaaminisha baadhi ya watz kwamba maisha ya umaskini ni utakatifu na maisha yenye nafuu nje umaskini ni laana.

kwa bahati mbaya alipata wafuasi wengi walioamini hiyo nadharia yake. ilikuwa ni sumu ya hatari, ilifika wakati baadhi ya "maskini wenzangu" walianza kujenga chuki na watu wenye kipato ktk jamii.

bahati nzuri sana Mungu akaingilia kati, akamuondoa. sijui hali ingekuaje kama angeendelea kuwepo mpaka leo.
Mtaje tu unamwogopa??😁😁
 
Umasikini ni Mkubwa KWA sababu mifumo yetu haisapoti watu kujikwamua tofauti na mifumo ya ulaya kule umasikini unataka mwenyewe.
Unafanywa muwe wengi masikini Ili iwe rahisi kuwatawala
Kabisa mkuu.ukichek mfumo auruhusu mtu kukuwa aisee.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom