Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,789
Kikiwa ndio kitovu kikubwa cha biashara nyingi za nchi kwa mizigo inayotoka nje hasa China.. Kuna wababe na mafioso ndio wamezikamata biashara za huo mji na wengine wote ni wapagazi na wajakazi kulingana na makundi yao lakini mwisho wa siku kila mtu anapata kulingana na urefu wa kamba yake!
Hawa ma godfather ndio wamiliki wa mabohari makubwa na utitiri wa mafremu.. .. Wakiuza jumla na rejareja kupitia mtandao wa wachuuzi wao waliotapakaa kwenye fremu, barabara na kila aina ya upenyo..hawa wao kuingiza miliom mia moja kwa siku ni jambo la kawaida
Hawa mabwanyenye wenye hela wao hawangaiki juani bali ni wapanga mipango na wachora racket.. Wanachoangalia wao kupitia mawakala wao ni biashara gani imeshika soko na mwanzilishi ni nani...na ana bei gani.
Ni kipindi ukiwa umeshaitangaza biashara yako mpya sokoni na kujaza wateja.. Mafioso hao huwatuma vijana mawakala wao na kukununuza baaadhi ya bidhaa zako... Hizo hurushwa China na kutafuta chimbo lake...
Wewe huku bila habari umeshapelelezwa mzigo wako unaisha na kuwahi China kuchukua mzigo mkubwa zaidi... Pengine container moja au mbili.. Wakati unatua China wenzako washafungasha container kumi za mzigo kama wako.. Na kwa wachina jinsi unavyochukua mzigo mkubwa ndivyo bei inavyopungua
Ukija kurudi bongo na mzigo wako wa container 2 unakuta sokoni bidhaa imetapakaa tena kwa bei ya chini zaidi kuliko yako!
Hapo utafanyaje?
Huna jinsi bali kupunguza bei ama kuwauzia mafioso hao mzigo wako wote...!! Kuna umafia mwingi sana Kariakoo usijaribu kujifanya mjanja kama huna nguvu za kutosha...! Biashara nyingi ni mali kauli na kuaminiana.. Ole wako ulete usela pori uchukue mzigo halafu usirejeshe pesa.. Wanakufuturu kimya kimya...
Biashara nyingi za Kariakoo ni kukopana pesa na kurejesha kwa siku, wiki na mwezi.. Ole wako uingie mitini usirejeshe.. Kesi zao hawapeleki mahakamani wanamaliza wenyewe kwa namna ya kuogofya na kutisha sana lakini kimya kimya
Kariakoo mtaondoka wote kwenda China kufunga mzigo lakini mkifika huko kila mtu anaingia chimbo lake.. Hakuna kuaminiana
Kwa upande wa nguvu za giza ndio usiseme kuna makafara ya kutosha kuliko sehemu nyingine yoyote nchini...kuna misukule ya kutosha kuliko sehemu nyingine yoyote Tanzania Kuna milango ya kuzimu
Kuna uchawi wa kutosha.. Kila mtu anakinga yake! Kila mtu anatafuta mvuto... Vita ya kiroho Kariakoo huwezi kuipata popote nchini
Kuna viumbe na wanyama wa kutisha lakini wote wako kwenye maumbo ya kibinadamu
Kuna vyumba vya mateso, kuna jela za siri, kuna utumwa wa kuanzia, kwenye biashara, nyumbani na sehemu za starehe.. Kuna watumwa wa ngono Kariakoo.. Ombaomba na watoto wa mitaani si wote ni halisi . .. Ni biashara za watu zile.. Tena zenye kipato kizuri tuu...
Soko kuu la Kariakoo limeungua(zwa) limeteketeza vingi lakini si vyote.. Vilinge bado viko hai na ule mlango wa kuzimu kule shimoni bado uko wazi... Ukitaka kupajua Kariakoo vizuri ingia pale shimoni usiku