umenena vyema kuwa wewe ni mtanzania ambaye umelowea goma. Inaonekana huna habari na amri ya jwtz kuwa sisi wananchi haturuhusiwi kuongelea masuala ya vita ya huko congo mpaka kwa kibali chao. Angalia usije ukaingia matatizoni na jeshi letu kwa kuongelea vita ambayo tayari kuna katazo la chombo chetu cha ulinzi na usalama.
Nadhani ndio maana kagame ameanza visa na Tanzania....tutamtandika kama mwizi, hatujui huyu
mkuu Nkunda ninani na yuko wapi kwa sasa?
anauhusiano na m23?
Mkuu FLASH HIDER asante sana kiasi fulani umeongeza mambo mengi ambayo nilikuwa siyajui.
Mm kaka napenda kuuliza maswali machache...wasaidizi wa karibu wa rais kabila ni watu wenye uwezo kiasi gani? Wa kumshauri na pia suala la kwamba rais kabila sio mkongo je linainfluence chochote kwenye governance ya raisi kabila
Hivyi ninvyoandika ninaangalia TV hapa, miji yote ambayo ilikuwa imekaliwa na M23 imekwishachukuliwa na FARDC. Kanzia Kiwanja, Rumangabo, Katale, Kibati (ulichukuliwa siku nyingi) yote ipo chini ya FARDC. Wamebakiza mji wa BUNAGANA ambapo ni mpakani kabisa na Uganda. Bila shaka kufikia Kesho mtasikia M23 imekwisha. Tuombe yasitokee tena mauaji kwa JWTZ maana naambiwa wanafanya kweli huko front.
ok, ngoja niwape hili ingawa kwa ufupi
Mgogoro katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Democratic Republic of Congo "DRC") una historia ndefu. Tokea nchi hiyo ipate uhuru wake kutoka kwa Ubeligiji hapo tarehe 30 Juni 1960, haijawahi kushuhudia hali ya kiusalama ya muda mrefu. Migogoro isiyopata ufumbuzi w kudumu ilianza mara tu baada ya uchanguzi wa kwanza nchini humo uliomweka Patrice Lumumba kuwa Waziri Mkuu na Joseph Kazavubu kuwa Rais. Kutokana na matatizo mbalimbali ya kimtazamo baina ya Rais na Waziri Mkuu, Serikali hiyo mpya ilijikuta ikipinduliwa na Kanali Jopeph Mobutu hapo tarehe 14 Septemba 1960 ambapo wiki chache baadaye, Kanali Joseph Mobutu alimuua Patrice Lumbumba. Mara baada ya mapinduzi na kifo cha Lumumba, nchi hiyo ilishuhudia machafuko kwa vipindi mbalimbali kuanzia mwaka 1960-1964 ambapo mara zote majeshi ya Serikali yakisaidiwa na yale ya Marekani pamoja na askari wa kukodiwa kutoka Ulaya yalikuwa wakidhibiti machafuko hayo. Mwaka 1965, Mobutu ambaye alijipandisha cheo na kuwa Luteni Jenerali, alijitangaza kuwa ni rais rasmi. Tokea mwaka 1965-1977 nchi hiyo ilishuhudia hali ya utulivu kiasi ingawa ilikuwa inaendeshwa kimabavu katika utawala wa kidikteta chini ya Rais Mobutu. Mwishoni mwa mwaka 1990, Serikali ya rais Mobutu iliandamwa na upinzani mkubwa kutoka ndani na nje ya nchi ikilalamikiwa kwa kutofuata haki za binadamu, rushwa, matumizi mabaya ya mali za serikali nk. Mwaka 1991 hali ya kiuchumi nchini Zaire ilizidi kuwa mbaya ambapo ilifikia wakati wanajeshi waligoma kutokana na kutolipwa mishahara.....
Mimi siyo mwandishi wa habari lakini bila shaka mmenipata ninachotaka kusema.
ninafanya hivi kwa nia njema na nadhani sijaharibu hali ya hewa
Karibu sana, hivi ninavyoandika hapa, Helikopta za FARDC zinapita hapa GOMA kuelekea eneo la mapigano, bila shaka M23 wanaadabishwa.
Karibu sana, hivi ninavyoandika hapa, Helikopta za FARDC zinapita hapa GOMA kuelekea eneo la mapigano, bila shaka M23 wanaadabishwa.
Karibu sana, hivi ninavyoandika hapa, Helikopta za FARDC zinapita hapa GOMA kuelekea eneo la mapigano, bila shaka M23 wanaadabishwa.
Kuna fununu kuwa wakati wa nyuma majeshi ya U.N yalituhumiwa kufanya biashara ya silaha na madini kwa waasi hasa Nkunda.Pia kuna fununu kuwa Nkunda alikuwa supported na belgium through Rwanda.Ni kweli mambo hayo yalikuwepo?ni nini kimeleta tofauti ya utendaji kati ya majeshi ya UN yaliyopita na haya ya sasa yaliyosheheni wabongo?
Du!JWTZ na majeshi mengine ya SA na Malawi yote yapo front. Tofauti ni kuwa JWTZ ndiyo lead army kwa kutoa kamanda wa majeshi ya FIB na viongozi. Hawajatulia kaka. Habari zilizopo ni kuwa Miji iliyokaliwa kiukamilfu mpaka sasa ni Kiwanja, Rumangabo, Kitale, Kibumba, Kibati, Munigi, Rwaza na Kalengele.
Flash hider hivi rwanda kuwasaidia m23 wanasaidiwa na nani? Na ni kwa nini congo toka miaka hiyo ya 1960
mpaka leo wanashindwa kuituliza nchi yao?
Du!
JWTZ noma sana!
Najua hawapo mitaani ,lakini ukiwaona waambie sisi huku tunawapa kidole gumba- big up!
Lakini yote ni lile zoezi la karibia miaka 50 ua ukombozi wa Afrika?
Kaka asante sana. Naiona nia njema yako kujujuza kinachoendelea huko Congo DRC. Binafsi nimejua mengine kiasi zaidi ya mwanzo.
Ila bado nina mashaka na amani ya kuduma Congo DRC, Kuanzia wananchi wa Congo DRC na hata serikali kuna haja ya kubadilisha mambo mengi sana.
Niliona baadhi ya clip za video zikionesha wanajeshi wa Congo DRC walevi, na matendo yao kipindi cha mapigano yanaonesha ni moja ya jeshi lisilokuwa na nidhamu kabisa.
Kama JWTZ wakiwasaidia WaCongoman kuwaondoa M23 bado tatizo litakuwepo kama hatutawasaidia kujenga jeshi lao. Tulifanya Uganda baada ya kumtoa Amin Dada, nadhani inahaja na Congo kusaidiwa.
Asante sana FLASH HIDER.
nilifikiri ni mamluki wa nduli kagame, pole sana kwa lugha kali niliyoitumia!