Uliza lolote kuhusu mgogoro ndani ya DRC hasa mapigano kati ya M23 na FARDC

Huyo afisa aliyefairki ni mwingine tofauti na yule wa miezi iliyopita? au ndiyo yule yule? tunaambiwa kuwa jeshi letu linalinda amani tu haliko front kuna ukweli?

Nasikia amani ya kweli haiwezi kupatakana bila paul Kgame kutolewa madarakani, na hii vita itaishia ilikoanzia yaana Rwanda. tunataka kumtia adabu huyu rais mwenye damu za watu na anayetishia kumuaa rais wetu,
tunafikir vita hii mwisho wake ni kigari unasemaje?
Tunashukuru kwa taarifa kwa sababu baba na kaka zetu wapo huko, inshallah MUNGU atawasaidia.
 
Katika makosa ambayo yatafanywa na Tanzania ni pamoja na kujaribu au kuondoa majeshi DRC. Hapa sisi watanzania tunaishi hapa GOMA imekuwa ni shangwe na ndelemo kutokana na mafanikio ya JWTZ. Sijui huko nyumbani mtachukuiaje lakini ukweli tupo juu. Hwa jamaa zetu wa Rwanda tupo nao wengi sana hapa nao hawaamini yanayoendelea chini ya JWTZ.

Naomba kujua hivi JWTZ imeingia vitani kuwasaidia FARDC au wao wametulia tu kama walinzi wa amani? Je ni miji gani amabyo inakaliwa kwa ukamilifu mpaka sasa na M23?
 
Kwanini Zimbabwe, Angola na Namibia walishindwa kuwazima hawa Banyamulenge?
Wacongo wanasemaje kuhusu nchi nyingtine za Africa ambazo zimewahi kuwasaidia ?

Zimbabwe, Angola na Namibia walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani kama isingekuwa wao, huenda leo hii Kabila asingekuwa Rais. Ni wao ndiyo walioyazuia majeshi ya hao jamaa zetu katika eneo la Kisangani wakijiandaa kuichukua Kinshasa. Walifanya kazi kubwa ambayo ndiyo iliyosababisha UN ikaanzisha mazungumzo ya kumaliza mgogoro. Kuna kiti kinaitwa KONGO KUU YA DRC.

Walipenda sana badala ya Malawi ingekuja ZIMBABWE na Angola kwani waliwasaidia sana kama nilivyoeleza.
 
Huyo afisa aliyefairki ni mwingine tofauti na yule wa miezi iliyopita? au ndiyo yule yule? tunaambiwa kuwa jeshi letu linalinda amani tu haliko front kuna ukweli?

Nasikia amani ya kweli haiwezi kupatakana bila paul Kgame kutolewa madarakani, na hii vita itaishia ilikoanzia yaana Rwanda. tunataka kumtia adabu huyu rais mwenye damu za watu na anayetishia kumuaa rais wetu,
tunafikir vita hii mwisho wake ni kigari unasemaje?
Tunashukuru kwa taarifa kwa sababu baba na kaka zetu wapo huko, inshallah MUNGU atawasaidia.

Ndugu yangu Mshino,

Huyu ni tofauti na yule wa awali (Agosti). Ukweli bila kuficha majeshi yetu JWTZ yapo front ndiyo maana vinatokea vifo.

Maelezo kuwa ni mpaka Kagame aondoke ndipo Mgogoro uishe huenda yana ukweli. Maana Rwanda wamekuwa wakiwasaidia sana hwa M23. Nadhani ni UN kummbana vilvivyo kama ilivyo sasa ambapo USA na UK wamesitisha baadi ya misaada. Jingine ni reform ya nchi ya DRC
 
Naomba kujua hivi JWTZ imeingia vitani kuwasaidia FARDC au wao wametulia tu kama walinzi wa amani? Je ni miji gani amabyo inakaliwa kwa ukamilifu mpaka sasa na M23?

JWTZ na majeshi mengine ya SA na Malawi yote yapo front. Tofauti ni kuwa JWTZ ndiyo lead army kwa kutoa kamanda wa majeshi ya FIB na viongozi. Hawajatulia kaka. Habari zilizopo ni kuwa Miji iliyokaliwa kiukamilfu mpaka sasa ni Kiwanja, Rumangabo, Kitale, Kibumba, Kibati, Munigi, Rwaza na Kalengele.
 
Zimbabwe, Angola na Namibia walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani kama isingekuwa wao, huenda leo hii Kabila asingekuwa Rais. Ni wao ndiyo walioyazuia majeshi ya hao jamaa zetu katika eneo la Kisangani wakijiandaa kuichukua Kinshasa. Walifanya kazi kubwa ambayo ndiyo iliyosababisha UN ikaanzisha mazungumzo ya kumaliza mgogoro. Kuna kiti kinaitwa KONGO KUU YA DRC.

Walipenda sana badala ya Malawi ingekuja ZIMBABWE na Angola kwani waliwasaidia sana kama nilivyoeleza.
Sawasawa, kwanini hawakuweza kuwa-push back miaka hiyo?
Ndiyo maana wengi wetu tulikuwa tunaona kuwa Rwanda ni nchi ndogo kulinganiusha na hizo, ila inawapa headache. Sasa kwanini walishindwa kuwasukuma mipakani wakati ule?
 
Ndugu zanguni hasa Watanzania,

Mimi ni mtanzania ninafanya biashara zangu huku DRC Goma kwa muda mrefu. Ninaishi hapa GOMA na nimekuwa nikisafiri kwenda sehemu mbalimbali ndani ya DRC.

Nimekuwa nikifuatilia mijadala kuhusu mgogoro wa M23 na serikali ya DRC, nimegundua watu wengi hawapo informed on what is going on.

Sasa kwa wale wenye swali au chochote wanachotaka kujua kuhusu mgogoro huu, mapigano yanayoendelea, na ushiriki na mapokeo ya WaKongo kuhusu JWTZ, mnaweza kuniuliza.

Nipo hapa kwa karibu miaka kumi na mbili sasa, bila sahaka nina kitu kipya ambacho huenda ninaweza kuwahabarisha.

Nafikiri ingekuwa vyema kama ungeanza kwa kutueleza japo kwa kifupi unachokijua kuhusu mgogoro huo, ili kama kuna maswali basi yaanzie hapo.
 
Umenena vyema kuwa wewe ni mtanzania ambaye umelowea Goma. Inaonekana huna habari na amri ya JWTZ kuwa sisi wananchi haturuhusiwi kuongelea masuala ya vita ya huko Congo mpaka kwa kibali chao. Angalia usije ukaingia matatizoni na jeshi letu kwa kuongelea vita ambayo tayari kuna katazo la chombo chetu cha ulinzi na usalama.

acha kutisha watu ilo jeshi lilisema kutupa taharifa kila wik 2 mbona wameshindwa aja wazalendo watujuze
 
Huyo afisa aliyefairki ni mwingine tofauti na yule wa miezi iliyopita? au ndiyo yule yule? tunaambiwa kuwa jeshi letu linalinda amani tu haliko front kuna ukweli?

Nasikia amani ya kweli haiwezi kupatakana bila paul Kgame kutolewa madarakani, na hii vita itaishia ilikoanzia yaana Rwanda. tunataka kumtia adabu huyu rais mwenye damu za watu na anayetishia kumuaa rais wetu,
tunafikir vita hii mwisho wake ni kigari unasemaje?
Tunashukuru kwa taarifa kwa sababu baba na kaka zetu wapo huko, inshallah MUNGU atawasaidia.

Mkuu, JWTZ ndo wapo front na wanatoa kipigo vibaya mno. FARDC walishashindwa na M23 Siku nyingi, tangu JWTZ kutua Goma ndo tunawasikia na hao FARDC.
 
tuambie kiini cha mgogoro ni nini, na kama unasema mgogoro unakaribia miaka 14 tuambie interest ni nini na kama hiyo interest inapersist kwa marais wote, na kama sio kwa nini vita isikome so long rais mwanzilishi au aliyehusika kwanza hayupo? na kama marais hawahusiki, basi wameshindwa mbinu ya kunyamazisha hiyo migogoro?

Nimejaribu kuelezea historia ya mgogoro wa DRC kama ninavyoijua amabayo imetaja chanzo cha mgogoro na juhudi za kulaiza mgogoro huo. Hapa niweka tena kaka.

Mgogoro katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Democratic Republic of Congo "DRC") una historia ndefu. Tokea nchi hiyo ipate uhuru wake kutoka kwa Ubeligiji hapo tarehe 30 Juni 1960, haijawahi kushuhudia hali ya kiusalama ya muda mrefu. Migogoro isiyopata ufumbuzi w kudumu ilianza mara tu baada ya uchanguzi wa kwanza nchini humo uliomweka Patrice Lumumba kuwa Waziri Mkuu na Joseph Kazavubu kuwa Rais. Kutokana na matatizo mbalimbali ya kimtazamo baina ya Rais na Waziri Mkuu, Serikali hiyo mpya ilijikuta ikipinduliwa na Kanali Jopeph Mobutu hapo tarehe 14 Septemba 1960 ambapo wiki chache baadaye, Kanali Joseph Mobutu alimuua Patrice Lumbumba. Mara baada ya mapinduzi na kifo cha Lumumba, nchi hiyo ilishuhudia machafuko kwa vipindi mbalimbali kuanzia mwaka 1960-1964 ambapo mara zote majeshi ya Serikali yakisaidiwa na yale ya Marekani pamoja na askari wa kukodiwa kutoka Ulaya yalikuwa wakidhibiti machafuko hayo.

Mwaka 1965, Mobutu ambaye alijipandisha cheo na kuwa Luteni Jenerali, alijitangaza kuwa ni rais rasmi. Tokea mwaka 1965-1977 nchi hiyo ilishuhudia hali ya utulivu kiasi ingawa ilikuwa inaendeshwa kimabavu katika utawala wa kidikteta chini ya Rais Mobutu. Mwishoni mwa mwaka 1990, Serikali ya rais Mobutu iliandamwa na upinzani mkubwa kutoka ndani na nje ya nchi ikilalamikiwa kwa kutofuata haki za binadamu, rushwa, matumizi mabaya ya mali za serikali nk. Mwaka 1991 hali ya kiuchumi nchini Zaire ilizidi kuwa mbaya ambapo ilifikia wakati wanajeshi waligoma kutokana na kutolipwa mishahara.

Mara baada ya mauaji ya Kimbari nchini Rwanda hapo mwaka 1994, nchi ya Zaire ilijikuta ipo katika mgogoro ambapo wahutu wengi waliokimbia Rwanda na kuingia Zaire walikuwa wanatumia makambi ya wakimbizi kujipanga na kufanya mashambulizi nchini Rwanda. Serikali ya Mobutu haikuwa inachukua hatua zozote kukabiliana na hali hiyo. Kitendo hicho kilileta uhasama baina ya Serikali ya rais Mobutu na ile ya Rwanda na Uganda. Kufuatia hali hiyo, Rwanda na Uganda zilikisaidia kikundi kilichojulikana kama "Alliance des Forces Démocratiques pour la Libération du Congo-Zaire (AFDL) chini ya Laurent-Desire Kabila kuishambulia Zaire. Kikundi hicho kilianza kufanya mashambulizi na kuchukua miji mbalimbali ndani ya Zaire ambapo tarehe 20 May 1997, Rais Mobutu alikimbia nchi na bwana Laurent Desire Kabila akajitangaza kuwa rais na kubadirisha jina la nchi hiyo na kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mapigano haya ya kumuondoa Rais Mobutu madarakani hujulikana kama Vita kuu ya kwanza ya Kongo.

Mwaka mmoja baada ya kushika madaraka, rais Kabila alitangaza kuwaondoa washauri wake wote wa kijeshi kutoka nchi jirani zilizomsaidia kumuondoa rais Mobutu hasa Rwanda. Ikumbukwe kuwa wakati huo, Rais Laurent Kabila alikuwa na washauri wengi wa kijeshi kutoka Rwanda akiwemo Waziri wa Ulinzi wa Rwanda wa sasa Bwana James Kabarebe aliyekuwa Mkuu wa Majeshi wa Jeshi la Zaire mpya. Kitendo hicho cha kuwaondosha washauri hao kilifuatiwa na machafuko nchini humo ambapo watu wenye asili ya jamii ya Kitusi walianza kulengwa katika mashambulizi hayo. Hali hiyo ilizifanya nchi za Rwanda, Burundi na Uganda kuishambulia Kongo kwa kile kinachoelezwa kama kuwalinda watu wa jamii ya Kitusi. Nchi za Zimbabwe, Namibia na Angola zilipigana kuisaidia Kongo baada ya kuombwa kupitia Umoja wa Kimaendeleo wa nchi za Kusini mwa Afika (Southern African Development Community). Nchi za Chad na Sudan nazo ziliingia vitani kuisaidia DRC baada ya kuombwa na Rais Kabila. Rais Kabila aliuawa tarehe 18 Januari, 2001 na mmoja wa walinzi wake aliyejulikana kama Rashidi Muzele, kwa namna isiyoeleweka vizuri hadi leo. Vita hiyo inayojulikana kama vita kuu ya pili ya Kongo au Vita Kubwa ya Afrika ilimalizika mwaka 2003 ambapo inakadiriwa kuwa jumla ya watu…..walipoteza maisha .

Baada ya kifo cha Rais Laurent Kabila, tarehe 26 Januari, 2001, Joseph Kabila (mtoto wa Laurent-Desire Kabila) aliteuliwa na baadae kuchaguliwa kuwa rais wa DRC. Serikali ya Rais Joseph Kabila nayo ikajikuta inakumbwa na changamoto kubwa za migogoro. Tarehe 30 Desemba, 2006, liliundwa kundi la "The National Congress for the Defence of the People (kwa kifaransa Congrès national pour la défense du peuple, CNDP)chini ya Bwana Laurent Nkunda. Madhumuni ya kundi hilo yalidaiwa ni kulinda haki za Watu wa jamii ya Kitusi waliopo DRC. Januari, 2009, kundi hilo la CNDP liligawanyika ambapo tarehe 22 Januari mwaka huo huo, Nkunda alikamatwa na kuwekwa kizuizini nchini Rwanda ambapo yupo huko mpaka sasa. Tarehe 23 Machi, 2009, kundi lililobaki likiongozwa na Bosco Ntaganda lilisaini makubaliano na Serikali na lilijiunga katika Jeshi la Serikali. Makubaliano hayo yalidumu kwa kipindi cha miaka mitatu tu ambapo mwaka 2012, wanajeshi, wengi wao wakiwa ni wale waliokuwa wa NDP walijiondoa katika Jeshi la Serikali na kuunda kundi la M23 wakilalamikia kutotekelezwa kwa baadhi ya makubaliano yaliyosainiwa mwaka 2009. Kundi hilo la M23 lilikalia eneo la Rutchuru ambalo linapakana na Rwanda na Uganda.

Kiongozi wa kundi hilo alikuwa ni Bosco Ntaganda akisaidiwa na Sultani Makenga. Mwezi Mei, 2013 kulitokea mapigano kati ya makundi mawili ndani ya M23, lile linalomuunga mkono Bosco Ntaganda na lile linalomuunga mkono Sultani Makenga. Kundi lililokuwa linamuunga mkono Bosco Ntaganda lilizidiwa na kuamua kuvuka mpaka na kuingia Rwanda na Ntaganda akaamua kujisalimisha katika Ubalozi wa Marekani nchini Rwanda. Kwa sasa wapiganaji hao wanaokariwa kuwa 682 wapo katika kambi maalum ya wakimbizi nchini Rwanda na Bosco Ntaganda yupo chini ya Mahakama ya Dunia ya Makosa ya Jinai(ICC) akishitakiwa kwa kwenda kinyume na haki za binadamu pamoja na mauaji ya raia. Kundi la M23 lililobaki nchini DRC sasa linaongozwa na Sultani Makenga. Kundi hilo limeendelea kuukalia mji wa Rutchuru huku likisababisha madhara makubwa kwa jamii.

Tokea mgogoro wa DRC uanze, Umoja wa Mataifa umekuwa ukichukua hatua mbalimbali kujaribu kuleta hali ya amani ndani ya DRC. Ikumbukwe kuwa Katibu Mkuu wa Pili wa Umoja wa Mataifa Bwana Dag Hjalmar Agne Carl Hammarskjöld alifariki dunia tarehe 18 Septemba 1961 kwa ajali ya ndege katika Eneo la Ndola huko Zambia (Wakati huo Rhodesia)akiwa katika jitihada za kutafuta suluhisho la mgogoro wa DRC.
 
JWTZ na majeshi mengine ya SA na Malawi yote yapo front. Tofauti ni kuwa JWTZ ndiyo lead army kwa kutoa kamanda wa majeshi ya FIB na viongozi. Hawajatulia kaka. Habari zilizopo ni kuwa Miji iliyokaliwa kiukamilfu mpaka sasa ni Kiwanja, Rumangabo, Kitale, Kibumba, Kibati, Munigi, Rwaza na Kalengele.

Nataka kujua miji iliyokaliwa na M23 Siyo Serikali ya kongo ili niweze ku-predict kazi iliyobakia
 
Mbona unaonekana km mtu uliyeenda shuke na unajua mambo hasa socialogy na polotical, we unafanya biahsra kweli au ni intelenjesia wetu unafanya kazi yako? hebu tueleze una muda gani unafanya u-FBI huko< tunakuomba usiwe kama mmarekani snoden. Naamini huwezi kuwa businessma huko kwa mtutu uliopo huko siyo rahisi. una uelewa mkubwa.
 
Kama unafuatilia vizuri jamaa walifanikiwa kuwa-push back na mapigano yakasimama kabisa. UN iliamua kuwa yafanyike mazungumzo ya kumaliza mgogoro huu. Hapo ndipo majeshi hayo yalitakiwa kurejea makwao. Kumbuka hiyo ilikuwa ni initiative ya SADC.
Sawasawa, kwanini hawakuweza kuwa-push back miaka hiyo?
Ndiyo maana wengi wetu tulikuwa tunaona kuwa Rwanda ni nchi ndogo kulinganiusha na hizo, ila inawapa headache. Sasa kwanini walishindwa kuwasukuma mipakani wakati ule?
 
Mkuu, JWTZ ndo wapo front na wanatoa kipigo vibaya mno. FARDC walishashindwa na M23 Siku nyingi, tangu JWTZ kutua Goma ndo tunawasikia na hao FARDC.
Nadhani ndio maana kagame ameanza visa na Tanzania....tutamtandika kama mwizi, hatujui huyu
 
Kwani si inasemekana marekani anashiriki kwa kiasi kikubwa sana kufanya wizi wa madini congo,kimetokea nini mpaka akaamua kumbadilikia m23(rwanda) aliyeko on ground kupiga mzigo?
 
Mm kaka napenda kuuliza maswali machache...wasaidizi wa karibu wa rais kabila ni watu wenye uwezo kiasi gani? Wa kumshauri na pia suala la kwamba rais kabila sio mkongo je linainfluence chochote kwenye governance ya raisi kabila
 
Huyo afisa aliyefairki ni mwingine tofauti na yule wa miezi iliyopita? au ndiyo yule yule? tunaambiwa kuwa jeshi letu linalinda amani tu haliko front kuna ukweli?

Nasikia amani ya kweli haiwezi kupatakana bila paul Kgame kutolewa madarakani, na hii vita itaishia ilikoanzia yaana Rwanda. tunataka kumtia adabu huyu rais mwenye damu za watu na anayetishia kumuaa rais wetu,
tunafikir vita hii mwisho wake ni kigari unasemaje?
Tunashukuru kwa taarifa kwa sababu baba na kaka zetu wapo huko, inshallah MUNGU atawasaidia.

sasa haya ni maswali,maoni,taarifa au vitisho jamani?ha ha haa!punguza hasira mkuu!
 
Back
Top Bottom