ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,115
- 49,833
Hivi hao M23 Wana Nguvu kiasi gani Hadi wanawazi Majeshi ya DRC na Washirika wa EAC?
Hivi DRC inajitambua kweli? Lile beat la Felix Tshisekedi kwamba ataishambulia Rwanda limeishia wapi wakati M23 Wanazidi kusogelea Mji wa Goma na maelfu ya watu kukimbia?
Hii ni aibu kubwa sana Kwa Linchi kubwa kama DRC kupelekeshwa na kanchi ka Rwanda.
==
Emile Bolingo hana uhakika kuhusu muda ambao yeye na wakazi wengine wa mji wa Goma, uliopo mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wataweza kustahimili hali inayowakumba.
Mji huu mkuu na ambao ni muhimu katika eneo hili, ambalo lina wakazi milioni mbili, limekatizwa kwa siku kadhaa na maeneo ya mashambani ambayo ndio panapotokea chakula kinachowalisha wakazi wake.
Hii ndio hali ya hivi karibuni ya kuzuka kwa ghasia na mapigano ambayo yamewasababisha watu zaidi ya milioni saba kuwa wakimbizi wa ndani na kuhama makazi kwa sababu ya vita vya mara kwa mara.
Waasi kutoka kundi la M23 ambalo linaongozwa na jamii ya AbaTutsi wamefunga barabara mbili kuu zinazoingia na kutoka Goma kwa upande wa Kaskazini na magharibi na kutatitza hatua za kuingiza chakula mjini humo.
‘Tunaogopa kwamba tutakabiliwa na njaa ikiwa jeshi la DRC halitakomboa hata angalau barabara moja kati ya hizo mbili kuu hivi karibuni. Unaweza kuhisi hali ya wasiwasi ilivyojaa huku…watu wameogopa sana,’ Bolingo aliiambia BBC.
Mundeke Kandundao, ambaye ni mwendeshaji bodaboda, amefanyiwa upasuaji hivi karibuni baada ya kuathirika kwenye shambulizi la kombora.
BBC Swahili

Makabiliano DRC: Wasiwasi waikumba Goma huku kundi la M23 likipiga hatua