Uliza lolote kuhusu mgogoro ndani ya DRC hasa mapigano kati ya M23 na FARDC

Mkuu FLASH HIDER hii nimeipata BBC "Kundi la waasi wa ADF nalo laripotiwa kutekeleza mauaji ya watu kumi na watatu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Makundi ya waasi yanasema masaibu ya DRC yangalipo licha ya M23 kushindwa." Mkuu huko mashariki ndo walipo askari wetu, na wameshaanza kudeal FDLR, najua vipo vikundi vingi lakini hawa ADF ndio akina nani haswa?
 
Mkuu FLASH HIDER pole kwa mihangaiko; hii nimeipata BBC "Kundi la waasi wa ADF nalo laripotiwa kutekeleza mauaji ya watu kumi na watatu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Makundi ya waasi yanasema masaibu ya DRC yangalipo licha ya M23 kushindwa." Mkuu huko mashariki ndo walipo askari wetu, na wameshaanza kudeal FDLR, najua vipo vikundi vingi lakini hawa ADF ndio akina nani haswa?
 
Kundi la ADF (Allied Democratic Front) ilianzishwa mwaka 1995 huko Uganda na Jamili Mukulu. Kundi hili linatajwa kuwa lina msimamo wa kislam ambapo malengo yake ya awali yalikuwa ni kuiondoa serikali ya Rais Museven (Kafiri). Baada ya serikali ya Uganda kufanya Operesheni mbalimbali dhidi ya kundi hili ndani ya Uganda, kundi hili lilivuka mpaka na kuingia DRC eneo la Beni ambako liliungana na kundi jingine liitwalo NALU (National Allience for Liberation of Uganda) na kuunda ADF-NALU. Kwa hapa DRC kundi hili lipo eneo la Beni na limekuwa kifanya mauaji makubwa kwa raia na vikosi vya serikali pamoja na UN. Linajihusisha na uchimbaji madini, Uwindaji, Ulimaji, Uchomaji wa Mkaa na biashara ya usafirishaji (bodaboda) na daladala. Ukienda BENI inaelezwa kuwa bodaboda na daladala nyingi zinamilikiwa na ADF-NALU. Kimsingi lengo la kuiangusha serikali ya Museveni linaonekana kama halipo tena bali wapo huko kimaisha zaidi ingawa ni hatari sana.
Hivi karibuni wameanza kuhusishwa na Al Shabaab hasa baada ya Alshabaab kushambuliwa huko SOMALIA. Linapata misaada kutoka kwa jamii mbalimali za kiislam duniani. Changamoto kubwa ni kuhusu eneo lilipo kwani lina misitu minene na milima mikubwa.
Wanajeshi wa Tanzania nasikia wamepelekwa huko maana hata hapa mjini hawaonekani. Nitawafahamisha zaidi kuhusu kundi hili.

Mkuu FLASH HIDER pole kwa mihangaiko; hii nimeipata BBC "Kundi la waasi wa ADF nalo laripotiwa kutekeleza mauaji ya watu kumi na watatu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Makundi ya waasi yanasema masaibu ya DRC yangalipo licha ya M23 kushindwa." Mkuu huko mashariki ndo walipo askari wetu, na wameshaanza kudeal FDLR, najua vipo vikundi vingi lakini hawa ADF ndio akina nani haswa?
 
Flash Hider asante sana kwa updates zote na pia hongera kwa jeshi letu la JWTZ linafanya kazi nzuri sana huko hata kumpa Rais wetu nguvu ya kutoa kauli huru kuelezea msimamo wa nchi yetu bila woga.

Mungu ibariki JWTZ iwamalize na hao ADF pamoja na vikundi vyote vinavyosumbua DRC ili waendelee kututungia nyimbo nyingi za ndombolo zije bongo tucheze.
 
Back
Top Bottom