Ulishughulika vipi na kisa cha namna hii?

Ulishughulika vipi na kisa cha namna hii?

Kwa kweli mmenielimisha pakubwa. Nilikuwa nawaza kumuoa lakini sasa nimepata sababu kwanini ni hatari kuingia nae katika maisha.
Huyo hakupendi mkuu, angekuwa anakupenda angefanya yafuatayo÷

Angesimama bega kwa bega na wewe tangu mwanzo.

Ange kupiga tafu na kukupa moyo pengine hata kukufariji katika mishe mishe zako , kwasababu anajua utakuwa nae katika mausha.

Asinge kuacha kwa staili aliyofanya , kama alikuwa na malengo na wewe, maana mwanamke anae kuheshimu hawezi kufanya aliyofanya huyo.

HUYO AMESHACHEMKA , AMESHATUMIKA SANA MPAKA WAMEMCHOKA , AMEONA WEWE ULIKUWA UNAMPENDA SANA NDIO MAANA ANAKUJA KIJARIBU HAHATI YAKE.

KIFUPI NI GARI BOVU HILO
 
Kwanza kwanini huna mwanamke mpaka leo kwa umri wako?
Nilikuwa nae kaka. Ila tuliachana kwa masuala la usaliti. Ulipata scholarship ya kwenda Australia, akarudi likizo akiwa mjamzito. Sasa hivi sitaki mahusiano ya kiujana ujana nataka kuoa tu.
 
Kula mzigo huo pita ivi nimekutana na izo screnario zote nimezichalaza Miti, then nime mute Siwapi namba zangu official hata kidogo
 
Mkuu hili wala sio swala la kuuliza. Huyu mleta mada ana viashiria vyote vya udomo zege kama vile:
1. Yuko singo. Mwanaume unaejua kutongoza, una kazi, una hela, una pa kuishi, unaanzia wapi kuwa singo? Yaani wanawake wote waliojaa kila mahali umeshindwa kuwapata? Kweli mpaka unakuja kukutana na mwanamke mlieachana form five halafu ulivyo ukamuambia ukweli kwamba uko singo! Yaani kwanza dem atakua kakushusha thamani sana kujua upo singo.
2. Tabia ya wanaume madomo zege ni kwamba huwa hawaachi mzoga! Yeye kwake kitendo cha mwanamke kumzoea anaona kama ngekewa maana la sivyo hajui atapata wapi mwingine?
3. Mwanamke kakutana nae juzi, lakini angalia kwenye uzi huu tangu mwanzo anamtetea jinsi ambavyo hataki kumuumiza, mara akimuacha atamuelewaje, mara ataonekana mshenzi.. ata hajajua kama mwanamke kweli anamtaka au labda ni ana shida anataka kumkopa tu hela?😂😂
4. Jamaa yuko tayari kumkaribisha dem aliekutana nae juzi nyumbani kwake! We ulisikia wapi? Demu umekutana nae baada ya kupotezana miaka kibao, hujui saiz anafanya mishe gani we unamkaribishaje home? Kama ni jambazi? Au malaya anajiuza?

NB: udomo zege sio tusi, ni hali.
Nimeomba ushauri au nimeomba univunje mbavu ?😂😂😂

Eti "hawaachi mizoga"😂

Kwahiyo kaka naonekana namtetea mwanzo mwisho ?😂
 
Nimeomba ushauri au nimeomba univunje mbavu ?😂😂😂

Eti "hawaachi mizoga"😂

Kwahiyo kaka naonekana namtetea mwanzo mwisho ?😂

I swear mkuu kwa nnavyokufahamu huyu demu humuachi hata kwa dawa! Lazima utamtafuna tu maana unaonekana una ukame sana wewe na hapo ni kama mbuzi kafia kwa muuza supu 🤣🤣🤣🤣 Kwanza usikute umeshamla umekuja hapa na stori ndeefu kupima upepo tu
 
Alikuwa sawa kukataa mkiwa wanafunzi (form six). Bado unamuona mzuri? Unampenda? Kama ndio, jipe muda ufahamu vizuri kwa nini "karudi" kwako (motives). Inaweza kuwa uchumi, revenge (wengine akishaukwaa, anataka kuusambaza!).

Hili mara nyingi halichukui muda. Ila kwa kuanzia, usikubali mtego wa "kumlala" mapema.....itakunyima fursa ya kumfahamu na kufanya maamuzi sahihi.
 
Natamani JF ingekua na uwezo wa Kutuma Voice note...


Anyways huyo dada anajijua yeye mzuri sasa wewe hukua type yake wakati mpo shule akawa anacheza na monta wenu ndo alikua type yake. Kaenda UDSM keshachezewa vya kutosha type yake sio type zao sasa kaona arudishe mpira kwako kwa kua anajua ulikua unampenda at one point. Huyo akija jmoc anakuja tayari kwa kuliwa. Na ukimla tu basi hakuachi huyo. Danny Unataka kumla au hutaki? Kama unataka kumla kulipiza alivyokua anakukataa enzi za shule, hapa nakushauri kama mwanamke peleka hiyo manzi gesti/lodge tena usimfuk bila condom. Huyo sio manzi ya kula getto atakuganda sana. Piga pita hivi ikiwezekana hata kwako asipajue.... labda ana mimba anaitaftia baba. Akili kumkichwa.
Hivi we ni Sakayo? samahani lakini kama nimekukwaza kukuuliza Mama.
 
Huyo hakupendi mkuu, angekuwa anakupenda angefanya yafuatayo÷

Angesimama bega kwa bega na wewe tangu mwanzo.

Ange kupiga tafu na kukupa moyo pengine hata kukufariji katika mishe mishe zako , kwasababu anajua utakuwa nae katika mausha.

Asinge kuacha kwa staili aliyofanya , kama alikuwa na malengo na wewe, maana mwanamke anae kuheshimu hawezi kufanya aliyofanya huyo.

HUYO AMESHACHEMKA , AMESHATUMIKA SANA MPAKA WAMEMCHOKA , AMEONA WEWE ULIKUWA UNAMPENDA SANA NDIO MAANA ANAKUJA KIJARIBU HAHATI YAKE.

KIFUPI NI GARI BOVU HILO
Hakika ninakubali. Asante sana
 
Huyu msichana nilisoma nae 'A' level katika shule fulani hapa Dar es salaam. Darasani kwetu hakuna ambae hakumjua maana alikuwa msichana mwenye sura nzuri sana tena kuliko wote darasani. Ila hakuwa social kiviile. Alikuwa na rafiki zake aliowazoea na hakupenda mazoea sana.

Sasa mi nikawa nimempenda. Nikaanza kumtongoza tokea tunaanza form five. Kipindi ambacho mimi ndo nilikuwa mtu wa kwanza kumtongoza pale shuleni lakini alinikataa. Baada ya miezi mitatu nikapiga moyo konde nikamtongoza tena akakataa nikapotezea.

Tukiwa tunafanya mitihani ya mwisho tunaingia form 6 nikasema ngoja nijaribu tena nikamtongoza tena kwa mara ya tatu akakataa. Nikamuomba namba ili tuwe tunawasiliana maana kuna rafiki yangu mmoja 'Kishoro' (bado marafiki mpaka sasa) alinishauri bora niwe naenda nae taratibu niwe nawasiliana nae namuhonga honga vocha, na ukizingatia kilikuwa kipindi cha mitihani tunakaribia kwenda likizo. Nikamuomba namba akaninyima.

Baadae tukiwa likizo nikaitafuta namba yake kwa mtu mwingine. Nikampigia simu akawa ananijibu kwa mkato ili maongezi yaishe nikimtumia meseji hajibu kabisa.

Nikaacha kuongea nae tukaingia form 6. Nikawa najaribu kwenda nae taratibu nikawa nalazimisha urafiki. Akawa ananikwepa kwepa. Hataki story na mimi. (Inauma sana aiseee!). Kuna siku nilimuomba twende Kunduchi beach jumamosi kila kitu nitalipa mimi (baada ya kukopa sana maana mwanafunzi hela unatoa wapi ?). Akakataa nikaja kuskia Jumamos alienda Beach kombo na monitor wetu nilikuja kuambiwa baada ya kumaliza kuwa wakati tunakaribia kumaliza alianza mahusiano na monitor.

Tukiwa tunakaribia kufanya paper ya Form 6 nikataka nimtongoze tena akakataa kuongea namimi. Ila tu nikamwambia "Sawa. Ila hakuna msichana nilikuwa nampenda kama wewe". Hakujibu akaondoka. Tukafanya paper tukamaliza.

Toka tumemaliza form 6 sikuwahi kuonana nae tena. Nimemaliza chuo miaka miwili iliyopita(degree)
Kazi nnayoifanya ni tofauti na niliyosomea. Sio ya maslahi ila inaniwezesha kuishi Dar. Nilishamsahau maana hatujaonana mda mrefu. Sasa juzi(jumatatu) niko makumbusho nasubiri daladala ya ubungo nikashangaa naguswa bega. Kugeuka ni yeye. Moyo ukapiga paa. Nilishangaa sana maana hakuwahi nianza mazungumzo wala kunisalimia popote.

Akaniambia Danny za siku nyingi nikamwambia safi. Tukaongea sana. Sana, tukakumbushana watu tuliosoma nao, mambo ya shule. Ila Gari la Kunduchi lilipofika akataka kupanda aondoke. Akaniambia "Danny naomba namba yako tuwasiliane." Nikashangaa sana. Nikampa namba.

Nilivofika nyumbani nikawaza sana kwamba kinachotokea ninaota ? Prisca wakuniomba mimi namba ? Mimi ambae miaka kadhaa iliyopita alininyima namba yake nikaitafuta kwa mtu mwingine ?

Ilivyofika saa tano kasoro akanipigia simu nikapokea. Tukaongea stori kibao. Hakusema kwanini amenipigia zaidi ya story za hapa na pale. Akanipa story za UDSM (mimi nilisoma SAUT). Baadae tukaagana nikalala. Ila asubuhi wazo la kwanza lililonijia ni kuwa yawezekana Prisca anataka kunikubali sasa hivi. Maana haiwezekani Prisca anipigie mimi Danny simu hivihivi. Tena Prisca, anipigie mie simu ?

Jumannne hatukuwasiliana ila Jana jumatano alinipigia simu mchana akanilaumu sana kwa sauti ya mapenzi mbona sikumtafuta siku ya Jumanne ? Mi nikamwambia 'sikuwa na vocha' ila sikuwa na sababu ya kumtafuta kusema ukweli. Tukiwa tunaongea na simu hiyo jana akaniuliza vipi wifi mzima ? Nikamwambia sina mwanamke. Akaniambia anataka kuja kunitembelea Jumamosi. Nikamwambia nikipata muda ntakwambia.

Nikakutana na Kishoro kumuomba ushauri. Alichoniambia ndicho kinachonifanya nilete uzi hapa.

Kishoro alisema: "Hakupendi huyo, ila tu anakuja kwako kupooza machungu kwa sababu aliowataka yawezekana kagombana nao. Sasa we jiangalie wewe unampenda ama humpendi?".

Mimi, naweza sema nampenda ila sio sana kama nilivyokuwa nampenda kipindi kile; ni kama alinitoka kiukweli, ila sijiskii vizuri kumpotezea. Nipo single na nataka KUOA(sitaki mahusiano ya kucheza cheza) lakini nafsi yangu inasita kumuoa yeye.

Ila pia maneno ya Kishoro yanajirudia rudia sana kwenye akili yangu "Hakupendi huyo, do for your own risk."

Halafu mimi mwenyewe nashangaa. Alivyokuwa ananitreat kipindi kile, leo hii Prisca ananipigia simu ? Ananiuliza mbona sijamtafuta ? Halafu anataka kuja kunitembelea ? Huyu ni Prisca kweli au naota ndoto za mchana ?

Anyway, Yawezekana humu kuna watu waliwahi kupitia kisa kinachofanana na changu na wangependa kushare uzoefu wao jinsi walivyoshughulika na hivyo visa. Ntafurahi nikipata kuskia kutoka kwenu.

Lakini pia dada zangu mtanisaidia maoni yenu; Je, inawezekana kwa mwanamke ambae alikuwa hakupendi miaka ya nyuma akaja kwako kwa upendo wa dhati ?

NB:Kuna vitu vingi nimevitoa ili kufupisha story, kama bado ndefu mniwie radhi
ACHANA NAE,
ulimtaka hakukutaka, anakutaka kwa muda anaotak yy wewe unamtaka.
ukikubali aingie katika maisha yako she wins, you lose.
hakuna pride yoyote kulala na women wasiostahili.
dont lose your dignity man, wewe sio rebound samaki wapo wengi baharin
 
I swear mkuu kwa nnavyokufahamu huyu demu humuachi hata kwa dawa! Lazima utamtafuna tu maana unaonekana una ukame sana wewe na hapo ni kama mbuzi kafia kwa muuza supu 🤣🤣🤣🤣 Kwanza usikute umeshamla umekuja hapa na stori ndeefu kupima upepo tu
Sasa na mimi mbona silagi mzoga😂😂😂.

Kwa kweli kaka nimezingatia ushauri wa watu mbali mbali. Nimeona ni hatari sana kuingia nae katika maisha.
 
Alikuwa sawa kukataa mkiwa wanafunzi (form six). Bado unamuona mzuri? Unampenda? Kama ndio, jipe muda ufahamu vizuri kwa nini "karudi" kwako (motives). Inaweza kuwa uchumi, revenge (wengine akishaukwaa, anataka kuusambaza!).

Hili mara nyingi halichukui muda. Ila kwa kuanzia, usikubali mtego wa "kumlala" mapema.....itakunyima fursa ya kumfahamu na kufanya maamuzi sahihi.
Asante ndugu yangu. Kwa kweli ni mapema mno kupeleka mambo fasta fasta.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom