kuna siku mshua alinipigia simu akasema tukutane Bar moja hivi kule ukonga inaitwa Alawa nkafika bila kufika mana nilijua kitibaridi kitakuwepo,basi ile tunapiga story mbili tatu na mshua si ndio akaja Mhudumu wa ile bar akakaa nasi.Wakaanza story na mshua mimi nawachora tu,mshua akaniambia mama yako mdogo huyo .Dah kumuamkia nashindwa mana tupo wa rika moja na alikuwa kaumbika balaa yani kiuno kwenda juu ni hataree.Nikawa namwangalia jinsi alivyobomba kwa kuibia ibia ili mshua asinishtukie si unajua washua wengine wanaweza wasikuite tena.Yani hapa ninampango wa kumuuliza mmshua kuwa mama mdogo anaendeleaje huko hajambo.Ila kuna siku nitaenda mwenyewe pale ALAWA na kama mama mdogo hayupo sitanunua kitu chochote nitarudi home