NO04
JF-Expert Member
- Jun 29, 2015
- 1,754
- 1,232
Kupitia hapa anaweza kupata koneksheni. Mfn, hata wewe naamini unaweza mpatia mchongo wowote akikutafta inbox, sio!? Maana unamwanga flani nauona. Barikiwa mkuu! MdaidieMdogo tuko nje ya mada kidogo, Ila wakati unasubiri connection hebu jaribu kujipambania kidogo Mambo yaende. Kama huna ajira rasmi, Basi jaribu kufanya kazi za kutumia nguvu za mwili upate hela ya kujikimu.
Mfano. Je wasiosoma kabisa wanaishije!???
1) saidia Fundi
2) kuchimba mchanga
3) kukusanya mawe
4) kuchimba kifusi
5) kubeba mizigo
6) dereva boda boda au bajaji kwa maeneo ya mjini
7) kua dalali wa vitu mbalimbali eg. Simu, vyumba, pikipiki n.k
8) omba utingo, tandiboi kwenye magari makubwa.
Cha muhimu ilimradi upate fedha ya kujikimu unapo endelea kutafuta ajira au kusubiri connection, huwezi kukaa tu bila kazi yoyote na kusubiri hivyo vitu mzee, lazima maisha yawe magumu tu.
Mm Ni Kama wewe nimegraduate kwa course Kama yako. Na Sina ajira mpaka leo. Na ninaafanya kazi zangu mwenyewe tu maisha yanaenda najikimu vizuri na nasaidia kidogo wazazi wangu.