Nina uhusiano na mke wa mtu. Natamani kumuacha lakini inakuwa ngumu

ngungwangungwa

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
642
554
Wanajamvi umofia kwenu,kwa wakristu wenzangu heri ya Ijumaa kuu.

Naomba nisiwachoshe. Binafsi nimeoa,nna mke naishi na familia yangu vizuri tu. Lkn nina hili tatizo ambalo kwa sasa limekuwa kero kubwa sana kwangu.

Mm ni kijana wa zamani kidogo umri wangu ni 40+ lkn huyu binti umri wake ni 25. Nilianza kudate naye tangu mwaka 2016. Huyu binti aliolewa mapema sana aliolewa mwaka 2011,baada tu ya kumaliza elimu ya Msingi. Na mwaka 2013 akawa amepata mtoto. Amedumu ktk hiyo ndoa hadi mwaka 2015 akaachika baada ya kushindana tabia na mwanaume huyo.

Baada ya kurudi kwao,ndio nikabahatika kukutana naye kuna siku alikuja ofisini kwangu kupata huduma,akanivutia na tukaongea mawili matatu kisha tukapeana contact safari ikaanzia hapo. Na tarehe 14 February mwaka 2016 rasmi nikaanza kudate naye.

Aisee kwanza sikutegemea kama ningeweza kudumu naye kwa kipindi kirefu kwa jinsi nilivyokuwa namchukulia.

Lkn ndo hivyo nimejikuta nipo naye hadi leo. Sikuwahi kumuahidi kumuoa. Mwaka juzi 2017 mwishoni,akachumbiwa,me hakuniambia. Alichumbiwa mwezi wa 11. Baada ya kuchumbiwa,kwa kiasi fulani akapunguza usumbufu kwangu na mimi wala sikumfuatilia. Lkn siku moja mwaka jana,akaja ofisini akinilalamikia me namchunia na maneno meengiii...!!

Siku hiyo alibaki hapo hadi muda wa kufunga. Nikafunga nikaenda naye kupiga show,me nikamuacha lodge nikaenda kulala kwangu,lkn siku hiyo ndio akaniambia km anataka kuolewa. Aisee,nilifurahi sana moyoni. Lkn akaniambia anataka idhini yangu,kama nipo tayari aolewe lkn nisimuache.

Kwa vile me nilijua anaenda kuwa mke wa mtu, nikamwambia asijali. Huku me nikijua kabisa hii ndo nafuu yangu. Kweli taratibu za ndoa zikaendelea na hatimae akaolewa mwaka jana mwezi wa 8.

Cha ajabu nilivyoona kweli anaolewa,kuna hali ya wivu ikaanza kuniingia. Siku ya ndoa ilikuwa Jumamosi,nikamlazimisha siku moja kabla ya ndoa lazima nipige mashine,demu akasema wewe tu yaani hata ukitaka siku yenyewe. Nikamwambia basi tufanye siku ya ndoa mapema alfajiri.

Me nikaenda kulala lodge ya karibu kabisa na huko kwao,nikampa maelekezo kweli saa 11 alfajiri akapiga simu anakuja. Nikapiga mashine hadi saa 2 asbh.

Binti akaolewa kweli. Tangu siku hiyo ya Jumamosi hakupatikana kwenye simu. Tulikubaliana kwamba,akiolewa atakaa ndani siku 7.( Nasikia hizo siku huwa ni za fimbo tu). Lkn demu kwa mazoea ambayo alishajijengea kwangu,alishindwa kumudu zile kumaliza zile siku 7. Jumatano tu ya wiki iliyofuata akanitafuta na tukaonana.

Tukayajenga na kesho yake mzigo nikapiga tena.

Tumefanya mengi sana na huyu dada lkn sasa kusema kweli,najisikia vibaya sana naona namnyanyasa sana huyu dogo aliyemuoa.

Maana mwanamke kwa sasa kawa kama mtumwa kwangu. Yaani hata akiwa na mumewe ukimwambia njoo,hata kama alikuwa anapika ataacha kila kitu.

Kiukweli nimeshajaribu sana kumwambia tuachane lkn inashindikana kwa sababu ya jinsi tulivyozoeana. Uhusiano wetu hata mama yake anaujua.

Natamani sana nimuache lkn nashindwa. Nitumie njia gani ambayo haitakuwa na madhara kwa pande zote!?? Yaani huwa namhurumia sana jamaa,mfano demu nikiwa naye jamaa anapiga simu hazipokelewi.

Mfano juzi hakuenda kazini,mchana akaja tukawa wote,baadae mumewe akawa anapiga simu lkn simu ikawa silent,na wakati huo sisi tunafanya yetu. Alivyopiga simu sana na simu haipokelewi,akatuma SMS akisema mwambie achomoe kwanza upokee simu..! Nilijisikia vibaya sana,na baadae demu alivyofika nyumbani akaongea naye akasema alitoka lkn simu aliacha ndani,maana jamaa alikuwa kazini.

Na jamaa hagusi kabisa simu ya mkewe. Na demu huwa hafuti SMS wala picha zetu na anajiamini kwa sababu simu ina password.

Kiukweli me kwa sasa natamani kumuacha maana hata mke wangu alishahisi kama natembea naye.

Naombeni nichukue njia gani kuachana naye!??

Nawasilisha kwenu.
 
Kuna sentensi mbili zimenifanya niwaze mbali sana, unaposema uhusiano wenu hadi mama yake binti anaujua na ambapo jamaa alituma sms mwambie achomoe upokee simu kwanza daah i can't feel namna hao watu wawili wanavyojiskia, Mama yake binti na mumewe!!
 
Simamia maamuzi yako unapoamua, kumbuka kwamba siku zote mwenye nguvu ya kusitisha mahusiano baina ya mke wa mtu na mwanaume yyt nje ya ndoa yake ni mwanaume. Ingawa wana ushawishi sana hawa viumbe i.e unaweza ukaamua kwa dhati kbs na kujiaminisha kwamba hutomt* mba tena ikapita hata mwaka au miaka lakini siku akiamua kukuingiza mtegoni unalegeza msimamo wako hasa hasa kama ulimkuna vilivyo na mbaya zaidi mkiwa mnaishi eneo moja ndio balaa zaidi.
 
Bravo JWTZ
tumblr_o6wgftCyph1r9khx4o1_400.gif
 
Kuna sentensi mbili zimenifanya niwaze mbali sana, unaposema uhusiano wenu hadi mama yake binti anaujua na ambapo jamaa alituma sms mwambie achomoe upokee simu kwanza daah i can't feel namna hao watu wawili wanavyojiskia, Mama yake binti na mumewe!!
Mama wa mabinti wengi wao huwa support binti zao hasa kama anaona kbs bintiye ana furaha na anachokifanya, mbaya zaidi me uwe na tabia ya kuhudumia aaaah wamama mbona hata nyumbani kwake sometimes anakuandalia mazingira unaenda kuchapa bintiye.

Speaking from experience
 
Duh!Unapaswa ufe na ufufuke na Yesu mkuu.Huwa ni ngumu sana kumuacha mtu uliyezoeana naye akiwa ni mwandani/hawara yako.Nakushauri tafuta siku tulivu,muite umueleze namna unavyouona uhusiano wenu.Ni uhusiano ndani ya uhusiano wa ndoa mbili.Mueleze wazi kwamba hauwezi kumuoa,ajue hilo.Vilevile weye ni mume wa mtu.Mkatishe uhusiano huo.Ni hatari kwa mustakabali wa maisha yenu.
Kumbuka,yule mumewe unayemuita dogo,akipata uhakika wa uhusiano wenu atageuka kuwa mbogo.Si yeye tu.Hata nduguze na nduguzo pia.Ninyi hamuiheshimu taasisi ya ndoa.Mbadilike.Mnaweza kupata mtoto asiye/wasio halali wa ndoa zenu ambao baadaye watazua kasheshe miongoni mwa familia zenu.Ni ngumu lakini inawezekana.Ikibidi jitahidi muishi maeneo yasiyo jirani jirani kuepusha kushawishiana.
 
Huyo dogo anakulia taiming tu mkuu usimchukulie boya kihivyo.
Jihadhari kaka kabla hayajakufika na kuharibu heshima yako ndogo iliyosalia.
Acha mahusiano na huyo mdada haraka na wala huna sababu ya kujiuliza mara mbili mbili,huyo si wa kwako ana mumewe sasa...NI MKE WA MTU!.
 
Can you share hata experience moja mkuu!!! I ask for this favor
Mama wa mabinti wengi wao huwa support binti zao hasa kama anaona kbs bintiye ana furaha na anachokifanya, mbaya zaidi me uwe na tabia ya kuhudumia aaaah wamama mbona hata nyumbani kwake sometimes anakuandalia mazingira unaenda kuchapa bintiye.

Speaking from experience
 
Sema Nini mzee

Unakosea Sana
Muhurumie mwanaume mwenzio.

Malipo hapa hapa duniani Kaka.
Mkuu sifanyi utani hapa ukweli kabisa hiii hali inanisumbua sana...kweli kabisa natamani kumuacha huyu dada,shida iliyopo kwanza ni mazoea,kumbuka ameolewa nikiwa naye. Ujue tuna mazoea yale ya ndani kabisa,masikhara upendo hata km wa kitapeli lkn ndo maisha yetu. So kuna wakati namkazia lkn anaondoka kwa mumewe anaenda kwa mama yake. Na huko mama atanisumbua balaa! Mama huyo ndo mtoto wake wa pekee! Huwa hapendi kabisa kumuona mwanaye akiwa hana furaha. Na nna heshimiana sana na mama...na ukimwambia issue ya kumuacha anakuambia bora yeye aondoke kwa mwanaume.
 
Mkuu sifanyi utani hapa ukweli kabisa hiii hali inanisumbua sana...kweli kabisa natamani kumuacha huyu dada,shida iliyopo kwanza ni mazoea,kumbuka ameolewa nikiwa naye. Ujue tuna mazoea yale ya ndani kabisa,masikhara upendo hata km wa kitapeli lkn ndo maisha yetu. So kuna wakati namkazia lkn anaondoka kwa mumewe anaenda kwa mama yake. Na huko mama atanisumbua balaa! Mama huyo ndo mtoto wake wa pekee! Huwa hapendi kabisa kumuona mwanaye akiwa hana furaha. Na nna heshimiana sana na mama...na ukimwambia issue ya kumuacha anakuambia bora yeye aondoke kwa mwanaume.
Hapo mwanamke pia nae Ni tatizo na huyo mama pia.

Kwanini wakubali aolewe na mwanaume mwngne kumbe hawampendi???

Hivi mfano ungekuwa ww ndo unafanyiwa hivo ungejiskiaje??





Tatizo
TUNAOA WAPENZI WAWATU
 
Kiongozi hakuna cha kuona huruma hebu mwache huyo binti ....uzinzi dhambi.....halafu hawa wanawake wanaokubali kuolewa halafu wanacheat huwa wanamaanisha nini labda??? Kwa nini kaolewa???
Mkuu hivyo vitu nimefanya sana,lkn ujue anapafahamu ofisini kwangu,lkn yeye anasema na siyo yeye tu,hata mama yake anasema km tatizo ni huyo mwanaume yy yupo tayari kuondoka. Mkuu ktk kutafuta jinsi ya kumuacha huyo dada,nilishawahi tena mwezi uliopita tu,nilichukua laini tofauti na zangu,nikajifanya me ni rafiki yake na huyo mwanaume lkn sitaki anijue. Nikamtumia SMS kumwambia kuwa kuna jamaa anatembea na mke wake,lengo langu achukue hatua za kumuogopesha. Yaani nilimueleza mpka muda anaopenda kupita. Nilimtumia maelezo mazuri sana..yy akawa ananipigia simu kutaka anijue nikawa sipokei. Cha ajabu jioni alivyorudi nyumbani,akamuonyesha mkewe zile SMS huku akisema kuna mbea anataka kutuchonganisha hapa hebu ona hizi SMS...!! Demu akazipiga screenshot akanitumia halafu akazifuta. Jamaa wala hakutilia maanani!
 
Hapo mwanamke pia nae Ni tatizo na huyo mama pia.

Kwanini wakubali aolewe na mwanaume mwngne kumbe hawampendi???

Hivi mfano ungekuwa ww ndo unafanyiwa hivo ungejiskiaje??





Tatizo
TUNAOA WAPENZI WAWATU
Mkuu mm hadi kuja kuandika hapa,hili jambo limenisumbua sana...!! Hata sielewi nifanye nn!!?? Yaani natamani hata nije nimuweke lodge halafu nimpigie jamaa akafumanie me nikiwa simo. Lkn najiuliza nikifanya hivyo atabaki naye au atamuacha!.. ?? Maana akimuacha ntakuwa nimemuaibisha bure mdada wa watu.
 
Back
Top Bottom