Soyuncu
Senior Member
- Nov 20, 2019
- 193
- 231
Boss boss.. Mi nijuavyo bas likitoka ubungo terminal stend ya kwanza kusimama mbez..
Sasa apo kwenye Mataa uyo Dada alipandaje Au kwa vile nimechelewa kufika dar
Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa apo kwenye Mataa uyo Dada alipandaje Au kwa vile nimechelewa kufika dar
Kuna mda kila kitu kinapangwa ili kitokee nakumbuka 2012 baada ya kuchelewa sana kulala kutokana na tungi najikurupua saa 3 asubuh ili niwah ubungo nichukue Basi la Arusha mana ilikuwa siku ya jumapili,jumatatu Kama kawaida natakiwa job Arusha.
Nimefikaa ubungo terminal kwenye saa 4 hv nakuta gari zote nzur zishaondoka ikanibidi nichukue Basi la KVC na tena na yenyewe nilikuta imebakiza siti mbili tena za mwisho kabisa kwenye siti ya watu 6,ile kutoka tu ndani ya stendi kufika kwenye mataa ya ubungo Kuna mdada akapanda yupo vzr ana shepu balaa.
Baada ya kupanda akaja moja kwa moja kwenye seat ambayo ilikuwa imebakia pemben yangu,kufika akaanza kuniongelesha Mara Arusha gari itafika saa ngapi kwa maana alikuwa anataka kuvuka boda aende kwao Kenya na viza yake ilikuwa inaisha saa 6 za usiku wa siku hyo.huyo manzi kwa maelezo yake alikuwa anatokea Zanzibar kwa jamaa yake anafanya kazi kule
so kwavile hajawah kupita Tanzania kwa njia ya barabara akaamua wakati huu apite kwa barabara badala ya ndege ili aione Tanzania vzr.
Tukiwa safarini tukikaribia hedaru na kwavile usiku sikulala vzr mda wote nilikuwa nmelala kwenye Basi nikiwa nmepakata begi la PC miguuni, Mara nasikia kelele kwenye Basi watu wanapiga kelele za taharuki,ile kukurupuka usingizin najikuta nshavuka Kama seat nne kutoka mwisho ili kuwah kushuka kwenye gari Mana watu walijua gar inaungua,na kwevile kila mtu alikuwa anataka kutoka nikasikia kwa nyuma yangu Kuna mdada alikuwa na mtoto mchanga ananipigia kelele nimpishe apite na wakat mbele yangu Kuna watu pia nikaona isiwe tabu nikajisogeza pemben nikafungua dirisha nikaruka chini.baadae kuja kuangalia kumbe haukuwa Moto Bali tairi lilijamu likaw linatoa Moshi na ule Moshi ukaingia ndani ya gar watu wakajua Moto.
Baada ya kukagua gar nakugundua sio motoa kila mtu alirudi kwenye seat yake narudi namkuta yule dada wa kikenya anacheka huku akiniangalia namuuliza why unacheka ànajibu nmependa jinsi ulivyoruka unaonekana ww ni mtu wa mazoez sana story kibao,mpka akaanza kunielezea mpka mambo yake binfsi.
Tulifanikiwaa kuingia Arusha kwenye saa 4 za usiku akaniomba nimtafutie Lodge au hotel nzur alale ili asubuh awah boda namanga,baada ya kumpeleka hotel na kumuaga kuwa naelekea kwangu alinizuia na kuniambia anahitaji kampn yngu kilichofuata ni historia since then ikawa kawaida kila ikifka ijumaa mtoto anatimba chuga tunayaendeleza
Sent using Jamii Forums mobile app