Foxhound
JF-Expert Member
- Dec 15, 2013
- 28,735
- 76,363
Hapa wenye thread sidhani kama watakuelewa!!Hii tabia unasafiri unaenda kituoni wapiga debe wanakupigia unapata kampani na pesa kidogo ya kulegeza mafuta.
Natokea moshi nafika segera nikalamba zangu vichwa vitatu dar mida ya jioni viwili vinaenda moro. Basi ikanilazimu nipite ya mlandizi japo siipendi nikawashushe chalinze waendelee na safari. Baasi tano usiku ndio tunakatiza chalinze kuhamaki wanashuka madume tu kabakia yule dame ndio anaelekea daslam.
Alikua siti ya nyuma nikamwbia pita mbele.
Stori zikaanza mbona unasafiri usiku mtoto wa kike peke yako?
Akaniambia alikua na wenzake gari ilijaa akabakia yeye.
Tukaenda kufika maeneo ya ruvu nasinzia tu ata sijielewi.
Basi kufika mlandizi kiroho safi nikamrudishia nauli yake apande tu gari ingine mi safari ndio imeishia hapo natafuta gesti nilale nishachoka.
Nitaendelea...


