Daah!! Ouyaaa Wee. Pombe sio Poa.
Nina VISA vingi sana yaani sanaa maana sijui hata nielezee kipi niache kipi lakini kuna kimoja hicho sitakisahau Maisha.
Kipindi flani miaka ya nyuma sana nlikua Vijijini, Mkoani huko Kikazi. Sasa mimi ni yule mtu wa kujichanganya sana alafu siwezagi kunywa mwenyewe hata nikienda sehemu naweza kuanza mwenyewe lakini baada ya muda tu nakuwa nimeshazoeana na nliowakuta kisha tunaendelea kuenjoy mdogomdogo.
One day wikiendi hivi Saturday flani hivi imetulia. Nikatoka Ofisini mapema maana ni nusu siku nikaeda home nikaoga fresh nikachange Mkanda nje nikatupia T-Shirt na Jeans nikaenda Road.
Nikaenda kutulia Bar moja kubwa hivi ina Counter 1 barabarani huku nje na ndani mwisho kabisa kuna Counter ya 2 hapo katikati ndiyo watu wanakaa. Mimi nikawa nimetulia counter ya barabarani huku nakula vyedi (Safari) huku nacheki Magari yanapita, mengine yanaingia Bar, na mengine yanatoka napata burdani tosha kabisa.
Mpaka inafika saa 1 nshakula vyedi kama 6 hivi nikaona kama sielewi nikamchombeza Dada wa Counter amuite mtu wa Jikon alafu alivyorudi nikamzingua... Aaf kama vipi anipe K nichachue kama Maskhara vile nlikula Mvua za Matusi pale kejeli na kubinuliwa mdomo alinisema sana na kuniambia mimi namdhalilisha na kumuona Malaya mara yeye hajiuzi maneno mengi yakamtoka; nikaona isiwe kesi nikamwambia Sorry basi kunywa Bia na mimi nipe Bia nimeshakuelewa... Am sorry. Akapoa na mda huo nshamugiza Jamaa Mbavu Portion 2 na Ndizi 4.
Wakati naendelea na chupa zangu akawa anahudumia wateja wengine na wahudumu wanakuja pale counter kuchukua vinywaji lakini ananiangalia kwa hasira alafu anatikisha kichwa kama anasikitika hivi, mimi kwakua nshaharibu nikawa sina habari nampiga kijicho pembe nampotezea tu. Mara muda sio mrefu msosi ukaja mixer kachumbari nini Ndizi zimeremba sahani ya Bati ile pembe kwa pembe nikanawa nikamwambia jamaa amnawishe na yeye aje kula ila aongeze kwanza Bia 2 kama mwanzo mimi na yeye aikua anakunywa Eagle(Ndege) alafu ndiyo tuendelee. Akaniangalia Akatabasam huku anasikitika kama hataki vile.
Wakati tunaendelea kula pale yeye yuko ndani mimi niko nje viti virefu akaniangalia tena ila sasahivi akanikazia macho hivi nikamuuliza vipi umekabwa au akacheka akaniuliza Uko Serious, Kweli!!? Mimi nikatabasamu nikapiga funda kumezea nyama nikamjibu Ndiyo au ulijua nakuzingua!!? Tukaendelea kudonoa menu.
Tukiwa tunakribia kumaliza, nikamwachia sahani akae nayo ndan kule amalizia kabisa, namuona anakenua tu, Jamaa akaja nikanawa nikalipa nikaendelea kula Mma.
Ghafla naona napewa kirisit nikatahamaki vipi tena nikamuangalia na kumuuliza kwani nimekuomba Bill? Akaniambia kwa ishara Fungua usome... Daah!! Nikafungua nakuta ameandika "...Asa ntakupea wapi, tunafunga saa 10 leo." Nikacheka... Nikakichanachana kile kirisitk nkakitupa. Nikatulia. Mule Kaunta akanza kuhaha Mara atoke aingie ananifanyia Ishara ya Mikono akimaanish VIPI SASA!!? Nikamjibu Niongezee Bia alafu uje.
Akaongeza aaf, akanisogelea nikamwambia; "WEWE MTU MZIMA, UNANIULIZAJE MASWALI YA KITOTO HIVO." Nikaendelea na vyupa vyangu nakula monde tu... Akang'ata kidole akaendelea kuwahudumia wengine. Mara akakaa kwenye kiti chake pale ndani akawazaa alafu akatoka kisha akarudi akandika kirisit kingine; "... Ukiona amekuja mhudumu counter humu na mimi nimetoka basi uje ChaKike mwisho kabisa." Akanipa nikakisoma Chap nikamuoneshe Ngumi yenye Dole Gumba nikimaanisha Fresh! nimekusoma.
~ Itaendelea~
Lakini palepale Counter wakati Jamaa wa jikoni ananinawisha baada ya kumaliza kuna Mwamba alikuja akasalimia akakaa juu pale Kaunta nikawa katika kuongea nae na kumdodosa nikagundua ni Wajina yaani wakuitwa jina langu basi katika storystory nikamwambia Dada muongezee Bia ingiza bill yangu; Mwamba alikua anakunywa Plisner(Bia inanukaga Vibaya hii) fresh tukaendelea na story kama Mabest tunaojuana kumbe tumekutana palepale tena night hiyo hiyo.
Huku na huku Mwamba akanipanga kuna Mama Ntilie mmoja bonge wemepanga wakutane hapo ila kama fresh amchek aje na Msaidizi wake ili na mimi nisiwe mnyonge nikamwambia fresh utakua umenifaa aisee!! Tukacheka... Akampandia hewani na ile nokia six button akampanga aje na yule aliyemuhudumia yeye Mchana alivyoenda kula pale. Bonge akakubali. Baada tu ya kumaliza kuongea nae akaanza kumsifia huyo Msaidizi na kuniambia ni yaani Chombo ya Kwenda Aaf hata yeye ndiyo alikua anamtaka sema nini Big kampenda mwenyewe tu kwahiyo wacha aishi nae kwanza. Daah!! Kwa jinsi Mwamba alivyonipanga nikamwambia Dada wa Counter amuongeze Plisner ingine maana amenifurahisha Mwamba akawa ana Bia ya 3 Mpya ya pili iko nusu na ya kwanza keshamaliza.
Naomba niconclude(Nachoka kuandika): Nlijikuta nimekula Madem wote wa3 kizembe sana kwasababu yule wa Kaunta kule Toi nlienda nikapiga kimoja cha Mkwezi kirefu cha kishujaa cha kushika ukuta alafu pale hatukukaa sana walivyokuja wale Bonge na Msaidizi kumbe ni mtu na Shangazi yake tukawapiga bia kadhaa kila mtu tu nikalipa Bill yangu na jamaa akalipa yake tukaondoka Mwamba akatupeleka Kilabuni moja hivi Mashambani sio mbali na pale wanauza Pombe kwenye Makopo ya Chooni yale sema Makubwa na Madogo kama yale ya kuuzia Mbege. Alafu sijui ilikua Pombe gani ile ipo kama Mbege sema inarangj ya Maziwa na Mafuta kwa juu (kama uhudumiwe Maziwa ya Moto yenye Cream alafu yaanze kupoa kwenye Kikombe) ule utando sasa na machicha kidogo kwa juu kama uchafu hivi umechanganyika na mafuta unapuliza unakunywa.
Haina kushea kila mtu na mtuwe, Mwamba akaagiza Kubwa 2 mimi nikatoa Buku 2 na Mwamba akatoa Buku Jero kumbe Lile kopo Dogo ni Buku na lile Kubwa Ni Buku Jero; Mimi nimebigwa na Butwaa lakini sielewi wale wenzangu inaonekaga ndiyo Pigo zao kwasababu Bi Mkubwa( Hawa ni wale waMama wanakuuzia huku wamevaa Kanga/ Vitenge viwili tu kiunoni na kifuani tu. Aaf, wanakuaga aidha Mnene Sana au Mwembamba sana kisha Ni weusiii kama Mkaa sijawi ona Mweupe mimi) alivyoleta nini mixer wanaongea Kilugha mara onja ndiyo unipe mara ya leo mbona kama kali sijui machicha yamefanyaje ivoo yaani. Asa kwasababu pale Bar hawakuwa wamekunywa kivilee kama sisi waliyafakamia yale Mapombe pale mixer yule Bonge akaongezaa na Kopo dogo lile la Buku tukiwa tumekaa upenuni kwenye Benchi hivi tumezunguka duara tukifuatana na Mabenji mengine.
Mwamba alizima pale pale ikabidi mimi niondoke nao wote wawili mpaka kwangu njia nzima tunaimba nyimbo za kilugha mimi nafanya kuitikia tu. Asubuhi, Bonge alitapika Uvunguni sijui hata sina kumbukumbu yaani alitapikaje Uvunguni ambako hakufikiki hata, huku Chumba kizima kinanuka puya la Pombe za Kienyeji aaf yule Shangazi yake na yeye alikua hataki kuondoka... Eti kapapenda ghetto. Mimi sasa ndiyo sifai Kichwa Kinauma, Naskia Kiu kishenzi na huku Mdomoni sasa sijui nlikua najiskiaje ni chefuchefu sio kichefuchefu, machicha kama nimekula Mchanga vile na uso unang'aa kama nimeoga Mafuta. Mimi nimeamka na Boxer na wao kila mmoja ana Pensi lake kubwa lina mifuko yenye zipu huku Vifua wazi hivi nikawatoa hela kidogo wakaondoka, Siwajui na wao hawanijui mpka leo maana walitaka wapike Chai na mimi nlikua sina Chombo chochote ndani basi walivyotoka saa 5 hiyo kweupe kabisa Majirani na wapangaji wengine kama vile waliambiana Wageni rasmi wanatoka wakawa wamejipanga nje wawaone... Daah!! Aibu ile sitaisahau kamwe.