Heshima kwenu.
Namfananisha Mwewe na Shetani. Naam mwewe huyu anaetubia vifaranga majumbani mwetu. Hana huruma na kifaranga akikiona. Anajicho kali sana awapo Juu lenye kuona mpaka mbali. Kucha zake anatumia kuralua na kushika/kubebea mboga zake. Twende pamoja
Namfananisha kuku . Na mama mlezi yule tetea wa nyumbani kwako na Mama ni kanisa ama sinagogi( yaani Msikiti) ama mahari ambapo watu wanakusanyana ili wapokee vitu vya ki Mungu.
Isaya 42:18 - Sikilizeni, enyi viziwi; tazameni, enyi vipofu, mpate kuona.
Kuku anapoatamia mayai ni sawa na nyumba za ibada zinavopaswa kuwaatamia hao watu humu katika hali zote walizonazo kwa kuhakikisha hawaharibikiwi. Vinapotoka vifaranga huvikumbatia kuvikinga na barid na mvua na hali zote za hatari Akiwapo mwewe.
Mpendwa ni hivo hivo hata ktk ulimwengu ule tuuendeao. Labda wengine hawajui niwakumbushe hapa tunapita. Tutakufa kimwili tutahama ulimwengu huu.
Kuku asipowalinda vifaranga dhidi ya mwewe si mzazi mzuri maana wataisha wote kwa kuwa chakula cha mwewe na kuwajeruhi pia. Mwewe hachoki ndivyo inavyopaswa kuwa ktk nyumba hizi za ibada. Viongozi wetu wamekuwa hawana wivu na waumini wao, hawana uchungu hata mmoja aondokapo kwenda nje kulanda landa, hawana wivu hata mmoja aendapo kutafuta uzima kwa Waganga wa kienyeji, hawana wivu mmoja akienda kwenye Uasherati na uzinzi tena kwa kutokupenda.
Na mengine mengi hawa wazazi wa kiroho si wazazi wazuri maana wameshindwa kuwanusuru watoto wao ktk matendo machafu ambayo ni ya kishetani na yamewachukua fahama zao. Wamemkataa Mungu hawamtaki, na hawatak mafundisho ya Mungu. Na matunda yake ni haya hasa kubwa MAWAZO MABAYA.
Warumi 1:28 - Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
Mungu aliyagundua haya maana Yeye hutazama mbali Akijua kwamba hawa wazazi ndo Mwewe wenyewe sasa ki roho ila kimwil ni Kuku

akaja ulimwenguni. Wengine husema ni Mtume tu(SAWA) akachagua timu aka ipa mafundisho wote twajua kinachoendelea. Mungu akawacha mashetani akawa anachomoa mmoja mmoja nikiwemo na wewe utachomolewa tu.
Wengine wakastuka watu wanaisha wakanzisha Kalestmatic sijui

kuwapumbaza hekima hizo ni za shetan maana ni mwerevu. Wengine wakaongeza ukali kama kutengwa na vingine.Baba usaidie taifa hili ikiwa ni mapenzi yako kwao.Ili ya kwamba-
2 Timotheo 2:26 - wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake.
Ni sawa kwa Mlokole halisi kutukanwa kila aina ya tusi sbb Yeye anakesha. Kwa ajir ya kumwombea anaemtukana. Yule Haoni sbb shetan yupo ndani yake anamtumia kutukana ili kumkatisha tamaa. Mtoto wa Nyoka ni nyoka kwann mtoto wa Mungu asiwe ni miungu midogo ni yasemayo ni hakika na kweli wala sijitaji Yeyote anishuhudie bali Mungu.
Isaya 54:1 - Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema Bwana.









Ni Neno Mungu anawaambia wale aliowatoa ktk mikono ya shetani. Maana wanaongezeka kwa manati sio wengi lakini Wameolewa na Yesu mwenyewe. Manake wamefunga agano na Mungu je watoto wa aliyeachwa yaan hao ambao wameshindwa kuwalinda watoto wao. Hayo madhehebu ambayo na wachawi wana Sali humu, na waasherati na wazinzi sio shida lakini wanafurahia hali hiyo na viongozi wao baadhi yao wanashirikiana kuhakikisha hakuna kuoa ili kutoruhusu uwepo wa Mungu ndan ya malango yao Neno la Mungu linasema watoto wao wao ni wengi.
Najaribu kukupa picha kidogo sana ili uone kwamba Sio wewe ambae unapenda kutenda haya bali ni shetani ambae bado hujamuona. Macho yako yatafunguliwa upate kuona kidogo kidogo. Ama yasifunguliwe maana Mungu watu wengine ameshawakataa.
Nakukumbusha umuhimu wa Toba mara kwa mara huko ndipo utaona Nuru. Huu Ndio upendo yakwamba tukumbushane pia tunapoziendea njia mbaya basa na njia nzuri zipo. Ashupazae shingo huvunjika.