Ulipofikia Ujenzi wa daraja la Kigongo - Busisi

kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu inaendelea na ujenzi wa miradi ya kimkakati iloachwa na awamu ya sita ikiwemo ujenzi wa Daraja la Magufuli lililopo maeneo ya Kigongo Busisi mkoani Mwanza.

Ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi umefika 67% na linatarajiwa kukamilika February mwaka 2024. Daraja hilo lina urefu wa kilomita 3.2 na barabara unganishi za kilomita 1.66.

Ujenzi wa miradi ya madaraja ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26).

Ilani hiyo katika ukurasa wake wa 67 na 68 inabainisha miradi ya madaraja iliyokamilika kujengwa na ile inayoendelea kujengwa wakati Mpango wa Maendeleo (Uk 31) ukieleza kuhusu kukamilika kwa ujenzi wa madaraja makubwa 12.

Mpango huo wa Maendeleo pia unatambua kuendelea kwa shughuli za ujenzi wa madaraja kadhaa likiwemo la Kigongo–Busisi, Sukuma, Simiyu, Mkenda, Mtera, Godegode, Malagarasi Chini na Ugalla.

1678363096056.png
 
Back
Top Bottom