Ulipigika miaka mingapi mpaka kupata Ajira ya Kwanza baada ya Chuo?

Ulipigika miaka mingapi mpaka kupata Ajira ya Kwanza baada ya Chuo?

...leo tupeane faraja baada ya kuchungulia nje na kukuta kuna kundi kubwa la wahitimu wa certificate, diploma, degree, masters wanaongezeka Tu Ka njugu mtaani!
Mie baada ya kumaliza Chuo nilipigika haswa! Yes, enzi zile tunavaa suruali za bugaa na mashati ya kung'aa na tai zenye mistari mistari Ka wachungaji wa kilokole au wasabato! Nguo zilipauka mpk intavyuu ukiitwa unaona aibu!
Baada ya msoto wa miaka miwili nikapata Ajira Kwa muhindi, mshahara 195,000/= o'clock! Yes! Niliiona ya maana japo msoto wa kitaa nishaanza kuuzoea as niliamua kufundisha tuisheni, huku nikimeki pesa mingi likizo za madent! Kulima nililima matikiti, cha Moto nilikiona! Ukiingia na overexpectation kwenye kilimo utaimba nyimbo zote za Remy Ongala!
Kuku nilifuga nikaishia Kula mayai japo I made something! At the end nikapata Marketing officer Kwa muhindi. Simsemei vibaya, he was good compared to others!
Msoto wa Ajira unaendelea kuwa mkali kadili maelfu ya wahitimu inavyoongezeka Kada zote! Ni bomu! Ni bomu!
Hakuna cha afya, kilimo, uchumi, engineering Mambo ni magumu!
Ushauri: Jifunze kutafuta pesa Kwa njia mbadala/ujasiliamali mapema Sana ili elimu ikikudiscourage uwe na mahali pa kulinda utu wako la sivyo utamaliza Series, CDs na magazeti sebuleni Kwa shemejio!!!
Karibuni wahitimu wa vyuo kitaa...huku hata wa degree ana endesha bodaboda na kuchoma chips!!!
, 😁😁 wanangu niliomaliza nao udsm miaka mitatu iliyopita nimekutana nao juzi wametundika suruali na socs mabegani wanauza kariakoo, wengine wanauza maji ya marehem kandoro mtaani.
 
Msoto baada ya kumaliza chuo usikie hivyo hivyo ni balaa kubwa.

Ukisikiliza wimbo wa Nash MC uitwao maisha baada ya chuo utaelewa zaidi.
Mkuu kama iyo ngoma naitafuta sana itakuwa poa kama utanipa.
 
Nilimaliza chuo miaka 10 iliyopita, mwanzo nlikua na mindset kwamba ipo siku ntaitwa boss ntavaa suti na tai ofisin. Nikazunguka sana na bahasha mpaka siku mzee ananiita ananiuliza "hivi hujawahi kuwaza mengine kwenye maisha yako zaid ya kuajiriwa" nayakumbuka sana yale maneno. Ever since nlituliza kichwa nashukuru mungu hyo mindset haipo tena na naitwa boss ila sivai suti wala tai. Nafurah Kuna watu mwisho wa mwezi mambo yao hayaend bila mimi. Asante mungu, asante baba yangu mzazi.
 
Nilimaliza chuo miaka 10 iliyopita, mwanzo nlikua na mindset kwamba ipo siku ntaitwa boss ntavaa suti na tai ofisin. Nikazunguka sana na bahasha mpaka siku mzee ananiita ananiuliza "hivi hujawahi kuwaza mengine kwenye maisha yako zaid ya kuajiriwa" nayakumbuka sana yale maneno. Ever since nlituliza kichwa nashukuru mungu hyo mindset haipo tena na naitwa boss ila sivai suti wala tai. Nafurah Kuna watu mwisho wa mwezi mambo yao hayaend bila mimi. Asante mungu, asante baba yangu mzazi.
Safi sana mkuu
 
Uoga wa kuthubutu na kulinda personality vinawaponza graduates wengi. Binafsi nifanya kazi ya kiupuuzi kwa macho ya wengi ila hii biashara yangu Ina miezi 3, nilianza na 150k mwezi wa tano sasa mtaji ni milion 2.5 hapo nakula na kulipa Kofi ya nyumba humohumo, vocha huwa naweka kifurushi cha 20k.

Utaniambia kuajiriwa vipi nikuelewe!
Kazi gani mkuu nipeane idea nami nianze
 
Kumaliza 2011. Kuanza msoto hadi 2015 ajira ndo inapatikana tena kwa mbinde yenye ushindani mkali sanaaaa nikatusua sasa shidah zote nimezisahau sitaki wanangu wawe na mawazo kama ya kwangu kabisa kqani nilikuwa nawaza kuajiriwa all time nimeanzisha miradi ya ufugaji , na kilimo cha bustani nawaelekeza kila nachokifanya nashujuru wamejifunza na wanafanya wenyewe na pesa wanapata wanajinunulia viatu,soksi,madaftari na mabegi ya shule wenyewe wapo darasa mkubwa darasa la 6 na mdogo darasa 4 .wasichana wote. Naona wameanza kujifunza kitu fulani.
 
Mimi nimemaliza chuo mwezi uliopita. msoto nimeanza kuuona, ee Mungu nitie nguvu.

Mkuu tatizo unakuwa na over ambition ambazo we mwenyewe huwezi tekeleza ..mfano matokeo hajatoka nafikiri ila umeshaanza chenga mentality kazi ni ngumu kupata sijui nini ,we just kaa tulia fanya mambo yako amini muda ni mwamuzi sahihi kufanikiwa kupo tena ikiwa bado uko 20s ujachelewa

Yaani nashangaa vijana saizi wanahaingika na internship wakati ata matokeo hayatoka, unakuta mtu analaumu kwa nini sipati instajabisha
 
Back
Top Bottom