Ulipigika miaka mingapi mpaka kupata Ajira ya Kwanza baada ya Chuo?

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
7,312
10,493
...leo tupeane faraja baada ya kuchungulia nje na kukuta kuna kundi kubwa la wahitimu wa certificate, diploma, degree, masters wanaongezeka Tu Ka njugu mtaani!

Mie baada ya kumaliza Chuo nilipigika haswa! Yes, enzi zile tunavaa suruali za bugaa na mashati ya kung'aa na tai zenye mistari mistari Ka wachungaji wa kilokole au wasabato! Nguo zilipauka mpk intavyuu ukiitwa unaona aibu!

Baada ya msoto wa miaka miwili nikapata Ajira Kwa muhindi, mshahara 195,000/= o'clock! Yes! Niliiona ya maana japo msoto wa kitaa nishaanza kuuzoea as niliamua kufundisha tuisheni, huku nikimeki pesa mingi likizo za madent! Kulima nililima matikiti, cha Moto nilikiona! Ukiingia na overexpectation kwenye kilimo utaimba nyimbo zote za Remy Ongala!

Kuku nilifuga nikaishia Kula mayai japo I made something! At the end nikapata Marketing officer Kwa muhindi. Simsemei vibaya, he was good compared to others!

Msoto wa Ajira unaendelea kuwa mkali kadili maelfu ya wahitimu inavyoongezeka Kada zote! Ni bomu! Ni bomu!

Hakuna cha afya, kilimo, uchumi, engineering Mambo ni magumu!

Ushauri: Jifunze kutafuta pesa Kwa njia mbadala/ujasiliamali mapema Sana ili elimu ikikudiscourage uwe na mahali pa kulinda utu wako la sivyo utamaliza Series, CDs na magazeti sebuleni Kwa shemejio!!!

Karibuni wahitimu wa vyuo kitaa...huku hata wa degree ana endesha bodaboda na kuchoma chips!!!
 
Tofauti na nilivyokuwa natarajia kuwa nitasota sana, nilimaliza mwezi na wiki mbili hivi

Nilimaliza chuo Julai, kisha Agosti nina kazi tayari, japo haikua dream job, niliifanya kwa mwaka mmoja na nusu nikaajiriwa kwingine, baada ya mwaka na nusu hivi nikaacha tena nikajiajiri
Sema silaumu waliochelewa kupata kazi au kujiajiri kuwa ni wazembe, maana upande wangu ulichangiwa kwa bahati sana

Kuna ndugu nilimaliza nao chuo nilikuwa nawasikitikia sana nilipokuwa nawaona

Huko mbele mambo yanazidi kuwa magumu zaidi maana ndio 'wasomi' wengi wanazidi kuzalishwa

Mimi wanangu najipanga angalau wakimaliza elimu yao waje kufanya kazi kwenye kampuni ya familia, sio kupitia nilikopitia japo nilibahatika
 
Uoga wa kuthubutu na kulinda personality vinawaponza graduates wengi. Binafsi nifanya kazi ya kiupuuzi kwa macho ya wengi ila hii biashara yangu Ina miezi 3, nilianza na 150k mwezi wa tano sasa mtaji ni milion 2.5 hapo nakula na kulipa Kofi ya nyumba humohumo, vocha huwa naweka kifurushi cha 20k.

Utaniambia kuajiriwa vipi nikuelewe!
 
Mishe gan hyo unafanya

Mimi binafsi sijawahi kukaa hata mwezi moja bila ajira, kwasababu nilijifunza jambo kujiajiri na discipline ya kazi, na tegeneza fursa mbadala incase ajira kuu ikipotea.....nashangaa watu wanao kosa kazi wakati wamesoma, kubali au kataa nchi yetu Tznia imeja fursa za kazi tere kinachokosekana ni entrepreneur ship skills determination, work discipline flexibility and trustworthy.
 
nchi yetu Tznia imeja fursa za kazi tere kinachokosekana ni entrepreneur ship skills determination, work discipline flexibility and trustworthy.
Ni rahisi sana kuandika nadharia kuliko ku-experience reality!

Hlf lazima uelewe kila mmoja ana ukurasa wake wa maisha hivyo background za wengine kuzibadilisha ni ngumu kidgo hadi awe boosted na mfumo wake wa elimu!
 
Watu ni rahisi sana kuandika sababu walikuwa na fursa na rasilimali za kuvuna hizo fursa, wanafikiri dunia yao ndio dunia ya kila mtu

Japo sikusota kupata ajira na kwa sasa hivi sihitaji tena ajira, siwezi kumlaumuasiye na kazi, maana mafanikio yangu yamechangiwa na luck kwa asilimia kubwa japo niliweka juhudi pia
 
Ni rahisi sana kuandika nadharia kuliko ku-experience reality!

Hlf lazima uelewe kila mmoja ana ukurasa wake wa maisha hivyo background za wengine kuzibadilisha ni ngumu kidgo hadi awe boosted na mfumo wake wa elimu!
Wengi tuna background za wazazi wetu kuwa waajiriwa na ujasiliamali ulikuwa Kama kazi za wengine, so kuajiriwa ndo ilikwa ndani ya minds zetu. Real kuibadili hii ni kazi haswa!
 
Tofauti na nilivyokuwa natarajia kuwa nitasota sana, nilimaliza mwezi na wiki mbili hivi

Nilimaliza chuo Julai, kisha Agosti nina kazi tayari, japo haikua dream job, niliifanya kwa mwaka mmoja na nusu nikaajiriwa kwingine, baada ya mwaka na nusu hivi nikaacha tena nikajiajiri
Sema silaumu waliochelewa kupata kazi au kujiajiri kuwa ni wazembe, maana upande wangu ulichangiwa kwa bahati sana

Kuna ndugu nilimaliza nao chuo nilikuwa nawasikitikia sana nilipokuwa nawaona

Huko mbele mambo yanazidi kuwa magumu zaidi maana ndio 'wasomi' wengi wanazidi kuzalishwa

Mimi wanangu najipanga angalau wakimaliza elimu yao waje kufanya kazi kwenye kampuni ya familia, sio kupitia nilikopitia japo nilibahatika
Nimekupata Sana dada. Real ni busara kuwandaa vijana kujiajiri tng mapema. Tunapoelekea sio!
 
Back
Top Bottom