Ulinzi wa Ziada kwa Dr Ulimboka. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulinzi wa Ziada kwa Dr Ulimboka.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jun 29, 2012.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni bora kwa sasa kwa kila anaehitaji kuingia hapo kwenye chumba cha mgonjwa NI LAZIMA AWE NA KITAMBULISHO MAALUM NA DHARURA ILIYOMFANYA ATAKE KUMUONA MGONJWA ,ICU si ruhusa mgonjwa kutembelewa ,yaani inakuwa NO ENTRY ,Pia mtembeleaji huyo akubali kusachiwa ,asiruhusiwe kuingia na chochote kile ,silaha simu au pochi vyote akabidhi sehemu maalumu iliyo na dhamana kwa kukaguliwa vilivyo.

  Na jambo hilo liwe kwa yeyote yule bila ya kujali Cheo Chake.
   
 2. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Sasa unatoa ushauri au ndiyo unapitisha sheria kabisa?
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  Zomba, u can pass for a witch, u know that?
   
 4. T

  Topical JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Tunataka rais dikteta kuliko dhaifu
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,318
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  Dikteta kwa maana halisia ya mambo makuu ya nchi yetu EPA,Rada,Pesa ya Uswisi,Kagoda,Dowans si wazalendo wanaotetea maslahi ya wanyonge!unataka kuua mtu anaedai CT Scan hospitalini?anaetaka aspirin ziletwe hospitalini!????huo ni udhaifu wa udikteta!
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Nenda zako subiri kigwagallah afike dsm Leo dingi yako azimishwe
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu changia jf umri wako hapa jamvini ni mkubwa sana hata sisi makinda tujifunze kutoka kwako
   
 8. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Huyu Zomba ndilo lile jini linaloitwa Maimuna!
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sasa hapa nafanya nini kama si kuchangia?
   
 10. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Ee mwenye enzi Mungu hebu muangalie huyu mtu unaempa pumzi ya bure ni kwa namna gani anavyoitumia vibaya,wajua cha kumlipia kulingana na maneno yake na vitendo vyake
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Watu wanaweza kupita na kaunga tu ndani ya kipochi na mlio ndani ya chumba mkapoteza umri baada ya siku au masaa machache.kuna Kaunga kalimwagwa ndani ya ndege ya Uingereza na majasusi wa Kirusi wakati kuna abiria alikuwa ndio target.
   
 12. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kupitia m-pesa mkuu
   
 13. b

  betty marandu JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 711
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 80
  Zomba hata kama humwogopi Mungu wala binadamu wenzio kumbuka kuna usemi usemao"mwenzio akinyolewa zako tia maji"kumbuka yalompata Dr.yaweza kukupata au hata zaidi.Au mwenzetu unaijua kesho yako?
   
 14. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Katika kipindi kifupi tumeshuhudia mengi, baadhi ya viongozi kutishiwa na wengine kuugua magonjwa ya ajabu. Pia wabunge/madiwani wamekatwa mapanga, watu wameuawa. Leo hii Ulimboka ametekwa na Kupigwa na hebu angalia pia kisa hiki:

  Dear friends

  Leo nimeona ni vyema nika-share nanyi kisa hiki cha kutekwa mfanyakazi mwenzetu ambaye ni cashier siku ya jumatano jioni wiki iliyopita.

  Ni kama movie lakini ni ukweli, cashier wetu aliomba ruhusa siku hiyo ya tukio aende kwenye mkutano wa wasabato uliokuwa uliendelea viwanja vya biafra. Yeye pia ni msabato aliyeishika dini ya Sabato haswa, kwa hiyo aliondoka saa kumi kamili badala ya saa kumi na moja

  Baada ya dakika 40 tulianza kupokea sms zinazosema mwenye namba xxx amepata ajali na kufa papo hapo na kwa taarifa zaidi twende muhimbili hospital. Baada ya kutazama hiyo namba xxx ilikuwa ni ya cashier wetu. Tulijaribu kuipiga iliita tu bila kupokelewa, na pia tulipiga namba iliyotutumia sms iliita bila majibu. Ilipofika saa kumi na moja tuliamua kuelekea muhimbili, ma baada ya kufika pale emergence tukaambiwa tuelekee chumba cha kuhifadhia maiti. Tulioneshwa mwili wa mtu aliyepata ajali lakini haukuwa wa cashier wetu, tukawatuma wenzetu waende hospitali zote lakini hapakuwa na taarifa zake

  Baada ya kuzunguka bila mafanikio tulitoa taarifa makao makuu ya usalama barabarani na baada ya dk kumi wakatwambia kuwa hakuna taarifa za ajali mbaya iliyotokea jioni hiyo. Hatua iliyofuata ilikuwa ni kutoa taarifa polisi juu ya tulio hilo na ndipo waliposema kwa kuwa ni mtu mzima tusubiri hadi siku inayofuata. Wakati huo huo ndugu zake pamoja na wafanyakazi wenzetu walikuwa pamoja wakiendelea na jitihada za kumtafuta hadi saa sita usiku. Kilichokuwa kinatia wasiwasi zaidi ile namba iliendelea kutumia sms namba takribani zote zilizokuwa kwenye phonebook yake na ndugu zake hawakuwahi kuona ndugu yao akichelewa kiasi hicho.

  Ilipotimu mida kama ya saa sita na nusu walisikia mtu akigonga mlango, alikuwa kaumizwa na amejaa matope, hakuwa na uwezo wa kuzungumza sana, ilibidi wampeleke kituo cha polisi na baada ya muda hospitali ya mwananyamala.

  Alipopata nguvu alianza kuwasimulia nduguze kilichotokea. Alipotoka ofisini alikwenda moja kwa moja kwenye kituo cha daladala cha karakana, pale kituoni walikuwa abiria wawili yaani yeye na mama mmoja. Baada ya dk chache ilikuja coaster iliyoandikwa mbele Kawe na ilikuwa na tinted nyeusi, yule mama hakupanda sababu alikuwa anaelekea posta ila yeye alipanda. Ndani ya gari kulikuwa na watu watatu pamoja na dereva, wawili wakiwa wamekaa nyuma na mmoja akiwa amekaa karibu na driver. Gari hiyo hiyo ilikuwa ni mpya, mmoja wa abiria alimumba simu cashier apige simu moja kwa jamaa yake maana alidai kuwa simu yake illiishiwa charge na walikuwa wametoka mtwara kupeleka maiti, alimuuliza cashier umri wake na kama ameoa na anafanya kazi wapi, cashier akamjibu hajaoa na hana kazi pia ana miaka 32. Walipofika Tazara hawakutaka kupakia abiria yoyote na walikuwa wote wamevaa miwani myeusi, na ndipo akaanza kuingiwa na mashaka akaomba ashuke, wao wakamwambia watapita biafra na hawana mpango wa kusanya kwa kuwa hata yeye walimpa lifti tu. Gari ilipokaribia taa za buguruni akainuka ili ashuke, jamaa wale wa nyuma wakamkalisha chini kwa nguvu, na sio kwenye viti yaani chini kabisa. Mmoja wao akafunga kitambaa cheusi kwenye macho na mikono ikafungwa kwa nyuma na mipira, baada ya muda akasikia kama wamempulizia perfume. Akihisi fahamu kumtoka polepole na neno lamwisho analokumbuka alisikia kuwa waelekee misitu ya Kibaha wakamalize kazi. Kilichomwamsha ni kofi zito alilopigwa na kusukumwa hadi nje ya gari. Alianza kulia na kuwasihi wasimdhuru, wakaanza kumrusha kichurachura huku wakimkanyaga. Walikuwa wameshamfungua kitambaa machoni na waliacha gari umbali kama wa dk kumi na lilikuwa ni pori zito na giza, wao walivaa vitu usoni na walikuwa wamevaa gloves. Wakamwekea simu yake mfukoni wakiwa wametoa simcard, walichomwambia wanachohitaji ni sehemu zake za siri na sio kitu kingine. Mmoja wao akaambiwa alete kisu kikali wanachokitumia, na walipompigia boss wao akawasisitiza nyeti zinazotakiwa lazma ziwe za mtu wa miaka 40 na kuendelea. Mwenzao mmoja akasema cashier alisema alikuwa na miaka 32, baada ya kumkagua wakakuta card yake inaonyesha kazaliwa mwaka 1979. Kulingana na yeye asemavyo ndicho kilichomwokoa ila waliendelea kumkung'uta kwa hasira. Wakamrudisha kwenye gari na baada ya mwendo wakampakia kwenye gari nyingine ndogo iliyokuwa na watu wawili ambao walimchukua na kumtelekeza maeneo ya sayansi. Hawakuchukua kitu hata kimoja wala kumwambia lolote,siku iliyofuata alipelekwa agakhan kwa uchunguzi zaidi na kwa sasa anaendelea vzr.

  Kwa ufupi ni hayo, ukweli mwenyezi Mungu atulinde na tumwombe pia abadilishe mioyo ya watu ambayo imekuwa migumu mno kwa ajili ya kupata vyeo na utajiri wa haraka


  Hili pia limetokea karibuni; wewe unathubutu kutamka maneno kama haya hapa? Kumbuka kesho zamu yako na wewe pia na hata yeye akifa hatabeba kifo chako maana na wewe utakufa siku yako tofauti.
   
 15. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  You are pathetic for not considering the majority because of your personel cormfort.
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Na yale yanayowapata wagonjwa wote wanaohaha bila kutibiwa na wengine kupoteza maisha, wewe hayawezi kukupata?
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,801
  Trophy Points: 280
  I can't believe what you have written zomba! Ina maana una support kitu alichofanyiwa? Kwa mamlaka gani na kwasababu gani? Huoni tutatengeneza magenge ya wahuni kama kule nigeria halafu nchi itakuwa ngumu kuendesheka? Mbona sioni huyu jamaa kama ana tishio lolote sasa watu wanatishika na nini?
  Well, mengine tunamuachia Mwenyezi Mungu, ila malipo hapa hapa duniani.
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,801
  Trophy Points: 280
  Kwanini tunataka kutatua tatizo moja kwa kutengeneza lingine? I have never seen such a wisdom anywhere in this world! Tatizo hili la pili limezaa makubwa kuliko lile la kwanza...tumekosa watu wenye busara somewhere....duuh
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Waliomfanyia hivyo wana sababu nzuri sana.
  Kuna mwanamke wa miaka 23 likuwa ajifunguwe kwa opereshen, dokta aliyekuwepo akasema mpelekeni bungeni akapasuliwe, hapa atazaa mwenyewe tu, matokeo yeye na mtoto wamepoteza maisha. Inasikitisha sana.
   
 20. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Uko sahihi Zomba, ila umesahau jambo moja. Ungeandika "Kwani Ulimboka bado mzima?

  Huyu itakuwa ni robot. Tumemvunja Mbavu, Meno. Miguu, Taya, Tumbo, Makalio, tumemvuta na gari (ina maana michubuko mwili mzima) ili apate maumivu mwili mzima, tukamtupa. Yaani kumbe bado yuko hai?."

  Hii ingesaidia kutimiza azma yako ya kuonyesha unyama uliojaaliwa.
   
Loading...