Nawasalimu katika jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania!
Wapendwa tumekua tukiona kwa macho yetu, kwamba Mh Rais Samia ana walinzi wenye mabunduki mazito mazito pindi anapokua kwenye tukio au sehemu yoyote hapa Nyumbani Tanzania!
Wale wana usalama ni wenye miili mikubwa,warefu na wamekula gwanda la kijeshi na pia zile bunduki sijui ni aina gani,maana hua ni heavy machines!
Sasa Jana Mh Rais Samia kaingia Marekani, Nchi ya watu watukutu,wanatembea na bunduki zao mifukoni na wananunua bunduki madukani kama sisi tunavyonunua unga wa ugali kwa Mpemba au kwa Mangi!
Sasa Jana sijawaona kabisa wale wanausalama wetu, Jana kina Mange Kimambi walikua wanamsogelea Mh Rais wetu,hadi yule mpambe wa Mh Rais,akawa na kazi yakumzuia Mange Kimambi,sijui alikua anataka kumpa zawadi gani Mh Rais!
Sasa nauliza,huu Ulinzi mzito wa Mh Rais wetu,hua ni wa hapa kwetu, Tanzania pekee? Mbona wao wakija hapa kwetu hua wanaweka Ulinzi mzito hadi kupanda kwenye paa letu la Ikulu? Airport yetu wanaichukua kwa mda wote ambao Rais wao yupo?? Je tunawaamini sana kwa ulinzi wa kiongozi wetu,ila wao hawatuamini kwa ulinzi wa kiongozi wao??