Ulinzi wa Rais Samia Marekani upoje?

Mangungu

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
2,391
3,014
Nawasalimu katika jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania!

Wapendwa tumekua tukiona kwa macho yetu, kwamba Mh Rais Samia ana walinzi wenye mabunduki mazito mazito pindi anapokua kwenye tukio au sehemu yoyote hapa Nyumbani Tanzania!

Wale wana usalama ni wenye miili mikubwa,warefu na wamekula gwanda la kijeshi na pia zile bunduki sijui ni aina gani,maana hua ni heavy machines!

Sasa Jana Mh Rais Samia kaingia Marekani, Nchi ya watu watukutu,wanatembea na bunduki zao mifukoni na wananunua bunduki madukani kama sisi tunavyonunua unga wa ugali kwa Mpemba au kwa Mangi!

Sasa Jana sijawaona kabisa wale wanausalama wetu, Jana kina Mange Kimambi walikua wanamsogelea Mh Rais wetu,hadi yule mpambe wa Mh Rais,akawa na kazi yakumzuia Mange Kimambi,sijui alikua anataka kumpa zawadi gani Mh Rais!

Sasa nauliza,huu Ulinzi mzito wa Mh Rais wetu,hua ni wa hapa kwetu, Tanzania pekee? Mbona wao wakija hapa kwetu hua wanaweka Ulinzi mzito hadi kupanda kwenye paa letu la Ikulu? Airport yetu wanaichukua kwa mda wote ambao Rais wao yupo?? Je tunawaamini sana kwa ulinzi wa kiongozi wetu,ila wao hawatuamini kwa ulinzi wa kiongozi wao??
 
Wale wanaitwa special weapon and tactics unit (Combat bakabaka) ni kikosi maalamu ndani ya kikosi cha ulinzi wa raisi kwa ajili ya kuboresha ulizi wa rais.

Na kwa ufupi ni kwamba kila nchi zina utaratibu wake wa ulinzi, hata kwa mama pia alipotua US kuna special security anakuwa amepangiwa na UN tena wale ndio wanaume kwelikweli achana na hawa wavulana wetu.

Ila nikirudi kwenye ile clip ya jana nimeumia mno kumuona mmoja wa walinzi wa Rais anaacha jukumu lake la ulinzi na kushika simu ya Mange kimambi (malaya wa kisiasa) na kuruhusu kupiga nae picha.

Tukifuata protokali za ulinzi hakupaswa kufanya vile kabisa, amevunja miiko ya ulinzi.
 
Acha roho mbaya. Kwani mlinzi wa rais sio binadamu hadi ashindwe kuchukua simu na kumpiga Mange na rais? Acheni kuwatukuza watu kama vile hawajazaliwa. Huu utukufu ni mentality tu za kidunia lakini walinzi wa rais ni watu kama wajomba zako tu huko kijijini.
 
Acha roho mbaya. Kwani mlinzi wa rais sio binadamu hadi ashindwe kuchukua simu na kumpiga Mange na rais? Acheni kuwatukuza watu kama vile hawajazaliwa. Huu utukufu ni mentality tu za kidunia lakini walinzi wa rais ni watu kama wajomba zako tu huko kijijini.
Unafahamu majukumu yake? Kulikuwa na ulazima gani wa yeye kupokea simu na kuipitisha kwa msaidizi mwingine what if ile simu ilikuwa imeungwa na kilipuzi chochote na madhara yakitokea nani wa kulaumiwa?

Walinzi hutakiwa kuwa FLEXIBLE hawapaswi kuishi kwa mazoea hata siku moja kwa kitendo kile cha jana wanadhidi kuuthibitishia umma kuwa hawako serious na majukumu yao.
 
Nchi ya watu watukutu,wanatembea na bunduki zao mifukoni na wananunua bunduki madukani kama sisi tunavyonunua unga wa ugali kwa Mpemba au kwa Mangi!

Tz ngumu
 
Kipindi cha vikao vya UMOJA WA MATAIFA(UNGA)...UN imewekeza ulinzi mkubwa sana...mnooo kuyazunguka maeneo yote wanayopita marais wa dunia.

#SiempreJMT
 
Unafahamu majukumu yake? Kulikuwa na ulazima gani wa yeye kupokea simu na kuipitisha kwa msaidizi mwingine what if ile simu ilikuwa imeungwa na kilipuzi chochote na madhara yakitokea nani wa kulaumiwa?..
Na yule akirudi tz anapangiwa ulinzi wa mkuu wa wilaya. Ameshindwa kujikontroo
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom