Ulinganisho wa Ofisi za Kaunti ya Machakos (Ksh350 milioni) dhidi ya Ikulu mpya ya Tanzania ya (Ksh175 milioni)

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
Mnamo mwaka 2020 Gavana wa Machakos Dkt. Alfred Mutua alizindua makao makuu mapya ya kaunti hiyo. Jengo hilo jipya, ambalo linafananishwa na Ikulu ya Marekani - lilifunguliwa rasmi Jumatano, Mei 6, 2020 baada ya ujenzi wake kukamilika kwa gharama ya kiasi cha fedha Ksh. 350 milioni ambazo ni zaidi ya Bilioni 6 za Tanzania.

White House Machakos.jpg

Mnamo tarehe 20 Mei, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliongoza uzinduzi rasmi wa Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma ambapo Rais na watumishi wengine watahamia katika Ikulu hiyo. Ujenzi wa Ikulu hiyo umegharimu zaidi kiasi cha fedha Ksh. 175 milioni ambazo ni zaidi ya Bilioni 3 za Tanzania.

Ikulu ya Serikali iliyoko Dar es Salaam ilijengwa na wakoloni, hata hivyo, Ikulu ya Chamwino inajivunia ujuzi na nguvu kazi kutoka kwa wenyeji kwa kupitia Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania (JKT). Ujenzi huo kutekelezwa na JKT kunaelezwa kusababisha kupungua kwa gharama za ujenzi huo.

Ikulu Chamwino 2.jpg
 
Aibu ofisi ya kaunti kenya ni sawa na ikulu ya chamwino.

Nilishangaa ikulu ya chamwino imejipanga kama mdadada za nyumba za kupanga.


Ikulu pia iko to exposed aiseee, Sijui wana mpango gani , sioni silaha juu ya dari la ikulu wakishambuliwa je?

Ni rahisi kwa mtu kuteka ndege na kwenda kuibamiza hapo ikulu huku chamia akiwa anakoroma usingizi
 
Hahah kwani hizi milwngo ni kama majumba za kukodisha!!
Stares ziko nje kienyeji style!!!!
Ata sikuwa nmenotice.
Machakos one is better.modern design too.
Finishing too Iko juu.
 
Una ushahidi wa hizi data? Kuwa Ikulu nimejengwa kwa 3 bilioni Tshs? Huu ni uwongo maana hata majengo ya hospitali za kawaida ni zaidi ya hiyo pesa!

What is the true cost of this construction?
 
Sasa hiyo Machakos ndiyo unajaribu kuringanisha na State house ya Chamwino?
Hiyo ya Machakosi si ni kama Magufuli Hostels zilizopo UDSM?
 
Hivi aliebuni hii ikulu ya chamwino alikua ni nani?🤔 Hovyo kabisa yani utadhani ni nyumba za kupangisha za mtaani tuu
 
Utofauti upo ni hivi

Makao ya gavana ni Tsh 300 milion the rest zilienda owa wapigaji means gigantic corrupt

Wakati ikulu ilijengewa kwa pesa halali hakuna kupiga apo .


Au nimekosea
 
Sasa hiyo Machakos ndiyo unajaribu kuringanisha na State house ya Chamwino?
Hiyo ya Machakosi si ni kama Magufuli Hostels zilizopo UDSM?
Hawa mbwa sijui wanatatizo gani na Tz,kwanini wasijolinganishe na Somalia au Ethiopia majirani zao
 
Baada ya Tanzania kuanza kuwapelekea moto kwenye mambo ya Uchumi,Wakenya wameanza kuwa na wivu Kwa kupondea majengo yetu hasa Ikulu.

Huko Twitter Tanzania haikauki midomoni mwao.kwa Kila kitu kujikinganisha.Mara wasema Dodoma ni Kama Kisii mara waseme Ikulu ya Dodoma Inafanana na Ofisi ya Gavana wao huko Machakos ilimradi tuu waichafue Nchi yetu.

My Take
Tusiache kupiga kazi Hadi wapasuke Kwa wivu .Kazi iendelee.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom