Kila Mtanzania ajivunie IKULU mpya ya Chamwino

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Jumamosi, tarehe 20 Mei 2023 Tanzania, imeandika historia nyingine kubwa katika Bara la Afrika na duniani. Ni kwa kuzindua Ikulu mpya katika Makao makuu ya nchi, Dodoma.

Ikulu mpya ya Chamwino ilizinduliwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, huku wageni mbalimbali wakishuhudia. Ni Ikulu ya kihistoria kwani ni kubwa ikiwa na ukubwa wa ekari 8,473, huku ikizungukwa na ukuta mrefu wenye kilometa 27.

Ndani ya Ikulu hiyo ya Chamwino kuna wanyama mbalimbali hususan swala, sungura, digidigi na tausi.
Jengo la Ikulu ya Chamwino linafanana kwa namna ilivyojengwa Ikulu ya Dar es Salaam,. ambayo ilianza kutumiwa na wakoloni mwaka 1891, baada ya kutangazwa kuwa makao makuu ya utawala wao katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kuzinduliwa kwa Ikulu hiyo ni fahari kwa kila Mtanzania. Ni fahari kwa sababu Ikulu hiyo imetokana na kodi za Watanzania. Lakini kubwa zaidi, imetokana na ujuzi na weledi wa Watanzania wenyewe kupitia vijana wazalendo wakiongozwa na maofisa wao kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Hivyo, kuzinduliwa kwa Ikulu mpya kunaendeleza dhana nzima ya taifa kujitegemea katika mambo yake nyeti na yenye maslahi mapana. Huu ni mwendelezo wa msingi wa taifa linalojitegemea, ambao uliwekwa na waasisi wetu chini ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Kujengwa kwa Ikulu hiyo mpya kwa kutumia kodi na nguvu kazi ya Watanzania, pia kunatoa somo kubwa kwa mataifa mengine ya Afrika na dunia kuiga Tanzania.

Ikulu hiyo imezidi kuifanya Tanzania kuendeleza historia ya kuwa na upekee katika mambo mbalimbali. Tanzania ina amani, utulivu, usalama wa hali ya juu na imekuwa ikipiga hatua mbalimbali ikiwemo kujenga |kulu hiyo kubwa na ya kisasa. Hongera Watanzania, tujivunie lkulu.​
 
Hongera sana hujaandika kishabiki(kichama). Ngoja waje wajinga wa CCM na CHADEMA.

Pia wale wafiwa wa yule mshamba wa Chato ambaye anaoza kaburini.
 
Nchi hii nisha gundu tatizo sio Satawala bali ni raia wenye upeo wa kiwango cha chini kabisa
 
Watanzania wana matatizo mengi kiasi kwamba hakuna mwenye tatizo na ikulu mpya, wala kujisikia fahari ya hiyo ikulu. Watu wanaoona ikulu ni ya maana ni viongozi, na wanaccm wanaodhani kujenga ikulu ni jambo la maana. Nyie mnaokula cake ya taifa ndio mnaona fahari ya ikulu mpya.
 
Kuna Watu Wana IQ ndogo sana hasa watanzania walio wengi,sioni mantiki ya kusherekea jengo wakati huo huo tunasaidiwa kujenga matundu ya vyoo katika shule zetu
 
Back
Top Bottom