Bila shaka wewe mwalimu wako alipata shida kukufundisha kwa sababu "mindset" yako ni "dogmatic".
Hiki ni kiashiria cha kushindwa kujenga hoja.
Katika mafundisho ya Uislamu, Mungu anatutaka hapa duniani tumuabudu na tufanye mema ili huko ahera akatulipe kulingana na ibada na wema tulioutenda hapa duniani, hivyo raha na furaha ya peponi ni malipo aliyotuahidi yeye Mungu mwenyewe na ili kututia moyo ndiyo maana akatoa "mifano" ya yale atakayotulipa huko akhera kwa njia ya hali ya hapa duniani---- Mungu anaposema atatupatia Asali, maziwa,maji, wasichana bikira, mabustani yapitayo mito, matunda nk, hivi ni vitu vya mfano tu ili tumuelewe na tuhamasike katika kumuabudu na kufanya wema, Asali,maziwa, wasichana bikira, matunda nk, vya kiroho ni tofauti kabisa na Asali, na maziwa nk, tulivyonavyo hapa duniani, na hili nililisema katika angalizo.
Huyu atakuwa si Mungu mkuu bali huyu atakuwa allah shetani mkubwa BAAL.
Mungu hawezi kuahidi ahadi za ajabu kama hizi mabikira 72 yani huko peponi kwa allah nyie mtakuwa mnafanyaga ngono tu?
Unasema; "mtaketi na Yesu upande wa kuume wa Mungu baba mkiimba na kumsifu"--- hapo unapinga nini na unaunga mkono nini??!!--- nikuulize, je mtaimba na kumsifu Baba Mungu kimwili kama hapa duniani au kiroho??!, kumbuka umesema huko hakuna tamaa/mambo ya kimwili.
Nilisema tangu awali mwili hufa ila roho haifi
Swali la kwanza umeuliza nakubali kipi na kupinga kipi hilo ni jambo moja tutaenda kuketi pamoja naye huku tukiimba na kuabudu.
Swali la pili umeuliza tutaimba na kusifu kimwili kama hapa duniani? Jibu ni hapana kwa sababu mwili hufa ila roho haifi na ili uyashinde mauti ni lazima uwe mwana wa Kristo huyu pekee ndiye aliyeyashinda mauti
Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu.
Lakini sasa KRISTO AMEFUFUKA katika wafu, limbuko lao waliolala."
1 Wakorintho 15:17, 20 SUV
Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. Hayupo hapa; maana AMEFUFUKA KAMA ALIVYOSEMA. Njooni, mpatazame mahali alipolazwa.
Mathayo 28:5-6 SUV
YESU YU HAI!
Katika Uislamu ni kwamba licha ya kulipwa raha na starehe peponi kutokana na wema tuliotenda, ibada na tasbihi kwa Mungu zitaendelea milele ILA ni hiyari ya mtu afanye au asifanye huko halazimishwi mtu kama tunavyolazimika hapa duniani, na huko mtu ukifanya ibada na tasbihi ndipo daraja lako la "kumkaribia" Mungu kiroho linaongezeka kwa sababu ndani ya pepo kuna madaraja na huko watu watajibidiisha kupanda hayo madaraja.
Yani kumbe kwa mujibu wa imani yenu hata mkifa na mlikuwa mnafuata mienendo yote ya allah bado hamtawahi kumfikia Mungu na hata parapanda itakapolia itabidi muendeleze ibada ili kuufikia utukufu wake?
Unasema; "kipigo" cha yesu msalabani ndiyo mmepona na hamna shaka tena dhidi ya mauti na hamuangaishwi na mambo ya kimwili"--- nikuulize; je, wale waliompigilia yesu msalabani ili mauti na dhambi zenu ziondoke mnawaitaje?? Mashujaa au wakombozi wenu pia??
Yesu alitabiri hili jambo mapema
" ....akawaambia, Mwana wa Adamu yuaenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua; na akiisha kuuawa, baada ya siku tatu ATAFUFUKA."
Marko 9:31 SUV
Wale waliomtesa Yesu walikuwa wanatekeleza amri iliyotolewa na pilato na Yesu alisema imekwisha yani dhambi haipo tena na aliwasamehe watu wote waliomkosea.
Kristo ana nguvu za kusamehe dhambi, kufufua, kuponya na ni njia ya uzima wa milele.
maana (kwa akili yenu mbovu) na wao wlishiriki katika tukio la UKOMBOZI WENU.-- Yesu hakupigiliwa msalabani kuokoa dhambi zenu, huo ni uongo mkubwa sana mnaozua, yeye nwenyewe hakupenda kunywa hicho kikombe cha laana ya kifo cha msalaba, kwani imeandikwa yeyote angikwaye msalabani na akafia hapo "amelaanika" (kumb, la torati).---- mimi sikubali kwamba Yesu anaweza kuwa laana, aliyelaanika ni mtu wa shetani.
Hii ni mada nyingine tena ambayo inaweza kuzua mjadala sisi kama Wakristo hatuna Torati, Torati ni sheria za mwili yani zinahusu mambo ya kimwili na si kiroho.
wakati wa Torati mwanamke mchawi alikuwa anapondwa mawe hadi kufa lakini wakati wa Kristo ni upendo na kumuonyesha njia
wakati wa Torati ilikuwa mzini anapondwa mawe hadi kufa ila sasa anahitaji huruma ya Yesu.
WARUMI 7:
5 Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao.
7 Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.
8 Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa.
9 Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa.
11 Kwa maana dhambi, kwa kupata nafasi kwa ile amri, ilinidanganya, na kwa hiyo ikaniua.
13 Basi je! Ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? Hasha! Bali dhambi, ili ionekane kuwa ni dhambi hasa, ilifanya mauti ndani yangu kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno.
14 Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.
15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.
16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.
17 Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu
18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
Umesema Yesu mwenyewe hakupenda hicho kikombe cha laana na hakupigiliwa msalabani kuokoa dhambi zetu "Yani unaandika neno uongo kabisa hata pasipo kutafuta maandiko" fuatana nami
2Wakorintho 5:21 inatufundisha, “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye.
Waefeso1:7 yasema, “katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.”
1Yohana 2:2 asema, “Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.
Yohana 3:16-17 ina habari hii ya ajab, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Nadhani sasa utakuwa umefahamu kwanini Kristo alisurubiea msalabani.
Wakati wa Torati ambako Mungu alikuwa ni wa Taifa moja tu Israel alikuwa anafanyiwa kafara ya damu kama kumpunguza hasira n.k ila hapa alitoa kafara moja tu ya Damu ya Kristo nasi tumepona
Ukisoma , Wagalatia 6:5, inasema:- "for each one should carry his own load".
🍒 Kila mmoja ataubeba mzigo wake mwenyewe 🍒-- na Yesu aliubeba mzigo wake mwenyewe na wewe dripboy utaubeba mzigo wako, Yesu hayupo nawe katika hiki.
Adieu.
Kwa hizo aya juu utatambua kuwa dhambi zangu sinazo tena Yesu alishazimaliza msalabani na nina amini katika hilo
Wagalatia 6: 4 Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake.
5 Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe.
6 Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote.
7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.
8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.
Soma uelewe nimekuwekea kuanzia 4-9