Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,956
Waarabu wanazidi kusema kuwa hawana dini tena, kwa mujibu wa utafiti mkubwa na wa kina uliofanywa wa eneo la mashariki ya kati na Afrika kaskazini.
Utafiti huo ni mmoja kati ya baadhi kuhusu namna waarabu wanahisi kuhusu masuala tofuati, kuanzia haki za wanawake na uhamiaji, usalama na mahusiano.
Zaidi ya watu 25,000 walihojiwa katika utafti huo - uliofanywa kwa niaba ya BBC News Arabic na kituo cha utafiti cha Arab Barometer research network - katika nchi 10 na maeneo ya Palestina kati ya mwisho wa mwaka 2018 na 2019.
Soma hiyo: https://www.bbc.com/swahili/habari-48754397
Cc: Kiranga, FaizaFoxy
Dini zipo nyingi, ni dini ipi waarabu wameipuuza, na ni waarabu kutoka wapi??, fafanua hapo.
Kama kupuuza dini ni kupuuza dini zingine mbali na uislamu hiyo siyo ajabu kwasababu waarabu wengi kiasilia ni waislamu.
Hatahivyo si waarabu pekee wanaopuuza dini hata wazungu siku hizi huko ulaya hawaendi tena makanisani kama ilivyokuwa zamani kiasi kwamba baadhi ya yaliyokuwa makanisa yameuzwa na kugeuzwa misikiti, na kumekuwa na wind of change from Christianity to Islam in the West Europe.