Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,764
- 10,639
Kauli yake ya "Mungu oyeeeeeeee!!!" aliyoitoa Zanzibar karibuni, katika kampeni za chama chake imewauzi wengi hapa...mzee huyu anazeeka vibaya apumzike tena.
Hebu ishushe kidogo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kauli yake ya "Mungu oyeeeeeeee!!!" aliyoitoa Zanzibar karibuni, katika kampeni za chama chake imewauzi wengi hapa...mzee huyu anazeeka vibaya apumzike tena.
Mzee anapokataa kuzeeka inabidi aachwe azeeke mwenyewe
Hivi Makamba amefikia kiwango gani cha elimu vile?
Hivi Makamba amefikia kiwango gani cha elimu vile?
Kariakoo ndo inayoipa ushindi CC'EMU kila kipindi, Makada na wazee wengi wa sisisem hadi mbunge wa ILALA "ZUNGU" la Unga ambalo halijawai hata kuonge neno moja bungeni limechaguliwa na watu haohao wa Kariakoo.Safi sana. CCM inajikaanga kwa mafuta yake yenyewe.
Tulisema mengi kuhusu Makamba kwamba ni mropokaji, hafai kuwa nafasi ya juu chama chochote.Tulisema kuwa CCM ya kina Makamba na JK imekumbatia matajiri na mafisadi na kuwasahau watu Maskini, ambao kwa upande moja imewasababishia umaskini, lakini wengine wakapinga.
Tuelewe kuwa CCM haina na muda kwa maskini. Hao wa Kariakoo ni mfano tu. Walipokuwa wanawasomba na magari ili wafike Jangwani kwenye mkutano wa ufunguzi wa kampeni msidhani wanapenda, ni kwa sababu walitaka kujaza uwanja, ionekane CCM inapendwa.
Maskini tupo wengi. Tunataka suala la njaa lisiwe mjadala ya miaka yote. CCM haina nia ya kumaliza njaa yetu. Tukirudisha madarakani tusibiri matusi zaidi.
Natumaini hadi sasa kila moja amekwishaona Chama gani kina nia thabiti ya kuwatoa wanzania kutoka lindi la umaskini, ila sio CCM.
Wanakariakoo, hakuna sababu ya kuhangaika na Makamba, eti aombe msamaha. Ni kutumia kura yako tu hapo Oktoba 31.
January is far better than his dad
Makamba nimefurahi yamekukuta maana wewe ni bingwa wa kubeba kauli za watu na kuzipigia filimbi, muosha huoshwa
LOL
Makamba, hajui alitendalo. Kwa maneno yake anatusaidia kuweka pembeni CCM. Makamba na asonge mbele kuropoa kwake ni mtaji katika kipindi hiki chakuelekea mabadiliko maana anazidi kuaminisha umma kwamba CCM haina mwelekeo na imekosa dira. Kukosa dira kw CCM ni zao laviongozi walio kosa dira.
Ulimi wamponza Yusuf Makamba
wakazi Kariakoo wadai amewadhalilisha
Washinikiza aombe radhi, ajiuzulu
Kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw Yusuf makamba kuhusu ombi la mdahalo la mgombea ubunge kupitia chama hicho Jimbo la Urambo Mashariki, Bw Samuel Sitta na mgombea urais kupitia Chadema, Dk Wilbrod Slkaa, imezua mtafaruku miongoni mwa wanachama wa chama hicho.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa CCM imenawa mikono na haihusiki na mgogoro baina ya wanasiasa hao huku vikimkariri Bw Makamba akisisitiza kuwa Sitta na Dk Slaa, wana mambo yao wenyewe na wala hayakihusu chama hicho.
Bw Makamba alikaririwa akisema CCM kimekataa midahalo kwa sababu hukusanya watu wa hovyo na hakuna mikakati maalum ya kuiendesha kwa kujieleza na kukosoana kulingana na sera za vyama husika.
Alisema chama hicho hakiogopi midahalo, bali kisingependa kuona kinashiriki kwenye midahalo kwa sababu zinaweza kuibuliwa hoja zisizo na msingi kwa makusudi ya kukichafua.
Tunataka mdahalo uwe wa sera. Sio unakusanya watu wa Kariakoo halafu anajitokeza miongoni mwao ambaye jana alilala njaa halafu anasema jana CCM ilitulaza njaa, alinukuliwa akisema Bw Makamba.
Kitendo cha Bw Makamba kutolea mfano wakazi wa eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam kimezua mtafaruku miongoni mwa wananchi hao na kuwafanya baadhi yao kufika katika ofisi za gazeti hili na wengine kupiga simu kwa madai wamedhalilishwa na Kariakoo kuonekana ni eneo wanaokusanyika watu wenye njaa.
Wananchi hao walionesha hisia za kukerwa na kauli hiyo huku wengine wakimtaka Bw Makamba awaombe radhi sambamba na kujiuzulu wadhiufa wake ndani ya chama hicho tawala kwani amewadhalilisha wakazi wa Kariakoo, watu wanaofanya biashara zao sehemu hiyo na eneo hilo kwa ujumla.
Walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa mdahalo ni haki ya wapiga kura na kwamba yeyote anayeshiriki awe mwenye njaa au aliyeshiba mawazo yake yanapaswa kuheshimiwa kwani kinachotakiwa kusikilizwa ni majibu ya kutoka pande zinazohojiwa.
Walidai kuwa kauli ya Makamba imejaa kejeli na dharau kubwa dhidi ya watu masikini kwani njaa zao zimechangiwa na wanasiasa hivyo wana haki ya kuwauliza kwa nini sera zao zinawaletea njaa.
Watu hawalali njaa kwa kupenda, kuna mambo mengi, mengi yanachangiwa na hawa wanasiasa. Sasa kama kuna mtu amelala njaa ana haki kwenda kwenye mdahalo na kuhoji chanzo cha njaa yake. Sasa kama Makamba anatuona tunaokaa Kariakoo au kufanya biashara zetu pale tukiamka na njaa zetu tunakuwa hatuna akili na hatutakiwi kwenda kwenye mdahalo kwa sababu tutauliza kwa nini hatukula, hii ni dharau kwa umma, awajibike, ametudhalilisha watu masikini! Njaa si kigezo cha kuzuiwa kwenda kuhoji watu wanaoomba uongozi ..
Habari zaidi katika Majira ya leo.
LIKE FATHER LIKE SON..au unaposema January is far better unamaanisha "FAR BETTER IN TALKING CHEAP SHIT than his dad"?
Haya ndo madhara ya kutoutumia ulimi vizuri:
- Yakobo 3:5
Yakobo 3:4-6 (in Context) Yakobo 3 (Whole Chapter)
- Yakobo 3:6
..........................nao ulimi huwashwa moto wa kuzimu.
Yakobo 3:5-7 (in Context) Yakobo 3 (Whole Chapter)
Hivi Makamba amefikia kiwango gani cha elimu vile?