Ulimi wamponza Yusuf Makamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulimi wamponza Yusuf Makamba

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Sep 20, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Ulimi wamponza Yusuf Makamba

  • wakazi Kariakoo wadai amewadhalilisha
  • Washinikiza aombe radhi, ajiuzulu


  Kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw Yusuf makamba kuhusu ombi la mdahalo la mgombea ubunge kupitia chama hicho Jimbo la Urambo Mashariki, Bw Samuel Sitta na mgombea urais kupitia Chadema, Dk Wilbrod Slkaa, imezua mtafaruku miongoni mwa wanachama wa chama hicho.

  Mwishoni mwa wiki iliyopita, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa CCM imenawa mikono na haihusiki na mgogoro baina ya wanasiasa hao huku vikimkariri Bw Makamba akisisitiza kuwa Sitta na Dk Slaa, wana mambo yao wenyewe na wala hayakihusu chama hicho.

  Bw Makamba alikaririwa akisema CCM kimekataa midahalo kwa sababu hukusanya watu wa hovyo na hakuna mikakati maalum ya kuiendesha kwa kujieleza na kukosoana kulingana na sera za vyama husika.

  Alisema chama hicho hakiogopi midahalo, bali kisingependa kuona kinashiriki kwenye midahalo kwa sababu zinaweza kuibuliwa hoja zisizo na msingi kwa makusudi ya kukichafua.

  “Tunataka mdahalo uwe wa sera. Sio unakusanya watu wa Kariakoo halafu anajitokeza miongoni mwao ambaye jana alilala njaa halafu anasema jana CCM ilitulaza njaa,” alinukuliwa akisema Bw Makamba.

  Kitendo cha Bw Makamba kutolea mfano wakazi wa eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam kimezua mtafaruku miongoni mwa wananchi hao na kuwafanya baadhi yao kufika katika ofisi za gazeti hili na wengine kupiga simu kwa madai wamedhalilishwa na Kariakoo kuonekana ni eneo wanaokusanyika watu wenye njaa.

  Wananchi hao walionesha hisia za kukerwa na kauli hiyo huku wengine wakimtaka Bw Makamba awaombe radhi sambamba na kujiuzulu wadhiufa wake ndani ya chama hicho tawala kwani amewadhalilisha wakazi wa Kariakoo, watu wanaofanya biashara zao sehemu hiyo na eneo hilo kwa ujumla.

  Walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa mdahalo ni haki ya wapiga kura na kwamba yeyote anayeshiriki awe mwenye njaa au aliyeshiba mawazo yake yanapaswa kuheshimiwa kwani kinachotakiwa kusikilizwa ni majibu ya kutoka pande zinazohojiwa.

  Walidai kuwa kauli ya Makamba imejaa kejeli na dharau kubwa dhidi ya watu masikini kwani njaa zao zimechangiwa na wanasiasa hivyo wana haki ya kuwauliza kwa nini sera zao zinawaletea njaa.

  “Watu hawalali njaa kwa kupenda, kuna mambo mengi, mengi yanachangiwa na hawa wanasiasa. Sasa kama kuna mtu amelala njaa ana haki kwenda kwenye mdahalo na kuhoji chanzo cha njaa yake. Sasa kama Makamba anatuona tunaokaa Kariakoo au kufanya biashara zetu pale tukiamka na njaa zetu tunakuwa hatuna akili na hatutakiwi kwenda kwenye mdahalo kwa sababu tutauliza kwa nini hatukula, hii ni dharau kwa umma, awajibike, ametudhalilisha watu masikini! Njaa si kigezo cha kuzuiwa kwenda kuhoji watu wanaoomba uongozi………..”

  Habari zaidi katika Majira ya leo.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  Makamba ana kipaji cha uropokaji.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  wHEN IT COMES TO SERIOUS MATTERS KAMA za ku'address kwa wananchi Makamba hatakiwi kusogeza pua yake huko, maana hana uwezo wa kutathmini aftermath za kauli zake!...he is known for talking off-points and unnecessary comments!
  Ukubwa wa umri si busara ati!, na atawagharimu sana yule babu..but at our advantage!
   
 4. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  "akheri ukajikwaa kidole kuliko kujikwaa ulimi", huyu Babu akili zake zimeisha sasa anaropoka tu pasipo hata maana, wamshikie baongo hivyo hivyo.
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Baba yake JANUARY mshauri wa JK
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawa viongozi wa CCM huwa wana dharau nyingi sana kwa wananchi. Baada ya JK kuwakejeli wafanyakazi nchini, sasa linakuja hili. Hii inakumbushia yule kada mwingine mropokaji wa CCM -- Pius Msekwa -- na bifu lake dhiidi ya wanawake miaka kadhaa iliyopita aliupokuwa Spika. Nimesahau tu issue yenyewe lakini alinukuliwa na vyombo vya habari akiwaambia wapinzani kwamba 'wasiwe na wivu kama wanawake.'

  Alijuta kwa kauli hiyo kwani wanawake, na hasa kupitia taasisi zao kama vile TAMWA n.k. walimjia juu hadi mwisho wake ilibidi aombe radhi kwao.
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Makes sense!!!!!
   
 8. e

  emalau JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Wakazi wa kariakoo kwa kauli ya makamba wanarepresent watu wote wenye shida na wanaolala na njaa nchi nzima. Kwa hiyo ni wakati muafaka wa kumpa adhabu yeye pamoja na chama chake kwa utowapa kura kwa kuwa inaonyesha wanataka matajiri peke yao ndo wawe karibu nao. Ama kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa.
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Unachosema ni kweli kabisa. Kama TBC wangesema mdahalo uwe un ahudhuriwa na matajiri tu kama ndiyo waulizaji maswali, CCM ingeafiki mara moja! Masikini hawana kauli katika sera za CCM.
   
 10. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,992
  Likes Received: 1,046
  Trophy Points: 280

  Haya ndo madhara ya kutoutumia ulimi vizuri:
  1. Yakobo 3:5
   Ulimi nao ni kiungo kidogo sana lakini hujivunia mambo makuu. Fikirini jinsi moto mdogo unavyoweza kuteketeza msitu mkubwa!
   Yakobo 3:4-6 (in Context) Yakobo 3 (Whole Chapter)
  1. Yakobo 3:6
   Ulimi pia ni kama moto. Ulimi ni ulimwengu wa uovu kati ya viungo vyetu. Humchafua mtu nafsi nzima na kuwasha moto maisha yake yote, nao ulimi huwashwa moto wa kuzimu.
   Yakobo 3:5-7 (in Context) Yakobo 3 (Whole Chapter)
   
 11. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kauli yake ya "Mungu oyeeeeeeee!!!" aliyoitoa Zanzibar karibuni, katika kampeni za chama chake imewauzi wengi hapa...mzee huyu anazeeka vibaya apumzike tena.
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mzee anapokataa kuzeeka inabidi aachwe azeeke mwenyewe
   
 13. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sio kama Ulimi wa Makamba au Manyuzi uliteleza, La hasha, alikua anaongea ukweli juu ya tabaka la watu wa CCM hasa viongozi, CCM ni chama cha matajiri ambao hawaijui njaa ndo maana hata M'kiti wake alipojaribu kufunga alishindwa hata kusimama huku akiongea hadi akaanguka....je angekua na swaumu then anatakiwa kwenda shamba ingekuaje?????

  Jamaa hauaijui njaa kabisa koz wao ndo wamiliki wa kila kitu, hata hizi tuzijuazo kama mali za uma wao wajuavyo ni zao na wanaweza fanya lolote koz ndio viongozi wa chama tawala na Serikali. Ila Ndg Makamba jua hakuna lenye mwanzo likosalo mwisho, kila nafsi itaonja umauti. Wamekufa mitume, viongozi wa mataifa yenye nguvu kiuchumi sembuse wewe Katibu wa CCM tena katika nchi masikini kama TZ?? Acha Dharau zisizo na mpango tenda haki kwa wote. CCM ndo imejenga matabaka kati ya Matatjiri na masikini bado mnaenda mbali kwa kuwadharau na kuwadhihaki masikini tena sio kwa siri bali shahir dhahir. Nini Dhamira yako katika hili????

  Hakuna mtu apendae kulala njaa, wala hakuna asiependa kuwa na kizuri. Kila binaadam hupenda kizuri ila sio wote wanaoweza kupata vizuri so inachotakiwa ni kujenga mazingira mazuri kwa masikini na asiekuwa naho kujisikia salama katika nchi yake. Hii nchi sio mali ya watu wachache ambao ni rafiki zako wanaoshiba. hao wanaolala Njaa ndo wengi katika nchi hii so siku wakichoka ndo uatajua pa kukimbilia wewe na Rafiki zako manaoshiba.

  Fikiri kabla ya kunena ndg Makamba. "UKIONA NENO USINENE NENO UKINENA NENO LITAKUJIA NENO" Haya sasa ushanena na ninauhakika ushajiona u mjinga na mpumbavu katika kuchagua ya kuongea. Sidhani kama una ubavu wa kupita kariakoo bila escort ya wana usalama. sasa ndy maisha gani hayo??????
   
 14. M

  Mkora JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Huyu kweli vuvuzela
  Kariakoo sindio sehemu tajiri kuliko zote Tanzania
  Kiwanja leo 1 bilion TSH kupanga chumba hadi 250,000 kwa mwezi
  Labda kama kuna karia koo nyingine bumbuli
   
 15. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hivi Makamba amefikia kiwango gani cha elimu vile?
   
 16. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wakazi wa Kariakoo adhabu muafaka kwa Makamba ni kuinyima kura CCM kuanzia yaani mafiga yake yote matatu(raisi, ubunge na udiwani) muone hiyo ropoka yake kama itakuja endelea tena
   
 17. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #17
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kwa kweli nilimsikia Makamba siku ile hadi hamu ya kula ikaisha; Kwa ufupi kauli yake ilikuwa hivi

  1. Kama ni mdahalo, kila chama kiende na ilani yake, kisome, alafu ambaye hajaelewa aulize swali kutokana na kilichosomwa!!!

  2. Hairuhusiwi kuulizwa swali nje ya ilani

  3. Iamuliwe ni watu gani watakaokuwa kwenye huo mdahalo, sio tu kuchukua watu kutoka Kariakoo huko unawaleta kwenye mdahalo...
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Huo ulimi sasa ni sugu kwa kumponza...hajaanza leo
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  January is far better than his dad

  Makamba nimefurahi yamekukuta maana wewe ni bingwa wa kubeba kauli za watu na kuzipigia filimbi, muosha huoshwa

  LOL
   
 20. D

  Dopas JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Safi sana. CCM inajikaanga kwa mafuta yake yenyewe.

  Tulisema mengi kuhusu Makamba kwamba ni mropokaji, hafai kuwa nafasi ya juu chama chochote.Tulisema kuwa CCM ya kina Makamba na JK imekumbatia matajiri na mafisadi na kuwasahau watu Maskini, ambao kwa upande moja imewasababishia umaskini, lakini wengine wakapinga.

  Tuelewe kuwa CCM haina na muda kwa maskini. Hao wa Kariakoo ni mfano tu. Walipokuwa wanawasomba na magari ili wafike Jangwani kwenye mkutano wa ufunguzi wa kampeni msidhani wanapenda, ni kwa sababu walitaka kujaza uwanja, ionekane CCM inapendwa.

  Maskini tupo wengi. Tunataka suala la njaa lisiwe mjadala ya miaka yote. CCM haina nia ya kumaliza njaa yetu. Tukirudisha madarakani tusibiri matusi zaidi.

  Natumaini hadi sasa kila moja amekwishaona Chama gani kina nia thabiti ya kuwatoa wanzania kutoka lindi la umaskini, ila sio CCM.

  Wanakariakoo, hakuna sababu ya kuhangaika na Makamba, eti aombe msamaha. Ni kutumia kura yako tu hapo Oktoba 31.
   
Loading...