Ulikuwa wapi siku kifo J. Nyerere (baba wa Taifa) kinatangazwa?

Nakumbuka wakati huo nlikua darasa la 4 pale naura primary-arusha,tulikuwa tunapga test ya maarifa ya jamii,ndo kifo chake kikatangazwa.RIP mwalimu,we wl miss u much.
 
Nakumbuka ilikuwa siku ya jumanne niko kidato cha pili majira ya saa 4:30 tuko darasani na mwl wa Archtectural drawing ,ilikuwa ni mlinzi wa shule ndio alikuwa anazunguka kwenye corridor za madarasa na kusema nyerere ameaga duniani huku yuko na redio ikipiga wimbo wa taifa then akaja mkapa kulìhutubia taifa. Wewe ulikuwa wapi wakati huo ?

dah safety last mm nakumbuka hiyo siku ilikuwa alhamis km sikosei nilikuwa shule moshi technical sec school, form two km wewe, hiyo siku sikwenda class nilibaki bwenini kwa kuwa nilikuwa naumwa, ndipo niliposikia huo msiba wa mwalimu JKN. na baad ya muda watu wote wakashuka toka madarsani kila mtu akihuzunika kivyake. RIP Nyerere.
 
Kipindi hicho nakumbuka nilikuwa form 2. Mbeya sec. School wakati ishu inatokea. Kufa kwake nakumbuka walituambia hakuna kusikiliza nyimbo za kujirusha zaid za kuomboleza.
 
Nilikuwa ndo natoka moja ya ofisi pale zilipokuwa ofisi za tume ya jiji Dar,kuchukua barua yangu ya kupangiwa kituo cha kazi, baada ya kupata uhamisho toka mikoani.
 
Nakumbuka ilikuwa siku ya jumanne niko kidato cha pili majira ya saa 4:30 tuko darasani na mwl wa Archtectural drawing ,ilikuwa ni mlinzi wa shule ndio alikuwa anazunguka kwenye corridor za madarasa na kusema nyerere ameaga duniani huku yuko na redio ikipiga wimbo wa taifa then akaja mkapa kulìhutubia taifa. Wewe ulikuwa wapi wakati huo ?

Nakumbuka tulikuwa tunajiandaa na gradu ya kumaliza shule ya msingi gafla mwalimu mkuu akatuambia mahafali hayatakuwepo kwa sababu Mpendwa baba wa taifa ameaga dunia..ilikuwa huzuni kwa kila mtu.
 
Nakumbuka nilikua darasa la5 shule moja ya boarding huko arusha.at that time tulikuwa porini tunakata kuni za shule,kuna baadh yetu walikuwa na viredio vidogo vile!ndo walitupa taarifa!it was so sad kwakweli.

mazee ulikuwa manyara ranch au?
 
Nilikuwa Kasulu Kigoma, nikifukuzia kibarua kwenye mashirika ya wakimbizi,wakati huo nikiwa nimemaliza form six na ktk harakati hizo ndipo nilikutana na Moses Machali yeye bado akiwa vidato vya chini Kasulu Sekondari.
 
Nilikuwa kidato cha nne tunajiaandaa kwenda kununua mahitaji kwaajili ya kuagwa YCS form 4 ndio mara Mkuu wa shule akatuita viongozi na kusema sherehe zote zimefutwa.......
kilichoendelea ni huzuni tu pale shule.......

Nakumbuka hata Graduation zote zilifutwa hivyo kila kitu kilikwenda tofauti.
 
Tulikuwa kwenye kikao cha maandalizi ya graduation ya form 4, kidato hicho wote tulikuwa assembly hall tunapanga ratiba na vitu vingine maana ilikuwa iwe Jumamosi inayofuata (zilibaki siku mbili tuu).

Lilikuja nunda moja la form three sijui likowapi siku hizi, alikuwa anaitwa Damson, likasimama dirishani na kushout 'tokeni humo Nyerere kafa hakuna cha Graduu' Ikatulazimu tutoke wote pamoja na walimu kwenda lounge kuangalia kama ni kweli

Michango na kila kitu tukasahau shuleni dah!!! Na ndiyo basi tena hatukuwa na graduu ten!!
 
Nakumbuka!
Nilikuwa Machimboni ktk kutafuta pesa ya ada kwaajili ya masomo ya mdogo wangu. Ni ktk mapori ya mpakani mwa TZ na Msumbiji eneo lijulikanalo kama Ndago Ligoma kwenye makutano ya Mto Muhuwesi, Mto Mtetesi na Mto Ruvuma ktk wilaya ya Tunduru kilomita zaidi ya mia kutoka barabara itokayo Masasi hadi Tunduru. Mimi pekee ndo nilikuwa namiliki radio ktk kambi yote ya wachimbaji wadogo. Wachimbaji walijazana pembeni ya shimo langu la kuchimba madini kusikiliza mara baada ya wimbo wa taifa kuanza kusikika. Baada ya taarifa ya kifo cha Mwl watu waliamua kuacha kuchimba kwa siku ile na kurudi kambini. Ajabu ni kuwa ndani ya wiki hiyo watu walipata madini na kurudi makwao na mijihela si haba! nikiwa mmoja wao. Nakumbuka Radio yangu ilikuwa aina ya National 277 (tamka mbili sabasaba) Dudu proof a.k.a Mkulima. Kutoka kiwanda cha Matsushita Electric Company pale Pugu Road DSM. Na bado ingalipo ikitwanga mzigo tangu iliponunuliwa na Baba yangu (R.i.p) mwaka 1978 ktk moja ya duka la RTC.
Nawatakia kumbukumbu njema Wajameni!
 
nilikuwa sekondar ARUSHA MERU SEC, 2katangaziwa na kwenda hm nikiwa stand niliona mmasai akipiga ukunga kumbe kasikia nyerere ame kick ze backet
 
Nakumbuka ilikuwa siku ya jumanne niko kidato cha pili majira ya saa 4:30 tuko darasani na mwl wa Archtectural drawing ,ilikuwa ni mlinzi wa shule ndio alikuwa anazunguka kwenye corridor za madarasa na kusema nyerere ameaga duniani huku yuko na redio ikipiga wimbo wa taifa then akaja mkapa kulìhutubia taifa. Wewe ulikuwa wapi wakati huo ?
duuh, umenikumbusha mbali sana. mi nilikuwa maeneo ya kasulu nikiwa najiandaa na mtihani wa form four. kwa sababu ya kifo hiki, nakumbuka hata hatukufanya graduation ceremony....
 
Back
Top Bottom