Ulikuwa wapi siku kifo J. Nyerere (baba wa Taifa) kinatangazwa?

Dah umenikumbusha mbali sana mbali sana...miaka 12 iliyopita...nilikuwa kidato cha pili seminarini,tujiandaa kwa jiving na nyimbo za kuwaaga form four...mgeni rasmi mtarajiwa angekuwa Askofu TARCISIUS NGALALEKUMTWA(Jimbo katoliki Iringa),ghafla Gombera(Rector) wetu akaamuru kengele igongwe kitu ambacho ni adimu sana,ukiona ivo ujue mtu anafukuzwa seminar kwa utovu wa nidhamu...na mim nilikuwa na kesi ya kuiba maparachichi na mapera bustanin kwa Masista Kamadolesi,nkajua ndo safari ya home....HP wetu ambaye sasa ni Padri wa kanisa katoliki uko Parelmo Italy akampa Rector nafasi...akatangaza kwa Huzuni kuondokewa kwa baba wa Taifa...wote tukapoa...huzuni ikatanda...Tulikuwa na Tv room inashka DSTV tu!Tukafunguliwa chanel ya SABC-AFRICA,Wakawa wanatoa wasifu,hstoria ya mwalimu..24hrs...na siku ya mazishi Tulitazama kupitia SABC-AFRICA ya South Africa...nakmbuka mengi sana,lakn nimewakmbuka zaid marafik zangu waloamua kuendelea na Upadri..weng wako nje ya nchi wakihubiri Injili...Ni mda mrefu!!R.I.P J.K.NYERERE

Hii imenichekesha sana. Pole sana kwa yaliyokukuta, hasa mawazo ya kesi yako.
 
nilikuwa sekondar ARUSHA MERU SEC, 2katangaziwa na kwenda hm nikiwa stand niliona mmasai akipiga ukunga kumbe kasikia nyerere ame kick ze backet
Aisee na wewe unakumbukumbu! Hv pale shuleni siku ile si kuna yule chalii we2 naye alitaka kupandisha mori tukampoza? Ama umesahau? Rest In Peace Mwalimu.
 
Ndg yangu mawazo yamesafili mbali sana siku hiyo nakumbuka tulikuwa dalasani ndipo mzee moja alipita huku analia ndipo watu walilipoka na kilio
 
Nilikuwa najiandaa na mahafali ya kidato cha nne ndipo tukatangaziwa, na maandalizi yaliishia pale!
 
Nilikuwa Dar, katikati ya jiji natafuta story. Nilipofika Kituo cha kulelea watoto, Dogodogo Center, mtaa wa mansfield, nikaambiwa Nyerere kafa. Nilikimbia ukumbi wa habari maelezo kuangalia TV nikatuta Mkapa anatangaza, baada ya tangazo, nje ya ukumbi, mtaa wa Samora, Azikiwe nilishuhudia watu wakibubujikwa machozi. Kweli alikuwa statesman.
 
kipindi anafariki, nilikuwa darasa la saba siku chache kabla ya kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi. Kifo chake

hapana ndugu, 1999 mtihani wa taifa darasa la saba ulikuwa ni tarehe 29 september, labda kama ulikuwa shule za tofauti sana na za kwetu.

mie nilikuwa nimemalizadarasa la saba nasuiri majibu na siku hiyo nilikuwa nauza duka la nyumbani na mara redio free africa wakakatiza matangazo... na nakumbuka neno la kwanza nikasikia mkapa akisema "... mwalimu atazikwa kwa mazishi ya kitaifa..." nikatoka nikikimbia ndani kuwaambia kuwa Nyerere amefariki
 
NYERERE akiwa hospitali ST Thomas,atukujua how serious he was sababu international press haikuandika chochote,tuki communicate na ndugu tanzania,tunaambiwa nyerere yuko hospital UK-siku 3 kabla hajafariki magazeti ya UK yakaandika nyerere is in coma and his family is around him-thats when we knew its all over
 
Nakumbuka!
Nilikuwa Machimboni ktk kutafuta pesa ya ada kwaajili ya masomo ya mdogo wangu. Ni ktk mapori ya mpakani mwa TZ na Msumbiji eneo lijulikanalo kama Ndago Ligoma kwenye makutano ya Mto Muhuwesi, Mto Mtetesi na Mto Ruvuma ktk wilaya ya Tunduru kilomita zaidi ya mia kutoka barabara itokayo Masasi hadi Tunduru. Mimi pekee ndo nilikuwa namiliki radio ktk kambi yote ya wachimbaji wadogo. Wachimbaji walijazana pembeni ya shimo langu la kuchimba madini kusikiliza mara baada ya wimbo wa taifa kuanza kusikika. Baada ya taarifa ya kifo cha Mwl watu waliamua kuacha kuchimba kwa siku ile na kurudi kambini. Ajabu ni kuwa ndani ya wiki hiyo watu walipata madini na kurudi makwao na mijihela si haba! nikiwa mmoja wao. Nakumbuka Radio yangu ilikuwa aina ya National 277 (tamka mbili sabasaba) Dudu proof a.k.a Mkulima. Kutoka kiwanda cha Matsushita Electric Company pale Pugu Road DSM. Na bado ingalipo ikitwanga mzigo tangu iliponunuliwa na Baba yangu (R.i.p) mwaka 1978 ktk moja ya duka la RTC.
Nawatakia kumbukumbu njema Wajameni!

Kumbukumbu yako imenigusa. Nzuri sana
 
Mkuu mimi nilikuwa kidato cha pili Lugalo Sec School pale Iringa mjini,nakumbuka tukiwa shule tulishangaa tu walimu hawaji darasani na wengine wamekaa kwenye vikundi vikundi wakiwa kama wanamajonzi huku wengine wakishindwa kuzui hisia zao na kumwaga chozi,tulipopata taarifa tulienda kwenye ukumbi wa shule ambao ulikuwa na TV ya shule tukakuta nyimbo za maombolezo zimeanza kupigwa sijui zilitungwa saa ngapi.............
 
Nilikuwa Mikicheni B kwenye mabwawa ya maji machafu, nikasikia kale kamlio ka ajabu ka Redio Tanzania, ilikuwa mida ya saa nne, ndipo Mkapa akatangaza kifo cha Mwalimu

buji unaeza kuwa jirani angu, mi nilikuwa shule darasa 3 pale msasani praimari, mwl. bendera akatangaza kwny paredi ya ghafla kilichojiri, shule ikaahirishwa automatikale. kurudi nyumbani nakuta komba asharekebisha kila kitu na nyimbo zake zinapigwa itv.
 
nilikuwa shule nakumbuka kama sikosei ilikuwa lunch time mara wimbo wa taifa wanafunzi tukatega masikio ikafatiwa na sauti ya mkapa hakika ilikuwa ni vilio kwani tuliamini ilikuwa mwisho wa tanzania..

kweli ilikua mwisho wa tanzania, we huonii?
 
Nilikuwadarasa la sita enzi hizo wakati narudi shule wakati wa mchana ndio nikasikia Kengele inagongwa na mwalimu mkuu akaja kutangza na bendera ikawa inaning'inia nusu mlingoti.
 
nilikuwa shule nakumbuka kama sikosei ilikuwa lunch time mara wimbo wa taifa wanafunzi tukatega masikio ikafatiwa na sauti ya mkapa hakika ilikuwa ni vilio kwani tuliamini ilikuwa mwisho wa tanzania..

Lunch time saa nne asubuhi kama huna historia andika uongo unaofanana na ukweli
 
siku ile nlikua pale home angoni arms karibu na shule ya msingi majimaji Songea nakumbuka nlikuwa form one na nlikua naingia shule saa saba taasisi ya elimu ya watu wazima majengo sub-centre na kulikuwa na mafundi wa kufyatua tofali za kuchoma pale home mimi nlikua nimetoka kunywa chai na makaba huku redio tanzania wakipiga kipindi kile cha wagonjwa mahospitalini ghafla wimbo wa taifa kuna babu mmoja alikuwa anaitwa mzee kijaruba akalopoka nyerere kafa nikastuka nikawa naangalia juu kama ntaona ndege za kivita sababu tuliambiwa huyu kiumbe akifa vita lazima itokee
 
nakumbuka nilikua darasa la 3,huko uko rubale bukoba vijijini, nakumbuka mama alilia..na tukasikia kwenye redio kuna mmama kafa kutokana na mshtuko..picha ya mazishi tulikua tunalipia miamia ili kuiona,nilimaliza miezi miwili naogopa chumbani.. na habari zilivuma eti siku ya mazishi kule butiama lilitokea tetemeko la ardhi,na habari za kutokea vita baada ya kifo chake pia nilizisikia toka kwa watu wanao heshimika mtaani kwetu..hakika alikua BABA WA TAIFA.
 
Nakumbuka nilikuwa form four Tumaini sec Singida, majira ya kama saa nne hivi kipindi cha mwisho kabla ya break. Baada ya Mwl. Jacob kushusha kisawasawa revision ya somo la Agriculture. Ghafla kengere ngo ngo ngo wote parade, alikuwa ni Mwl. Mwanja ndiye aliye toa taarifa kuwa Mwl hatupo nae tena. Maandalizi ya graduu yakaisha hapohapo ambayo kwa kweli niliipania kwani nilikuwa na uhakika wa kupewa cheti cha sifa katika michezo {basketball} siku ya graduu, hivyo tulipewa kimya kimya mmoja mmoja ofisini. Toka siku hiyo sijawahi fanya graduu tena katika ngazi zilizofatia za elimu!
 
Sikumbuki nilikuwa kidato cha ngapi ila kengele ya parade ilipigwa tukakusanyika tulivyoambiwa tu kuwa baba wa taiga kafa kuna mwana mmoja alikuwa form six akapiga makofi kwa nguvu ... Watu wote wakamwangalia kwa mshangao
 
nakumbuka nilikuwa nacheza gololi na masela kitaa, kipindo nilikuwa na karedio kadogo aina ya philips ndo nikapata habari kupitia redio yangu
 
Back
Top Bottom