Ulikuwa wapi siku kifo J. Nyerere (baba wa Taifa) kinatangazwa?

Nilikuwa nipo form six pale Pugu Secondary na tukiwa bado darasani tukijisomea ndipo tulipopata habari za msiba wa mwalimu.Kwa kweli kila mtu alikuwa ktk huzuni kubwa sana.Baada ya hapo nakumbuka shughuli zote za masomo zilisimama kuanzia siku hiyo na baada ya siku chache tulifanya maandamano mpaka Karimjee hall.
 
Nilikuwa Form Sixx pale Tosamaganga Secondary na akina Lugano Mwampeta na Obeid Malima. Nakumbuka nilikuwa natoka kupiga ulanzi Junction basi Mkangwa akatoa TV ya shule ikawekwa DH watu tukawa tunakula news tu.
 
Sikumbuki nilikuwa wapi ila nakumbuka ilibidi tu cancel birthday party ambayo ilikuwa inafanyika weekend hiyo.
 
Nilikuwa SA schooling lakini I remember the whole day watching the footage of what was happening. Nilifurahi sana kuona SA actually showing live coverage, I was very touched. This is one of the very few men in the world I still have respect for. I really admire him and all hos ideology. He is a man of integrity na with Tanzania a man like him is yet to be born. I want to know more about his private life, alikua anapenda kunywa nini au kula nini just hw was his normal life
 
Nilikuwa Form Sixx pale Tosamaganga Secondary na akina Lugano Mwampeta na Obeid Malima. Nakumbuka nilikuwa natoka kupiga ulanzi Junction basi Mkangwa akatoa TV ya shule ikawekwa DH watu tukawa tunakula news tu.

hahahahahahaaaaa we jamaa balaa,yani toka Tosa adi Njiapanda ya Tosa?kisa ulasi?na utakuwa uliufuata adi Mseke wewe,kwani Ipamba uliona mbali?
 
I was in class teaching Geography form fours in their preps for national exams. By then I was working in rural Moshi.
 
Tarehe 14, 1999 Oktoba..Ndugu ulikuwa unafanya nini?
[video=vimeo;30555061]http://vimeo.com/30555061[/video]

[kutoka]
 
Nilikuwadarasa la sita enzi hizo wakati narudi shule wakati wa mchana ndio nikasikia Kengele inagongwa na mwalimu mkuu akaja kutangza na bendera ikawa inaning'inia nusu mlingoti.

kwahiyo mwaka huu umetimiza miaka 23
 
Nakumbuka nilikua darasa la5 shule moja ya boarding huko arusha.at that time tulikuwa porini tunakata kuni za shule,kuna baadh yetu walikuwa na viredio vidogo vile!ndo walitupa taarifa!it was so sad kwakweli.

manyara ranch au longido primary?
 
kumbe mwita na kelele zote ni mtoto wa juzi kati tu hapa
kumbe hata life hujaelewa inakwendaje ww na jamii yako
mm wakati huo nlishamaliza form six mkwawa najiandaa kuingia mliman.
Nilikuwa Form Sixx pale Tosamaganga Secondary na akina Lugano Mwampeta na Obeid Malima. Nakumbuka nilikuwa natoka kupiga ulanzi Junction basi Mkangwa akatoa TV ya shule ikawekwa DH watu tukawa tunakula news tu.
 
nakumbuka nllikuwa arusha baada ya kumaliza form six nkila raha kusubiria kuingia mlimani.wakati anafariki nlikuwa town center gafla daladala zote zikasimama watu wakapaki magari yao na kushuka kama vile kuna moto umetokea wakaanza kukaa vikundi kuzungumza
kuuliza ndio nkaambiwa nyerere katutoka
kweli ilikuwa huzuni kila mahali
cha kushangaza nyimbo za komba zikaanza kupigwa redioni na ITV wakati huo ndio kama tv ya taifaa nkashangaa nyimbo hizo kazitunga saa ngapi na zimerekodiwa lini kwa hivo alijua anakufa au alishakufa mapema wakaogopa kutangaza.
 
Masomoni Marekani
Nakumbuka ilikuwa siku ya jumanne niko kidato cha pili majira ya saa 4:30 tuko darasani na mwl wa Archtectural drawing ,ilikuwa ni mlinzi wa shule ndio alikuwa anazunguka kwenye corridor za madarasa na kusema nyerere ameaga duniani huku yuko na redio ikipiga wimbo wa taifa then akaja mkapa kulìhutubia taifa. Wewe ulikuwa wapi wakati huo ?
 
Back
Top Bottom