Ulikuwa unabebaje begi lako kipindi uko shule?

Ulikuwa unabebaje begi lako kipindi uko shule?

Nilibebea mfuko wa RAMBO, na ulipo chanika nikaamua kuanza kuyazungusha kwa duara kisha nachomeka kwenye mfuko wa nyuma kwenye kaptula
 
Mimi nilibeba begi kwa style zote sita, kutegemeana na siku nilivyoamka.


Style A nilikuwa nimechelewa shule, nikabeba begi upande mmoja nikakimbia.


Style B nilipokuwa nimebeba madaftari mengi, nililibeba mbele kama nimebeba mtoto mchanga.


Style C siku ambazo begi lilikuwa na vitu vichache, nilining'iniza begani na kuendelea na safari.


Style D siku ambazo nilikuwa nimechoka, nilibeba begi upande mmoja huku nikitembea kama nimebebeshwa deni.


Style E siku nilipojisikia mwanafunzi mwenye nidhamu, nilibeba begi mbele kwa heshima zote, kana kwamba naenda kupokea tuzo ya ufaulu.


Style F siku ambazo nilikuwa nimeamka na kiburi cha kitoto, nilirusha begi begani moja nikatembea kifua mbele kama meneja wa shule.


Kwa kifupi, mimi nilikuwa nabadilisha style kulingana na mood, siyo ratiba ya shule. Hata begi lenyewe lilikuwa halijui leo linaenda kuvaliwa vipi.
Hiyo B mvua ikinyesha unaweka mbele huku unajikinga na mwavuli.
 
Back
Top Bottom