Ulikutana na kituko gani ugenini

Niko mdogo tumetoka Mwanza kwa treni tumefikia Dar kwa ndugu wa kishua huko posta. Kutua tu mzigo nikapitilizishwa kuoga kwa kuswagwa, wengine wako kwenye ngazi hata ndani hawajafika. Baadaye ndiyo nikajafahamu kuwa walikuwa wananitoa kunguni na shombo ya treni.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nimecheka
 
Nilishikwa na tumbo la kuhara ghafla halafu choo kiko nje na hapo karibu na mlango wa choo wamekaa wa mama na mabinti wengine wako na majiko hapo wanapika
Nilijipa ujasiri nikaingia chooni kibabe ambapo mara baada ya kuvua nguo tu ili ilisikika Sauti kama ya ngurumo za radi yaani niliharisha mzigo wa maana kama kilo saba hivi ilikuwa kinyesi laini mithili ya ftari ya mihogo na viazi vitamu au grisi!
Ile nagusa koki ya bomba kumbe maji yamekatika!
Nilijikongoja nikavaa sarawili yangu kisha nikatoka nje ili niombe japo maji nisukume lile nyesi ambalo limeziba mpaka choo
Lakini cha ajabu ile ntafungua tu mlango nakutana na mamkwe huyu hapa anataka aingie!
Sikugeuka nyuma ilibidi nitoke nduki nikapitiliza nje ya geti na kuita boda nikaenda stendi kupanda gari kurudi Dom
Hata begi langu alikuja kulituma kwenye basi na suala la kujitambulisha kwao iliishia hapo hapo!
 
Kwetu huko… Uko sahihi πŸ’―
 
Chai imekolea chumvi na majani.

Kwahiyo ukapamda boda, ukaenda stendi, ukapanda bus hadi dom ila ukashindwa kuingia hata choo cha stendi kujisafisha?
 
Chai imekolea chumvi na majani.

Kwahiyo ukapamda boda, ukaenda stendi, ukapanda bus hadi dom ila ukashindwa kuingia hata choo cha stendi kujisafisha?
Mkuu nimefupisha story suala la kujisafisha nililifanya nilipofika stendi kuna choo cha kulipia
 
Nilienda kuangalia mashamba ya umwagiliaji. Sehemu mbali ya kutembea. Wakati wa kurudi nimechoka kiu imenishika. Nikapita nyumba moja ipo kando ya mfereji wa umwagiliaji. Γ‘ikawaomba wenyeji maji. Wakamtuma mtoto akachukue jagi ndani. Alipofika wakachota maji mferejini wakanipa! Hata nguvu za kugoma zikaisha.
 
Hatimaye Pdidy Kapata mrithi
 
daaaaah nime Cheka kwa sauti
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…