Ulijuaje mpenzi uliyenaye amekuacha?

Acha tu hawa viumbe lazima uwe nao wa akiba moja hata akizingua you dont care
Sure ndo maana Mungu amewafanya wamekuwa wengi kuliko sisi.. Kuna mmoja anafanyiwa engagement this week lakini kaniambia mpenzi wake anamapungufu kibao

Nikawa najiuliza kwanini amemkubalia yani sielewi hawa viumbe ni hatari yani hata siku moja usimpe mwanamke moyo 100% hiyo 40% inawatosha sana 60% iliyobaki waigizie tu.
 
Haya mambo Mimi yamenikuta siku chache zilizopitaa kitu nilichogundua hapa nimeshaachwa ila najilazimisha kwanza

1.mawasiliano ukimtumia text inavyojibiwa
Kikawaida sio kimahaba tena kama zamani

2.mkiongea kwenye anaongea kwa hasira hasira kila saa analalamika sijui hivi Mara vile mara mwanaume wewe hivi Mara vile

3.kitu kidogo mnagombana na ugomvi wake sio wa kitoto alafu kauli zake kila saa kama umenichoka niambie, Mara sikulazimishi kuwa na mie, Mara upendo wangu kwako umepungua,

4.maji yalivyonifika shingon nikalileta hili jambo jf comments nilizoshauliwa niachane na Huyo mwanamke ameshakuchoka na ukiendelea kumfata fata utaumia zaidi

5.mwisho wa siku niliamua tuu kupotezea niendelee na maisha mengine na demu nae akanipotezea baada ya week mbili alivyogundua nimempotezea alinitext usiku wa manane Mimi na wewe basiii sikumjibu chochote hata simu zake sikuzipokeaa

6.baada ya miezi sita kupita aliniatafuta kuniomba turudiane ila alikuwa kachakaaa kinoma noma
Ulimrudia tena Mkuu?
 
Haya Mambo acheni kabisa. Mi Nilimpenda Sana mpaka kuzaa 2 kids but unajua Nini... Nikiwa chuo naongeza kataaluma mawasiliano yakawa yanapungua ukiuliza kwa Nini sababu eti ubize anajisahau. Nisipopiga Mimi ndo nitolee bembeleza kuwa mawasiliano ni Muhimu hamna kitu. Dah ndo hivyo Tena mpaka tukajabreak up. Ogopa Sana kumpenda Mtu kwa Moyo wako wote. Nilishavurugwa mpaka leo sijielewi. Naona Kuna uzi Jamaa anasisitiza Sana kumpenda MUNGU Kwanza kwa Moyo wote ndipo umpende binadamu.
 
Mimi mawasiliano yalianza kupungua, Mwisho ikafika tamati nikaambiwa sio kusudi la Mungu tuwe pamoja, Yeye kapokea ufunuo huo kutoka Kwa Mungu. Sikuwa na kingine zaidi ya kumwambia Mapenzi ya Mungu yatimizwe, kama ni kweli namshukuru Mungu kama si kweli atajua Mwenyewe. Kumpenda nilimpenda na nilikuwa na Malengo naye makubwa
 
Mimi mawasiliano yalianza kupungua. Ukimtumia Msg anajibu P, Tantee,K . Mara Usinipigie Tuchat nk. Nikajua hapa Sina changu .

Siku moja nilitoka kuoga nikakuta Missed call na Sms moja muda huohuo kwamba ""Ninakupigia Simu upokei..? haya maisha mema" ile namtafta nijitete nakuta kaishanilamba Block
Malizia hii story mkuu
 
Nikimpigia simu jioni anasema ametoka kazini amechoka nijaribu (sio nimpigie na uhakika) asubuhi, nikimpigia asubuhi hapokei nikipiga mchana ananiambia alikuwa kwenye foleni asubuhi asingeweza kuongea na muda huu yupo kazini na boss wake yupo hivyo niwe mpole atapiga. Hapigi mpaka jioni, nikimtafuta ananiambia nisubiri afike home. Kwahiyo siku mbili nzima mzunguko ulikuwa huo nikaona huu ni ufala. Nikamlamba pini moja nzito mpaka kwenye social network kisha nikafuta namba zake zote na call history.

Nilikaa kama wiki tatu nikaingia kusoma spam messages nikakuta meseji zake nyingi akilalamika na ya mwisho akaandika asante. Makisudi nikampigia nikamuuliza "wewe nani, nimekuta meseji zako kwenye simu yangu." Akauliza kama nimeshafuta namba yake nikamwambia ajitambulishe sikumbuki. Akataja jina nikamwambia endelea na kazi za boss wako kisha nikakata.

Kalinifanya nikawa na moyo mgumu kwa mwanamke. Sasahv hata nikiamka asubuhi nikaambiwa naondoka najibu poa fanya chap.
 
Haaah moyo wako kama wangu kwa hawa viumbe
 
Naweza kupiga call ata 7 na asirespond ata akiona missed call
Muda akijisikia kupokea ukimuuliza anasema alikuwa busy na hajaona chochote

iliniwia vigumu kukubaliana na ukweli ila mwisho wa siku nilikaza Roho na kuibukia huku kwenye Uchakataji,

"MIMI NIJE KUPENDA TENA MWANAMKE LABDA NIFE NA KUFUFUKA TENA "
ulipigwa tukio
 
Haya mambo Mimi yamenikuta siku chache zilizopitaa kitu nilichogundua hapa nimeshaachwa ila najilazimisha kwanza

1.mawasiliano ukimtumia text inavyojibiwa
Kikawaida sio kimahaba tena kama zamani

2.mkiongea kwenye anaongea kwa hasira hasira kila saa analalamika sijui hivi Mara vile mara mwanaume wewe hivi Mara vile

3.kitu kidogo mnagombana na ugomvi wake sio wa kitoto alafu kauli zake kila saa kama umenichoka niambie, Mara sikulazimishi kuwa na mie, Mara upendo wangu kwako umepungua,

4.maji yalivyonifika shingon nikalileta hili jambo jf comments nilizoshauliwa niachane na Huyo mwanamke ameshakuchoka na ukiendelea kumfata fata utaumia zaidi

5.mwisho wa siku niliamua tuu kupotezea niendelee na maisha mengine na demu nae akanipotezea baada ya week mbili alivyogundua nimempotezea alinitext usiku wa manane Mimi na wewe basiii sikumjibu chochote hata simu zake sikuzipokeaa

6.baada ya miezi sita kupita aliniatafuta kuniomba turudiane ila alikuwa kachakaaa kinoma noma
woiiii
 
Mimi niliona mawasiliano yanapungua kuuliza akaniambia tutakuja kuongea. Asubuhi sa 11 niliamshwa kwa kibuti.

Kinachoniuma tupo ofisi moja na ss yupo likizo akirudi sijui maisha yatakuwaje ya kazi. Kufanya kazi na ex wako afu ulimpenda inaumiza.
Aiseee I feel you pole Sana

Tafuta manzi haraka sana jiweke itasaidia ku-upgrade brand yako
 
Aliamua kuwa kimya ghafla, ukimtafuta na kumuuliza shida nini, anasema hamna shida, nikiuliza mbona kimya anajibu itajisolve, nisipomtafuta hanitafuti, I was ghosted, after like 3 years nikaona anaolewa.
Nilichakaa
Duhh miaka mi3 umekaa unamsubiri mtu asiye onyesha kukujali ..I can't aise
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom